Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uteuzi wa Wajumbe wa bunge maalum la Katiba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,984
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA
WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA



UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali

anapotoka mjumbe husika.


2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama

ifuatavyo:-

(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;

(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na

(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali

10 yanayohusika.


3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-


(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)

(ii) Taasisi za Kidini (20)

(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);

(iv) Taasisi za Elimu (20);

(v) Watu wenye Ulemavu (20);

(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);

(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);

(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);

(ix) Vyama vya Wakulima (20); na

(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).


4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.

5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu

Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

2

upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya

Mapinduzi Zanzibar.


6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.


7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi

mbalimbali ni kama ifuatavyo:

Fungua kiambatanisho..
 

Attachments

  • TAARIFA_KWA_VYOMBO_VYA_HABARI_WAJUMBE_BUNGE_LA_KATIBA_-_MAWASILIANO_2_en.pdf
    442.2 KB · Views: 85
hawa jamaa wamekosa busara kabisa....watanzania tuingie mitaani kudai KATIBA MPYA....udikteta uchwara lazima ufe!
 
Iweke vizuri hiyo taarifa, sielewi inalenga nini kimaudhui kwa sababu hiyo ni ya tarehe 07 Februari 2014.

Je! ndio kusema sasa Nov. 2017 mchakato wa Katiba Mpya unaendelea/unaanza au vipi?
 
Back
Top Bottom