Taarifa kwa vyombo vya habari

Taarifa kwa vyombo vya habari

Ondoka nenda kwenye chama kinachokufaa uiache CHADEMA. Na vitisho vyako ni sawa na kutisha jiwe upo hapo/
 
wanaotetea uongozi uliooza ndani ya chadema ni wale wanaonufaika na ufisadi huo
 
Sometime ago..........

Katika uchaguzi ule majina yaliyokuwa yakizungumzwa sana yalikuwa ni Ben Saanane, John Heche na Habib Mchange. Kampeni za hape na pale zilifanyika na waliokwenda kinyume na taratibu, kanuni na katiba ya CHADEMA hakika waliondolewa katika kinyang'anyiro kile na waliondolewa alikuwepo Habib Mchange aliyekutwa na kosa la kutoa rushwa kwa viongozi wa mikoa na wilaya kwa kutumia m-pesa na tigo pesa ambapo baada ya kuonyeshwa ushahidi usiyo na shaka ndani yake kutoka vodacom na tigo hakika alikubali na hatimaye kukosa sifa za kugombea.

Baada ya Mchange kuenguliwa aliweza kuwashawishi wagombea wengine akiwemo Saanane wajitoe kugombea na wamuunge mkono Mwampamba. Hakika Saanane alikubali na hatimaye wakaanza kufanya kampeni chafu dhidi ya Heche kinyume na taratibu, kanuni na katiba ya chadema kwa kufanya kampeni usiku kucha pasipo kujificha katika maeneo ya magomeni na hatimaye walipoitwa kwenye vikao halali vya chama na kuhojiwa walikiri makosa yao na hatimaye kukosa sifa za kuwa wagombea.

Baada ya hapo uchaguzi ulifanyika na hatimaye bwana John Heche aliibuka kuwa mwenyekiti wa BAVICHA.

Sintofahamu ilianza kujitokeza tokea siku hiyo ambapo wale wote waliokosa sifa za kugombea walianza kumpinga, kumchafua, kumtukana na kufanya mbinu zote za kumkwamisha bwana Heche katika majukumu yake ya kila siku pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA akiwemo mh Mbowe na Dr Slaa.

Hali hii iliendelea kwa muda mrefu kwa wasaliti hawa (masalia) kufanya vikao vya siri na kuapanga mikakati mbalimbali wakiongozwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa CHADEMA pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM kwa kuwapa pesa za kufanya usaliti wao akiwepo Nape Nnauye.

Baada ya nafsi kumsuta hatimaye bwana Ben Saanane aliamua kuwaambia wenzake waachane na usaliti maana haumbomoi bwana Heche bali unakibomoa pia chama na yeye hayuko tayari kuona hilo likitokea. Cha kushangaza ni kwamba wenzake hao waligoma na kuanza kumwita Saanane ni msaliti amesaliti kundi lao na wataanza kushughulikia na yeye pia.

Na kweli walianza harakati hizo za kumchafua Saanane pamoja na viongozi wa juu wa chadema na hata sms ambazo wasaliti hawa wamekuwa wakimtumia Saanane ninazo na akiniruhusu nitazileta hapa wana jamvi mzione.

Lakini baada ya kuongea na bwana Saanane aliniambia yeye ni jasiri sana na haogopi chochote na atasimamia ukweli maisha yake yote hata kama itamgharimu kifo. Nikamuuliza miongoni mwa wasaliti na waliokuwa wakiufadhili usaliti ni kina nani? Na yeye alinitajia kama ifuatavyo:-
1.Zitto Zuberi Kabwe.
2.Juliana Shonza
3.Habib Mchange.
4.Mwampamba.
5.Gwakisa
6.Nyakarungu.

Na wengine kwa sasa naomba nisiwataje kwa majina yao.

Kwa mujibu wa Saanane wasaliti hawa wameweza kuanzisha majina tofauti tofauti huku Jamii Forum na katika mitandao mingine kwa lengo la kutukana na kukashifu viongozi wa juu wa chama sana sana mh Mbowe, Dr Slaa na John Heche.

Na amenipa zaidi ya majina 20 ambayo wanayatumia vijana hawa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/370013-huyo-ndiye-ben-saanane-na-majibu-ya-zitto.html
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
‘TANGAZO RASMI LA WAPIGANIA DEMOKRASIA ‘WAUASI’
UTANGULIZI
......................

BRIGEDIA NYAKARUNGU natoa wito kwa wananchi wote walioumizwa na kulia wengine kukata tamaa wafahamu sasa tunachukua hatua kwa hawa Mahafidhina na mafisi wa mistu ya Nyamandicha.

Naamuru waliopenyezwa kukaimu nafasi za uongozi huko mikoani wajiondoe haraka kabla hatujawaondoa kwa nguvu ya umma,

KUHUSU MM2,


MM2 yupo na hakuna atakayemtaja mpaka mwenyewe atakapojitokeza siku yoyote ile kama ataona inafaa, lakini kwa heshima yake kwa vijana na chama na kuaminiwa na wahafidhina tumwache akae kati yao kwanza, lakini siku akijitokeza hamtaamini ka ndiye MM2, nadhani siku hiyo mtaamini ukweli wa haya yote.

BRIGEDIA NYAKARUNGU NATOA SIKU TANO (5) HADI TAREHE MOJA DECEMBER MWAKA HUU KUWATAKA VIONGOZI WALIONDOLEWA KUREJEA KWENYE NAFASI ZAO NA ENDAPO WATAPUUZA TUTAANZA MIKUTANO YA HADHARA KUWASIMIKA VIONGZOI WAPYA NA KILA KONA YA WATANZANIA WATAJUA JUA HILI!

Imetolea na BRIGEDIA NYAKARUNGU,
Mkuu wa kikosi cha kuisaka Demokrasia Chadema.

Nimeona waraka wako nimecheka sana, are you guys serious? yaani wewe kwanza umetokezea wapi? nilijua ushaondoka make unayotapika khs CHADEMA unatia kichefu chefu, by the way, msitutishe. Fanyeni mnachotaka nyie vifaranga wa Zitto
 
Wahafidhina watasema mengi na wataendelea kusema, reason why? Their days are numbered, wana tapatapa na they will die hard kubaki madarakani (wanao umia ni watu walio wa amini kuwa mtawa vukisha salama lkn mumeshindwa) ushauri wangu democracy iwe ya kweli ndani na nje ya chama.
 
Hivi "mirembe" hakuna nafasi za kutosha?
 
Huwa una ndoto mbaya ...maake naona umeshindwa hata kabla ya kuanza na Mungu akukemee kila utakacho fanya kiwe kinyume cha matakwa yako
 
Nyakarungu naona release yako INACHEKESHA NA KUKUDHALILISHA.Huwezi kushindana na chadema ya umma kaka,ZITTO Mwenyewe amepwaya licha wewe.nenda CHAUSTA Ukawe baunsa wao.
 
Hahahahahaa....kweli akili zako changanya na mkuu wa kaya
 
aisee hii post inaujumbe mkali sna kwa mwenye akili,ni mtu ambaye ameandika kwa hisia tena za kweli!!nimeamini chadema kuna tatizo kubwa sana na CCM watatumia upenyo huo huo
 
Yaani TISS inamaana kuna wavutabangi kiasi hiki, sasa hiki ni nini, alaf jaribuni kuwekeza mahala panapofaa sasa zitt kweli jamani
 
Back
Top Bottom