TAA hakikuwa chama cha kushughulika na maslahi ya wafanyakazi waafrika wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,081
TAA HAKIKUWA CHAMA CHA KUSHUGHULIKA NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAAFRIKA WA TANGANYIKA

Abdul Sykes alikuwa na fikra ya kuunda chama cha siasa toka yuko Burma wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 – 1945) na alipoingia katika uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee.

Wajumbe wengine walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Churembo, Steven Mhando na John Rupia.

Nia ya kuunda hii kamati ilikuwa kuunda chama cha siasa.

Itamshangaza mtu yoyote kusikia kuwa Nyerere aliyepokelewa ndani ya TAA na Abdul Sykes 1952 tena wakati huo Abdul akiwa Kaimu Rais na Katibu TAA, awe Nyerere ndiye aliyemshawishi Abdul na wenzake katika uongozi wa TAA ati wavunje TAA waunde TANU.

Chembelecho Mzee Msekwa, ''wavunje chama chao.''

Mzee Msekwa anazungumza historia ambayo yeye haijui.

Ukweli ni kuwa kulikuwa na mazungumzo kabla na nyuma sana kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuhusu kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Abdul alishaanza mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia achaguliwe Rais wa TAA na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Kuna mengi hapa hadi Nyerere akaja kuchaguliwa kuwa Rais wa TAA mwaka wa 1953 na Abdul Sykes akawa makamu wake katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo.

Kikao cha kumpa Nyerere uongozi wa TAA kilifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe katika miezi ya mwanzoni 1953 kati ya mwenyeji Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ally Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama ambacho aliasisi baba yake Abdul mwaka wa 1933 na chama hiki ndicho kilichotoa wanachama na viongozi wa mwanzo wa TANU mwaka wa 1954.

Itoshe tu kufahamu hafla ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955 ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Kwa kumalizia ningependa kumweleza Mzee Msekwa ni chama gani kilikuwa kinashughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika katika serikali ya kikoloni.

Chama hiki hakikuwa TAA.

Chama kilichoshughulika na maslahi ya wafanyakazi Waafrika kilikuwa kinaitwa, ''Tanganyika Government Servant Association,'' (TAGSA).

Chama hicho kiliasisiwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na watumishi wake Waafrika ili kuboresha huduma na kuendeleza maslahi na ustawi wa waajiriwa Waafrika.

Katika kipindi hiki cha mwanzoni mwa mwaka wa 1950 viongozi wa TAGSA walikuwa Thomas Marealle kama Rais na Ally Sykes Katibu.

Rashid Kawawa, Dr. Wibard Mwanjisi, Steven Mhando, Dr. Michael Lugazi walikuwa wanakamati na hawa wote walihusika sana katika kuunda TANU na wakiishi na fikra ya kuunda chama cha siasa kudai uhuru wa Tanganyika wala hawajasikia jina la Julius Nyerere.

Huu ndiyo ukweli wa historia ya TANU.
Kujaribu kukwepa ukweli huu matokeo yake ni kuvuruga hata hiyo historia yenyewe ya CCM.

Picha:
Chief David Kidaha Makwaia
Abdul Sykes kulia na Ally Sykes Burma Infantry, 6th Battallion, Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945)

Mzee unaonaje ukitueleza mchango halisi wa Hayati Julius Nyerere kwenye ukombozi wa nchi yetu?
Uzalendo,
Baada ya TAA Political Subcommittee kuwasilisha mapendekezo ya katiba kwa Gavana Twining serikali ilipigwa na mshtuko mkubwa.

Yale mapendekezo ya TAA yalidai katika mengi pawepo na uchaguzi kuingia LEGCO na baada ya miaka 13 Tanganyika ipewe uhuru wake.

Twining akaanza mbinu ya kuivunja nguvu TAA kwa kuwahamisha kutoka Dar es Salaam viongozi wa TAA ili kupunguza joto la siasa.

Dr. Kyaruzi akapelekwa Kingolwira kisha Nzega.

Hamza Mwapachu akatupwa kisiwani Nansio ilimuradi hakubaki kiongozi pale TAA New Street.

Hii ilikuwa 1950.

Hamza Mwapachu na Abdul wakaamua juhudi zifanyike TANU iundwe.

Ndipo mazungumzo yakaanza kati ya Abdul na Chief Kidaha aje TAA achaguliwe kama President na mwaka unaofuatia TANU iundwe.

Hizi juhudi hazikufanikiwa na kwa miaka minne Abdul Sykes hakuitisha mkutano mkuu wa TAA.

Abdul alikuwa amekifikisha chama mahali ambako hakuweza kukipeleka mbele zaidi ya pale.

Ndipo 1952 alipokutana na Julius Nyerere ambae alipelekwa kwake na Kasella Bantu.

Haikumchukua muda mrefu kwa Abdul Sykes kutambua kuwa Nyerere ana uwezo mkubwa wa kukiongoza chama.

Mwaka wa 1953 Nyerere aligombea nafasi ya urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes na Nyerere akashinda ingawa ilikuwa tabu kumpitisha na mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.

Kuanzia hapa harakati za kudai uhuru zikaanza na wananchi waliitika mwito wa uhuru kwa hamasa kubwa sana.
 
Mzee nawezasoma wapi haya mammbo.
 
Mzee nawezasoma wapi haya mammbo.
M...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Bookshops Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani Dar es Salaam.

Pia kipo Soma Bookshop Mikocheni na Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Bei elfu kumi tu Ibn Hazm kwengine ni zaidi ya hapo kidogo.

Unaweza kuingia hapo chini ikiwa unapenda historia ya Tanzania fanya search kwa majina au matukio mfano ''Abduwahid Sykes,'' au ''Abdulwahid Sykes na Dockworkers Union,'' nk. nk.

mohamedsaidsalum.blogspot.com

Screenshot_20210504-035048_Photos.jpg

Screenshot_20210504-035324_Photos.jpg
 
M...
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Bookshops Msikiti wa Mtoro, Manyema na Mtambani Dar es Salaam.

Pia kipo Soma Bookshop Mikocheni na Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Bei elfu kumi tu Ibn Hazm kwengine ni zaidi ya hapo kidogo.

Unaweza kuingia hapo chini ikiwa unapenda historia ya Tanzania fanya search kwa majina au matukio mfano ''Abduwahid Sykes,'' au ''Abdulwahid Sykes na Dockworkers Union,'' nk. nk.

mohamedsaidsalum.blogspot.com

View attachment 1772621

View attachment 1772622
Na tulio mikoani mzee tunakipataje.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom