T-shirts za Jambo Forums (na zile za jamii Forums ?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

T-shirts za Jambo Forums (na zile za jamii Forums ?)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichuguu, Jul 24, 2012.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,095
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 280
  Mwaka 2007 nilipata T-Shirt ya Jamboforums bila malipo (nadhani kwa vile Jamboforums ilibadilishwa kuwa jamii Forums); bado naamini nina deni linalotokana na gharama za ile T-shirt, na nitalilipa au nimeshaanza kulilipa kivyakevyake.

  Nia yangu kuandika thread hii ni kuwa jana nilikuwa Tel Aviv ambako nilishangaa sana kukutana na myahudi mmoja amevaa T-Shirt ya JamboForms kama ile ya kwangu, ingawa ya kwake ilionekeana kuchoka kidogo labda kwa vile mimi huwa siitumii mara kwa mara hii yangu. Nilitaka kumpiga picha ila nikaogopa kwa sababu eneo lile watu hawaaminiani, anaweza kusema mimi na agent wa hamas nikabinywa bila hatia yoyote. Ila bado najiuliza sana huyu jamaa na ile Tshirt ya JamboForums kulikoni? Sina uhakika kama maandishi yake yalikuwa ni nyuzi au yalikuwa ni ya wino kwa sabau sikuweza kumkaribia sana wakati tukiwa kwenye basi. Baada kufika mwishs wa safari nilijaribu kumsemesha ikawa hata kiingereza hajui, halafu akawa kama anatajitahidi kunikwepa, na mimi nikaamua kuachana naye.

  Baada ya taarifa hiyo interesting, ninauliza tena, je zile T-Shirts za JamiiForums ziliishia wapi? Sisi wakongwe wa JF tunazitaka; angalau ziwe kwenye mikoba yetu tusije tukaziona na wayahudi na kubaki midomo wazi tena.
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Nadhani hilo swala la kupatikana kwa hizo T shirt limewashinda kabisa viongozi/mods wa jf. Wamebaki kuwapiga watu ban na kusahau kabisa ahadi ya kutupatia T shirt walizotuahidi!
   
 3. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 914
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Natamani niwe nayo nivae kitaa,hebu mods fanyia kazi zipatikane nchi nzima
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,347
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Na mimi nazihitaji kama tulivyo yaani mimi na familiya yangu.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...