Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
TAA HAKIKUWA CHAMA CHA KUSHUGHULIKA NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAAFRIKA WA TANGANYIKA
Abdul Sykes alikuwa na fikra ya kuunda chama cha siasa toka yuko Burma wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 – 1945) na alipoingia katika uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee.
Wajumbe wengine walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Churembo, Steven Mhando na John Rupia.
Nia ya kuunda hii kamati ilikuwa kuunda chama cha siasa.
Itamshangaza mtu yoyote kusikia kuwa Nyerere aliyepokelewa ndani ya TAA na Abdul Sykes 1952 tena wakati huo Abdul akiwa Kaimu Rais na Katibu TAA, awe Nyerere ndiye aliyemshawishi Abdul na wenzake katika uongozi wa TAA ati wavunje TAA waunde TANU.
Chembelecho Mzee Msekwa, ''wavunje chama chao.''
Mzee Msekwa anazungumza historia ambayo yeye haijui.
Ukweli ni kuwa kulikuwa na mazungumzo kabla na nyuma sana kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuhusu kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Abdul alishaanza mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia achaguliwe Rais wa TAA na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Kuna mengi hapa hadi Nyerere akaja kuchaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka wa 1953 na Abdul Sykes akawa makamu wake katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo.
Kikao cha kumpa Nyerere uongozi wa TAA kilifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe katika miezi ya mwanzoni 1953 kati ya mwenyeji Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ally Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama ambacho aliasisi baba yake Abdul mwaka wa 1933 na chama hiki ndicho kilichotoa wanachama na viongozi wa mwanzo wa TANU mwaka wa 1954.
Itoshe tu kufahamu hafla ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955 ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Kwa kumalizia ningependa kumweleza Mzee Msekwa ni chama gani kilikuwa kinashughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika katika serikali ya kikoloni.
Chama hiki hakikuwa TAA.
Chama kilichoshughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika kilikuwa kinaitwa, ''Tanganyika Government Servant Association,'' (TAGSA).
Chama hicho kiliasisiwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na watumishi wake Waafrika ili kuboresha huduma na kuendeleza maslahi na ustawi wa waajiriwa Waafrika.
Katika kipindi hiki cha mwanzoni mwa mwaka wa 1950 viongozi wa TAGSA walikuwa Thomas Marealle kama Rais na Ally Sykes Katibu.
Rashid Kawawa, Dr. Wibard Mwanjisi, Steven Mhando, Dr. Michael Lugazi walikuwa wanakamati na hawa wote walihusika sana katika kuunda TANU na wakiishi na fikra ya kuunda chama cha siasa kudai uhuru wa Tanganyika wala hawajasikia jina la Julius Nyerere.
Huu ndiyo ukweli wa historia ya TANU.
Kujaribu kukwepa ukweli huu matokeo yake ni kuvuruga hata hiyo historia yenyewe ya CCM.
Picha:
Chief David Kidaha Makwaia
Abdul Sykes kulia na Ally Sykes Burma Infantry, 6th Battallion, Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945)