Taarifa kwa umma: NEC yaviliza vyama vya siasa kwa kutoa taarifa hii

inasikitisha sana, yaani wengine watukaneeeeweeeeee, wazidishe na muda wa kampeni,

tume kimya kabisa,

wengine wakifanya shuguli za kuwatembelea wapiga kura wao,

tume ina tunga sheria na kuja na mikwara. Dah na yaona kwa mbaaaaaali ya kenya kwa mtindo uhu, amakweli kivuitu tutamwona tena hapa,
 
wananhci wote tujiandae na kupambana na hii tume ya kifisadi iliyowekwa mfukoni na serikali ya CCM, Lubuva from being a good Judge to ccm follower
, na wewe Kailima Ramadhan umewekwa hapo haraka haraka na Kikwete ili uekeleze ila unachoambiwa kaa msukule ila sio tume huru

Jiongelee wewe na kama kupambana tangulia mbele na familia yako!
 
Mikutano yote ya kampeni itaanza saa 2:00 asubuhi na kuisha saa 12:00 jioni!!!!! Hii tume kama iko huru, tungeshasikia kuhusu CCM waliokwenda hadi saa 12:40 jioni, labda wanaandaa waraka/tamko juu ya hilo.
 
Mikutano yote ya kampeni itaanza saa 2:00 asubuhi na kuisha saa 12:00 jioni!!!!! Hii tume kama iko huru, tungeshasikia kuhusu CCM waliokwenda hadi saa 12:40 jioni, labda wanaandaa waraka/tamko juu ya hilo.

mkuu hatuna tume hapa, bali tuna kamati ya ushindi ya chama cha mapinduzi,
 

View attachment 280602


Ukawa and CCM.jpg
 
Humu ndani kuna watu hawatumii akili kwel kwel? Hizi kanuni zilipitiwa na vyama vyote na kukubaliwa na wote sasa UCCM unakuja vipi hapa??

Mnalalamika kama wafa maji? Kushinda ni lazima mpende msipende Raisi ni Magufuli

UCCM unakuja pale CCM wanapokiuka muda wa kampeni (saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni) lakini tume wala polisi kimya. Wakati huohuo CHADEMA mgombea wake wa uRais anatembea kuonana na wananchi (maeneo ambayo hayajaainishwa katika ratiba) tume na polisi tayari wameshaliongelea hilo. Hapo mkuu huoni kweli? hebu jifanye huru bila kuegemea upande wowote kama nilivyohuru mimi katika hizo red bolded utaona tu.
 
Hii tume maandazi kweli Magufuri na wenzake walipofanya mkutano mpaka saa 12:30 usiku barua haikutoka wala vifungu havikutolewa achilia mbali hata kwenye hii barua wametoa mfano wa mgombea wa wakimlenga Lowassa tu kwanini wasitolee mfano Mama samia kwenda hospital au magufuri kufanya mkutano hadi saa mmoja. Mimi nilikuwa naimani na magufuri ila kwa uonevu huu nimejisikia nimeanza kumzimia Lowassa na ukawa...aisee sijui huyu babu ana nini...nimemmpendaje gafla...jana kanishika mkono Tandale yaani sikutegemea kama naweza kukutana na hawa wagombea wa urais huku vichocholoni kwetu...anasema mara ya mwisho kupita barabara ya tandale ni kipindi kile akiwa waziri wa ardhi..hakutegemea kukuta khali kama ile ile...hakuna maendeleo hata kidogo
 
[h=2] [/h]


Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 pamoja na Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015. Kampeni za Uchaguzi huanza siku moja baada ya uteuzi na huisha siku moja kabla ya siku ya kupiga Kura.
Kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa Kampeni zinafuata muda, Kanuni ya 39 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na Maadili ya Uchaguzi kifungu cha 2.1 (c) inaelezwa Mikutano yote ya Kampeni itaanza saa 2:00 asubuhi n kuisha saa 12:00 jioni.
Kanuni ya 40 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inasema, Mkurugenzi wa Uchaguzi kabla Kampeni za Uchaguzi wa Rais hazijaanza atavitaka vyama vya Siasa kuwasilisha mapendekezo ya ratiba za Mikutano ya Kampeni, na kanuni ndogo ya (3) inasema, lazima Chama kiwasilishe mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ikionesha tarehe, muda, Mkoa na Wilaya ambapo Mkutano utafanyika.
Aidha, kanuni ya 41 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inaeleza kuwa iwapo Chama cha Siasa kitahitaji kufanya mabadiliko ratiba au eneo la Mkutano wa Kampeni, kitawasilisha mapendekezo yakiambatishwa na sababu za kutaka kufanya mabadiliko kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambaye kabla ya kufanya marekebisho katika Ratiba husika ataitisha Mkutano wa Kamati ya Kuratibu Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi wa Rais inayojumuisha vyama vyote vyenye wagombea katika nafasi hiyo ili vikubali au kukataa mabadiliko yanayopendekezwa.
Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni tajwa hapo juu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivialika Vyama vya Siasa vyenye Wagombea wa kiti cha Rais kuwasilisha mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ya Rais. Mnamo tarehe 22


1


 
Chonde chonde nec, tumieni busara na ubinadamu. Angalieni wananchi walivyochoka na chama kilicopo madarakani. Hizo sheria zote hawaelewi, wanasubiri tu agizo. Umimilivu ukikosekana, hata nyie hapo Posta mtakosa pa kukaa. Mungu ibariki Tanzania na tupe umumilivu utoepushe na kikombe hiki.
 
Naona Lowassa hata Kanisani watamzuia kwenda, maana nako kuna kusanyiko
 
Back
Top Bottom