SoC03 Taa ya umeme inavyoweza kutokomeza malaria kwa kunasa na kuua mbu

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 18, 2022
24
47
TAA YA UMEME INAVYOWEZA KUZUIA MALARIA KWA KUNASA NA KUUA MBU

Utangulizi
Malaria ni miongoni mwa magonjwa ambayo yamekuwa tatizo kubwa na umekuwa ukiuua watu miaka hadi miaka. Malaria husababishwa na mbu jike ajulikanaye kama Anofelesi. Katika nchi zinazoendelea malaria ni ugonjwa unaosababisha vifo vingi hususani kwa watoto chini ya miaka 5, wamama wajawazito, vijana, wazee na waathirika wa magonjwa kama HIV/AIDS, TB n.k. Kuna sababu nyingi ambazo zinafanya ugonjwa huu uendelee kuenea na kuwepo miaka yote ambazo ni umaskini, elimu, muingiliano wa watu na mabadiliko ya hali ya hewa (ongezeko la joto).

Taa mbuu.png


Miongoni mwa sababu zinazopelekea kushindwa kudhibiti/kutokomeza ugonjwa wa malaria barani Afrika na nchi zinazoendelea kama Tanzania ni kwamba Afrika ni nyumbani kwa wadudu hususani mbu ambao ni Anopheles gambiae na An. funestos.

TEKNOLOJIA YA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA.

Njia nyingi zimetumika kupambana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na kupulizia dawa milango, madirisha na majumbani ili kuua mbu. Pia ugawaji wa vyandarua na kutibu ugonjwa wa malaria. Ifuatayo ni njia ya kiteknolojia itakayoweza kudhibiti maambukizi na kuenea kwa mbu maeneo mbalimbali kama majumbani na maofisini.

Matumizi ya sumaku kwenye taa za umeme (Rejea Kiambatanisho katika andiko hili).
Kwa nchi nyingi zinazoendelea kwa sehemu kubwa umeme umeanza kufika mpaka vijijini kitu ambacho kinavutia matumizi ya taa za umeme majumbani. Taa hizi zitatengenezwa maalumu kwa ajili ya umeme wa kawaida lakini wakati huo huo zikiwekwa sumaku kali yenye uwezo wa kunasa mbu popote pale alipo chumbani, sebuleni na bafuni umbali wa mita 5-10. Kila chumba kitatumia taa za umeme ambazo zina uwezo wa kutoa mwanga na wakati huo huo zikinasa na kuua mbu wote waliomo chumbani na wale watakaoingia.

Vilevile, taa hizi zitafungwa kwenye madirisha au milango kwa nje ambapo zitakuwa na uwezo huohuo wa kunasa mbu wote wanaoingia ndani na kuwaua. Kadhalika, maeneo ya jikoni, chooni, bafuni na ofisini kutakuwa na taa hizi kwa ajili ya kudhibiti na kuua mbu wote katika eneo hilo. Changamoto iliyopo sasa hususani kwenye matumizi ya vyandarua ni kwamba vyandarua hutumika vyumbani tu wanakolala watu lakini sehemu zingine ambazo mbu wanapatikana vyandarua havipo mfano maofisini, vyooni, bafuni, jikoni, kumbi za starehe, kanisani, misikitini, bar, sokoni, mahotelini, migahawani, shuleni, vyuoni, stendi na maeneo ambayo taa za umeme zipo. Maeneo hayo yote niliyoyataja yanaweza kufungwa taa hizi ili kutokomeza mbu wa eneo hilo na watu wakawa salama kabisa.

Faida ya ubunifu huu wa kiteknolojia

1. Kutokana na usumbufu mkubwa wanaopata watu kutokana na mbu itakuwa ni rahisi mtu kununua taa ambayo ina uwezo wa kunasa na kuua mbu hivyo basi bidhaa hii zitapata soko kubwa kwa kuwa taa zitakuwa zimeongezwa thamani kufanya kazi zaidi ya moja.

2. Ubunifu huu utachochea matumizi ya umeme vijijini na mjini na hivyo serikali itawajibika kupeleka umeme ili pamoja na malengo mengine uweze kutatua changamoto zaidi ya moja ambayo ni nishati na ugonjwa wa malaria.

3. Maeneo yote ambayo watu hukusanyika kama vile maofisini, vyooni, bafuni, jikoni, kumbi za starehe, kanisani, misikitini, bar, sokoni, mahotelini, migahawani, shuleni, vyuoni na stendi ambayo kwa sasa hayatiliwi manani kama kichocheo kikubwa cha kuenea kwa malaria yatafungwa taa kwa ajili ya mwanga wakati huo huo kwa ajili ya kuua na kunasa mbu.

4. Ubunifu huu utamfanya kila mtu kuwajibika kwa kuwa hakuna mtu atakayekubali kung’atwa na mbu. Kwa maana hivyo basi, kama ambavyo watu wananunua taa kwa matumizi ya kawaida ndivyo watakavyonunua taa kwa ajili ya kutokomeza mbu.

5. Kuinua uchumi wa nchi na ajira kwa makundi katika jamii especially vijana. Ukiachilia mbali kutokomeza ugonjwa wa malaria taa hizi zitakuwa ni sehemu ya biashara na watu watakuwa na uwezo wa kuziuza na kujipatia kipato.

6. Taa za umeme zitaweza kufika maeneo ambayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha maambukizi ya malaria na ambayo hayakuwahi kufikiriwa kama chanzo cha ugonjwa huu mfano stendi za mabasi, stersheni, vyombo vya usafiri, sokoni, misikitini, makanisani, saluni, bar, kumbi za starehe, jikoni, migahawani na maofisini ambako kote huku mbu ni wengi sana na wanafanya maambukizi ya malaria ambako taa za umeme zipo pia.

7. Kuyafikia makundi yote bila ubaguzi. Makundi yote yatanufaika na ubunifu huu kama vile watoto, vijana, wazee na wanawake kwa kuwa hakuna mtu ambaye atakuwa yuko exchuded. Kama ilivyo matumizi ya umeme kwa rika zote ndivyo itakavyokuwa katika matumizi ya taa hizi.

8. Utunzaji wa mazingira - kumekuwa na ukataji miti, nyasi na uoto wa asili sehemu nyingi kama sehemu ya kudhibiti mazalia ya mbu. Kupitia ubunifu huu sehemu zenye misitu au vichaka zinaweza kufungwa taa za kunasa na kuua mbu na bado mazingira yakabaki kama yalivyo.

9. Kuendeleza ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia katika kutatua changamoto zinazoikumba dunia kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals – SDGs).
10. Kutokomeza ugonjwa wa malaria katika nchi zinazoendelea na hivyo kuongeza uzalishaji wenye tija katika jamii kwa kuwa jamii zitakuwa na afya njema.

Nini kifanyike?
Ili ubunifu huu uweze kufanya kazi inatakiwa kampuni (ambayo inajihusisha na masuala ya umeme yenye teknolojia ya hali ya juu) izalishe wazo hili la kutengeneza taa (bulb) za umeme ambazo zitakuwa na uwezo wa kunasa na kuua mbu. Baada ya hapo taa zifanyiwe majaribio zianze kuuzwa au kusambazwa kwa watu kwa ajili ya matumizi. Sumaku ya kunasa mbu ni muhimu na ili kupnguza gharama za uzalishaji na mlaji wa mwisho ambaye ni mwananchi serikali na wadau wote watoe ruzuku na ufadhili ili wananchi wagawiwe taa hizi bure au kwa gharama nafuu.

Hitimisho
Nawashukuru sana wadau wote pamoja na jopo zima la JamiiForums kwa kunipigia kura kwenye shindano la mwaka jana na kuibuka mshindi wa pili. Mungu awabariki sana nyote. Naombeni msinichoke tena kama utaguswa na andiko langu hili usiache kunipigia kura kwa mara nyingine kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa vote.
 
Back
Top Bottom