Taarifa kwa wanakinondoni - Mapokezi ya Mwenge kesho asubuhi Kigogo

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
TAARIFA KWA WANA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa ally hapi anawaalika wananchi na wakazi wote wa Wilaya ya Kinondoni kushiriki kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika kesho saa mbili asubuhi Kigogo.
Baada ya mapokezi, Mwenge wa Uhuru utafungua miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilayani humo na kisha mkesha wa Mwenge utafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe.
Nyote mnakaribishwa.
IMG_20170529_214511_166.jpg
 
Magufuli hebu liangalie na hili jipu hili,
Tunapoteza pesa na muda tu hapa.
 
Kama kuna kitu naelewa mantiki yake kama kitatumika vyema ni mbio za mwenge wa uhuru.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Aisee mbona umekosea Timing, usiku huu wanakinondoni tushalala. Ila watatuwakilisha walimu wetu wa msingi na sekondari.
 
Hivi Mwenge una faida gani hapa nchini na haswa mijini? Nipeni mimi niuwashe shambani kwangu nipambane na ngiri vizuri usiku.
 
Tafakarini vyema, una faida nyingi. Au kwakuwa uliasisiwa na mtu mweusi nchini?
 
Back
Top Bottom