Taarifa kwa Umma: Serikali haidaiwi na Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Wizara ya Fedha na Mipango inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 18/12/2019 yenye kichwa cha habari “Wastaafu EAC waibuka na mafao yao” ambapo taarifa hiyo ilieleza kuwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa mafao yao kwa miaka 40 iliyopita.

Wizara ya Fedha na Mipango inapenda kuufahamisha Umma kuwa imekwishawalipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mujibu wa “Hati ya Makubaliano (Deed of Settlement) iliyosajiliwa Mahakama Kuu tarehe 21/09/2005, kati ya Serikali na watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hati ya Makubaliano ilibainisha wazi mambo yafuatayo:-
  1. Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walikubali kufuta madai yao yote yaliyokuwa katika Kesi Na. 95 ya mwaka 2003, waliyoifungua Mahakama Kuu ya Tanzania;
  2. Serikali ilikubali kuwalipa wadai wote waliokuwa wamefungua kesi mahakamani na wengine wote waliofanya kazi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya Juni 30, 1977, na baada ya malipo hayo kufanyika, Serikali isingedaiwa tena;
  3. Serikali ilikubali kuwalipa wastaafu 31,831 jumla ya shilingi 117.0 bilioni kwa misingi ya stahili ya kila mmoja kulingana na taarifa ya kila mmoja wao kwenye jalada au nyaraka nyingine zilizothibitishwa. Aidha, Serikali ilikubali kuchukua gharama za mawakili wa wadai ili malipo wanayolipwa wastaafu hao yasikatwe chochote.
Zoezi la ulipaji mafao kwa ujumla lilikamilishwa mwaka 2009/2010 na serikali iliiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kushughulikia madai halali yatakayojitokeza, hususan yale yanayohusu mirathi kwa wahusika katika zoezi hili (case by case basis) kwa kutumia Sheria na taratibu zilizotumika katika zoezi husika. Hadi Desemba 2013 jumla ya wastaafu 31,788 kati ya 31,831, walikwishalipwa kiasi cha Shs 116,880,813,918.39 ikiwa ni sawa na asilimia 99.9 ya fedha zote zilizokubalika kulipwa.

Kwa maelezo haya Serikali kwa mara nyingine tena inarejea kusisitiza kuwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamelipwa haki zao zote kwa mujibu wa sheria na inatoa wito kwa wastaafu wote wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukubali kuwa malipo yaliyolipwa baada ya uhakiki ni halali kwa mujibu wa sheria.

Kwa kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa maslahi ya watanzania wote hususan wanyonge, hata mara baada ya kuwa imelipa mafao hayo, bado imefungua mlango wa kupokea na kuendelea kusikiliza madai ya mtu mmoja mmoja na kulipa baada ya kujiridhisha na uhalali wa madai husika.

Aidha, Serikali inawasihi sana wazee wetu hawa kujiepusha na upotoshaji na udanganyifu kutoka kwa wajanja wachache wanaotaka kujinufaisha kupitia migongo yao kwa kuendelea kujidai kwamba wao wana uwezo wa kusimamia madai yao ambayo hayapo.
 
Mbona kiwango ni kidogo sana wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mishahara ya zamani ni kiduchu sana. Kuna mtumishi wa umma mwaka 1995 alistahafu na kiinua mgongo hakikuzidi 1M.
Waliozidi hicho kiasi ni wachache, wazee wengi wa EAC hawakuwa wasomi.
Wengine darasa la nne tu na kazi zao za chini kama ukarani, ufagizi na ulinzi.
Hali ni mbaya sana hiyo mishahara yao.

Ukumbuke kipindi cha Nyerere watanzania wengi walikuwa na elimu ndogo mno.
 
Mishahara ya zamani ni kiduchu sana. Kuna mtumishi wa umma mwaka 1995 alistahafu na kiinua mgongo hakikuzidi 1M.
Waliozidi hicho kiasi ni wachache, wazee wengi wa EAC hawakuwa wasomi.
Wengine darasa la nne tu na kazi zao za chini kama ukarani, ufagizi na ulinzi.
Hali ni mbaya sana hiyo mishahara yao.

Ukumbuke kipindi cha Nyerere watanzania wengi walikuwa na elimu ndogo mno.
Mnadhimu wa Jeshi enzi za kina Gen Sarakikya yeye kwny mahojiano na gazeti la mwananchi alisema analipwa Tsh.25,000(Elfu ishirini na tano tu) kwa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnadhimu wa Jeshi enzi za kina Gen Sarakikya yeye kwny mahojiano na gazeti la mwananchi alisema analipwa Tsh.25,000(Elfu ishirini na tano tu) kwa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzuri wa jeshi kama amtu amefikia ngazi au cheo cha ujenerali nafikiri anahudumiwa na serikali mambo mengi hadi siku yake ya kufa.
Lakini bado huo mshahara au posho ndogo sana kwa hadhi yake na kwa maisha ya sasa.
Nakumbuka kuna watumishi walikuwa na miaka zaidi ya 30 serikalini miaka ya 90's lakini walikuwa na mshahara kati ya 30,000/- hadi 60,000/- na hao walijiendeleza elimu kufikia kidato cha nne.
 
Hahaha ccm wanaondoa ajenda ya kuwalipa wastaafu wa iliykuwa EAC, uchaguzi umekaribia.
 
Mnadhimu wa Jeshi enzi za kina Gen Sarakikya yeye kwny mahojiano na gazeti la mwananchi alisema analipwa Tsh.25,000(Elfu ishirini na tano tu) kwa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli! Hawa wanalipwa 80% ya mshahara anaolipwa generali aliyepo kazini na stahiki za posho, wageni na usafiri wanapata sawia! Hawana mafao ya kila mwezi kwani sio wanachama wa mashirika ya kijamii yanayohusiana na mafao!
 
Yeye alikua ni kanali na alisema Gen.Sarakikya analipwa Tsh.50,000(elfu hamsini) kwa mwezi,sasa kama wewe unaweza kubishana na Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa Jeshi haya.

Habari hii hapo chini.

Sio kweli! Hawa wanalipwa 80% ya mshahara anaolipwa generali aliyepo kazini na stahiki za posho, wageni na usafiri wanapata sawia! Hawana mafao ya kila mwezi kwani sio wanachama wa mashirika ya kijamii yanayohusiana na mafao!

Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Ameen Kashimir, ameilalamikia serikali kwa kutotambua mchango wake licha ya kuinusuru serikali wakati wa maasi ya jeshi hilo ya mwaka 1964.

Kadhalika, alisema pamoja na mchango wake kwa taifa mpaka sasa analipwa Sh. 22,000 kwa mwezi kama mafao ya uzeeni.

Kashimir ambaye alikuwa afisa wa kwanza kupata Kamisheni Jeshi la Tanganyika Rifles, kabla ya uhuru na baada ya uhuru, alikuwa Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa jeshi hilo ambaye alifanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwafundisha wanajeshi 30,000 kwa ajili ya kuanzisha jeshi jipya.

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam wakati alipohojiwa na waandishi wa habari wakati wa uwasilishwaji wa video kuhusiana na historia ya maisha yake.

Alisema mchango wake katika jeshi umesahaulika licha ya kwamba umesaidia kujenga msingi wa jeshi kutoka askari 50 waliobakia baada ya waasi na kuanzisha jeshi jipya la wanajeshi 30,000.

Alisema jeshi hilo lilikuwa imara na lilionyesha uhodari wake katika vita dhidi ya Idi Amini wa Uganda.

Kashmir alisema, yote waliyoyafanya yamesahaulika. "Kwa mimi binafsi nilibaki na cheo cha Kanali wakati nilitakiwa kuwa Meja Jenerali sasa hapa labda kulikuwa na ubaguzi wa aina fulani au sijui ni nini lakini nadhani serikali inatakiwa kuangalia suala la maofisa wa zamani."

"Kwa mfano Jenerali Mstaafu Mrisho Sarakikya mafao anayopata ni Sh. 50,000 kwa mwezi na mimi napatiwa Sh. 22,000 na kama nisingekuwa na akili timamu na nguvu ningekuwa maskini na kuomba omba," anasema.

Aliomba serikali ifikirie upya waliojitolea na kusaidia kujenga jeshi linaloonekana sasa wakumbukwe katika michango yao.

Aidha, alisema vijana wanatakiwa kuiga mfano wao kwa kuwa walikuwa ni wazalendo na nchi yao.

Alisema kuonyeshwa kwa video hiyo kutasaidia vijana kuelewa kazi walizokuwa wakizifanya katika kujenga nchi.

Alilishauri jeshi kuwa la kisasa lenye silaha za aina mbali mbali zinazotumia teknolojia mpya.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa chuo kikuu, Profesa Issa Shivji, alisema mchango wa mtu binafsi unakumbusha suala la historia na kwamba ni jambo zuri kukumbukwa kwa Kanali Kashmir kwani baada ya kutokea waasi wa jeshi mwaka 1964 ni nchi pekee Afrika ilivunja jeshi lake na kuunda jeshi jipya.

Alisema hatua hiyo ni muhimu kwa upande wake kwa kuwa ilikwenda sambamba na kizazi kile kujenga utaifa.

Profesa Shivji alisema wanapoangalia michango ya watu wanatakiwa kujikumbushia historia zao kwani ilikuwa na dira kwa nchi hivyo ni muhimu wakakumbukwa.


CHANZO: NIPASHE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alitumia Fedha za Wazee hawa kwenda kumchokoza Iddy Ameen ili tu amuweke kibaraka wake Museven ambae leo hii Waganda wanamlaani kichizi
 
Back
Top Bottom