TAA: Hakuna ajali ya ndege ziwa Victoria, yasema ni zoezi la utayari

Wadau na nyie mmeona. Kuna ndege imeanguka ziwa Victoria.

===
Ndege Ndogo ya Abiria imeanguka na kuzama Ziwa Victoria. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wamefika eneo la tukio na kutoa msaada kwa abiria walikuwamo kwenye ndege hiyo.

====
UPDATE
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mussa Mbura amesema hakuna ajali ya ndege leo kwenye Ziwa Victoria Jijini Mwanza bali kilichofanyika ni mazoezi ya utayari.

Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu, Mussa Mbura amesema yafuatayo "Haya ni mazoezi ya kujiweka tayari ambayo tumeendelea kuyafanya, kama Mamlaka za Viwanja vya Ndege miongozo inatutaka tuwe tunafanya mazoezi ya mara kwa mara kuhakikisha Watu wetu wapo tayari pale inapotokea tatizo kila Mtu kwenye eneo lake awe tayari"

"Serikali ina Airport inazoziendesha takribani 58, haya mazoezi yanatakiwa yafanyike kwenye Airport zote hizo ndio maana mnaona series ya mazoezi kwenye Airport tofauti ndio maana tumefanya Kahama na leo tumefanya hapa Mwanza, kwahiyo hakuna ajali halisi leo kama inavyoripotiwa ni mazoezi tu ya utayari"

Jamani! Jamani!
 
Back
Top Bottom