Taarifa kwa umma kuhusu tuhuma za kula ada za watoto

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
TAARIFA KWA UMMA
Yah: TUHUMA ZA KULA ADA ZA WATOTO
UMOJA WA WANAUME WENYE KIPATO CHA KATI (UWAWEKIKA)

Tumesikitishwa na kauli za upotoshaji, kashfa, kejeli na matusi, dhidi ya wanachama wake kwa ujumla.
Tunalaani vikali maneno ya:

"Kizazi kilichokula ada wakati kinasoma, kimekula ada tena wakati kikisomesha."

Kwa kuwa maneno haya yamejaa dharau, kutusimanga na kutudhalilisha. Kwamba kukosa kwetu elimu kubwa kunahusishwa na utukutu wa kula ada.

UWAWEKIKA tunapenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba:

"Pesa tulizokuwa tulipie ada kwa watoto wetu, tulitumia katika mazingira ya dharula yaliyojitokeza kutokana na COVID-19."

Katika mazingira kama yale, mlitaka tutunze ada badala ya kuokoa uhai wa watu wetu? Mpo timamu kichwani kweli?
Sisi kwa kauli moja tunasema, tulitumia pesa zile kusafirishia watoto kwenda vijijini kwa bibi zao. Na pia pesa hizo hizo tulitumia kununulia akiba ya vyakula.

Mwisho mkae mkijua kuwa pesa ikiwa mfukoni kwa mzazi, hakuna mwenye mamlaka wa kuita pesa hiyo ni ada. Bado itaitwa pesa ya matumizi tu. Na ada ni sehemu ndogo sana ya matumizi ya familia.


Imetolewa na:
Dk Levy (Escobar)
Msemaji wa Umoja wa Wanaume Wenye Kipato Cha Kati.
(UWAWEKIKA)
Dar es Salaam.
 
Kipindi kile sie tuliosoma sek. za serikali za kutwa miaka ya 90 ada ilikuwa elfu 5 kwa mwaka. Tulikula sana mpaka ilifika kipindi kupandikiza (baba feki).

Unamchukua unaendanaye shule anakupiga mitama na makofi ya kufa mtu mbele ya walimu hadi walimu wanapata kibarua cha kumbembeleza akuachie asije akakuvutisha mbele yao na kumsihi alete siku nyingine yeye mwenyewe na wewe ufanye "pepa".
Jioni ukirudi home unamtoa kidogo huyo (baba-feki)------unakuwa umesolve msala bila "baba-og" kujua kilichojiri !
 
Kipindi kile sie tuliosoma sek. za serikali za kutwa miaka ya 90 ada ilikuwa elfu 5 kwa mwaka. Tulikula sana mpaka ilifika kipindi kupandikiza (baba feki) .
Unamchukua unaendanaye shule anakupiga mitama na makofi ya kufa mtu mbele ya walimu hadi walimu wanapata kibarua cha kumbembeleza akuachie asije akakuvutisha mbele yao na kumsihi alete siku nyingine yeye mwenyewe na wewe ufanye "pepa".
Jioni ukirudi home unamtoa kidogo huyo (baba-feki)------unakuwa umesolve msala bila "baba-og" kujua kilichojiri !
 
Hela ya ada huwa hairudi,unasema ngoja nitoe twenty kisha nita ireplace ndo imetoka hiyo.
 
Back
Top Bottom