Taarifa kwa vyombo vya habari na wadau wote wa elimu

MTUNZA AMANI

Senior Member
Jun 2, 2012
187
21
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WADAU WOTE WA ELIMU
Ndugu wanahabari wote,kwanza nimshukuru Mungu kwa uhai na afya njema aliyonijalia hadi siku ya leo.

Ndugu zangu kwanza kabisa niwapongeze wanafunzi wote wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani yao. Hongereni sana.

Ndugu zangu, jana nilijaribu tu kuelezea azma yangu ya kutaka kuirudisha SHULE YA JANGWANI KATIKA HADHI YAKE, lakina nimepokea maoni mbalimbali wengi wakinitia moyo na wengine wakinibeza kwa kua na mawazo hasi. Lakini niseme tu sikukurupuka juu ya hilo.

KWANINI NIMEAMUA KUOMBA NIPELEKWE JANGWANI HIGH SCHOOL NA NINA NINI CHA PEKEE?

Ndugu zangu, mimi ni mwalimu kwa taaluma na siyo wito. Mtu anaweza kua na wito wa ualimu lakini asiwe na maarifa ya kutimiza majukumu ipasavyo,naomba niweke wazi kua nakwenda JANGWANI HIGH SCHOOL KAMA MWALIMU MWENYE WEREDI KAMILI NINAYEJUA JINSI YA KUPUNGUZA KIWANGO CHA UJINGA NA KUONGEZA KIWANGO MAARIFA KWA WANAFUNZI.

Ndugu zangu, rekodi zangu tangu nikiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu ninapenda kusoma na kujifunza njia bora za kufundishia na kujifunzia. Kilichotokea JANGWANI ndicho kinatokea kwenye shule nyingi za binafsi na serikali maana walimu wengi mbali na kutofundisha kwa weledi pia hawana utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali pamoja na majarida mbalimbali yanayohusu ulimwengu wa elimu na namna bora ya kumfundisha mwanafunzi. Mwalimu bora ni yule anayesoma vitabu mara kwa mara na tena vitabu vya waandishi mbalimbali na kujiimarisha kimaarifa.

Mwalimu bora ni yule anayewapenda wanafunzi wake kwa namna ya kuwafanya walipende somo lake na kipindi chake.

Mwalimu bora ni yule anayewatambua wanafunzi kwa majina na uwezo wao wa darasani ili aandae mbinu bora za kuwawezesha kuelewa somo lake kila mwanafunzi kulingana na uwezo wake.

Mwalimu bora ni yule anayewapatia mazoezi,majaribio na mitihani ya kutosha wanafunzi wake na kusahihisha ili kubaini ufaulu na mabadiliko ya wanafunzi kitaaluma na kujua jinsi ya kuwasaidia zaidi.

Mwalimu bora ni yule anayetoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na kuwatia moyo wanafunz wale waliopata alama hafifu katika majaribio na mitihani.

Mwalimu bora ni yule anayefanya vikao na mazungumzo mara kwa mara na wanafunzi wake ili apokee maoni na mapendekezo yao kwa lengo la kuwasaidia zaidi.

Mwalimu bora ni yule anayebaini tabia na nidhamu ya wanafunzi wake ili aweze kuwasaidia maana nidhamu bora ndoyo inayozaa matunda bora kitaaluma.

Mwalimu bora ni yule anayewapa muda wanafunzi wake kucheza michezo mbalimbali ili aweze kuwasaidia wanafunzi kupumzisja akili na kujenga afya bora.

Mwalimu bora ni yule anayewapa miongizo mbalimbali wanafunzi wake ili iwasaidie katika masomo yao na maisha yao.

Nugu zangu, nitareje ten ILA NAOMBA NIPELEKWA JANGWANI HIGH SCHOOL NAWAHAKIKISHIA SHULE ITAUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUFANYA VUZURI KITAALUMA.

Na MWL SADICK F MASILU
0652583409
 
Mwalimu bora ni yule anayewapa muda wanafunzi wake kucheza michezo mbalimbali ili aweze kuwasaidia wanafunzi kupumzisja akili na kujenga afya bora.
Michezo? Nimesoma Mzumbe secondary na kwa kipindi ambacho nimekaa pale, nimeshuhudia mpira wa miguu ukichezwa mara mbili tu kwa miaka yote ile miwili. Yani mechi moja kwa mwaka. Pale hapakuwa na michezo michezo. Ilikuwa ni msuli kwa kwenda mbele!
 
Masuala ya saikolojia ya elimu au sio
 
Walimu wana njaa kali halafu eti hapa kazi tu.
Hapa kazi tu bila kula.
 
Uzi wako utafutwa kwa kukiuka kanuni za JF

Umekuja na ID Fake lakini kwenye uzi umeweka Jina Halisi Na Namba Za Simu
CC Moderator
 
Walimu wana njaa kali halafu eti hapa kazi tu.
Hapa kazi tu bila kula.
MKOA WA KILIMANJARO UNAVYOUAIBISHA MKOA WA DARESALAM KITAALUMA.

Na Thadei Ole Mushi.

[HASHTAG]#Mkoa[/HASHTAG] wa Kilimanjaro pekee una shule 66 za Advance yaani mara sita ya shule zote za Mkoa wa Mtwara na Geita ambayo mtwara inashika nafasi ya kwanza na Geita ya Tatu, Kilimanjro ina Shule za Advance zaidi ya mara nane ya shule zote Lindi na karibu mara tatu zaidi ya shule zote za Morogoro na mara Mbili zaidi ya shule zote za Tanga.

Mikoa yote niliyotaja imeipita Kilimanjaro kwenye swala la Ufaulu ila kwangu Kilimanjaro ndio mkoa bora kabisa kielimu mwaka huu. Kwa wingi wa shule zake Kilimanjaro angalau ilipaswa kushindanishwa tu na mkoa wa Daresalam japokuwa Daresalam nayo imezidiwa kwa shule Sita na Kilimanjaro.

Kilimanjaro pekee imetoa division One 1,023 wakati anayeshika nafasi ya kwanza akiwa na one 172, wa pili one 95 wa tatu one 233 wa nne one 433 na wa tano one 435. Unaweza ukaona hilo Gape ni kubwa kiasi Gani. Anayemfuatia angalau kwa mbali sana Kilimanjaro ni mkoa wa Daresalam wenye One 747.

Trend ndio hiyo hiyo kwa division two Kilimanjaro inaongoza kwa idadi ya waliopata Two ikifuatiwa na Mbeya huku Divison Three Kilimajaro ikipitwa kidogo sana na Mkoa wa Daresalam. Haya kwangu ndio madaraja ya Ufaulu achana na four na Ziro.

[HASHTAG]#Nini[/HASHTAG] cha kujifunza hapa.

[HASHTAG]#Daresalam[/HASHTAG] na Kiliamanjaro ilikuwa na karibu idadi sawa ya watahiniwa Kilimanjaro ikiwa na watahiniwa 7,707 huku ikifuatiwa na Daresalam ambao walikuwa watahiniwa 6,663.

Kwa wingi idadi hiyo ya watahiniwa wa Mkoa wa Kiliamanjaro na perfomance waliyoionyesha ni dhahiri kuna factor ya ziada ya shule nyingine kujifunza.

Kilimanjaro naishindanisha na Daresalam kwa kuwa kwanza zote zina karibu uwiano sawa wa shule na uwiano sawa wa watahiniwa lakini matokeo yao ni Ardhi na Mbingu.

Daresalam shule zake nyingi hazili chakula cha mchana huku kwa shule zote za Advance Mkoa wa Kilimanjaro na hata za msingi na O level zikipata mlo wa mchana. Hii ni facto ya kwanza Kubwa mno na haipaswi kudharauliwa kama tunavyofanya.

[HASHTAG]#Shule[/HASHTAG] karibia Zote za advance mkoa wa Kilimanjaro wanafunzi wake wanalala shuleni huku kwa mkoa wa Daresala ikiwa ni karibia nusu kwa nusu. Yaani nusu wanalala na nusu wanarudi nyumbani.

Kimazingira Daresalam ingepaswa kuwa juu ya Kilimanjaro kutokana na access ya mambo mengi waliyoanayo katika mkoa wao. Hawa wana kila kitu kasoro tu mambo mawili niliyotaja hapo juu chakula na Baadhi kulala nyumbani.

Kwa bahati mbaya sana swala la chakula mashuleni si kipaumbele chetu. Swala la Boarding ni mpaka msichana abakwe au apate mimba ndio tuanze kuhamasiashana kujenga bweni.

[HASHTAG]#Unawezaje[/HASHTAG] kumfundisha mwanafunzi mwenye njaa? Atajifunza au atawaza chipsi za Kwa mangi?

[HASHTAG]#Unawezaje[/HASHTAG] kumdhibiti mwanafunzi mara baada ya masomo? Naamini hawa wa Dar karibia wote wana smart phone hawa, wanajichamganya na sisi jioni, watasoma saa ngapi?

NILIWAHI KUSEMA.

Mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wakifanya mambo bila Tafiti. Nikitolea mfano viongoz wa mkoa Wa Daresalam kuwa wanachapa kazi sana lakini impact ya kazi zao haionekani sana kutokana na kutokufuata misingi ya tafiti kwanza.

Nilipinga ujenzi wa Ofisi kwanza kama kweli tulihitaji ufaulu wa haraka rafiki yangu Fredy Dotto Mauki alinipinga moja kwa moja kuwa swala la Ofisi za waalimu ni kipaumbele. Nikamwambia hakuna significant relationship kati ya Ofisi na matokeo ya mwanafunzi. Yaani hakuna uhusiano wa moja kwa moja.... uhusiano uliopo ni mdogo sana.

Mwaka jana Daresalam haikuwa na Ofisi lakini ilikuwa ya 20 mwaka huu Ofisi zina mpaka kiyoyozi imekuwa ya 26. Hapa tuongee kitaalamu kumsaidia Mh [HASHTAG]#Makonda[/HASHTAG] apige hatua kubwa zaidi kwenye scandal hii ya Elimu katika mkoa wake inayomchafulia Taswira ya kazi zake.

Kama Daresalam wakigusa tu haya mambo mawili Chakula na Hostel hakika watatuletea tabu kubwa sana. Hawataki kusikia waache wakimbizane na Ofisi tu....

Zipo factor nyingine ila hizi ni za msingi kuliko yote.

[HASHTAG]#Hongereni[/HASHTAG] viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuanzia mkuu wa mkoa hadi staff za waalimu. Mmetisha sana. Na hongereni pia wazazi kwa kuendelea kukataa siasa Mashuleni na kuamua kuwekez haswa kwenye Elimu.

Unaruhusiwa kubisha....... Ngoja niingie class kufundisha tutakutana baadaye.

Ole Mushi.
0712702602
 
Jangwani unatakiwa WELEDI sio WEREDI... sasa hebu weka nukuu sawa wewe unataka kupeleka kipi kati ya hivyo?
 
Back
Top Bottom