T 814 BGZ Kilimanjaro Express | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

T 814 BGZ Kilimanjaro Express

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dropingcoco, Apr 26, 2011.

 1. d

  dropingcoco Senior Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  juzi nimepanda bus tajwa hapo juu, kwa kweli abiria tuliteseka sana, lilikuwa linaendeshwa na dereva anaitwa Salakana,huyu bwana alikuwa anakimbia sana na mbaya zaidi huku anaongea na simu kila wakati, watu tulihama makampuni mengine tukiamini wapo makini,lakini sasa wanapoelekea watapoteza wateja, ukizingatia na magari yao siku hizi yameanza kuwa mabovu....tunawashauri wajirekebishe
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hapo umenena ila kwanini mlipoona anakimbia msimwambie apunguze mwendo yaani nguvu ya uma ingefanya kazi ndani ya basi hilo!kwa kawaida maisha ya sasa yapo mikononi mwenu wenyewe msiitegemee serikali hii iliyochoka unapoona mtu anakosea mwambieni akikaidi piga simu kituo cha polisi au mumchape ndani ya basi humohumo tumechoka na ujinga huu kila siku maisha ya watu yanapotea roho zinateketea na wengine kubaki vilema kutokana na ujinga na uzembe huu wa baadhi ya madereva vilaza!kweli ifike wakati abiria na sisi tuchukue sheria mikononi mwetu kabla roho zetu hazijateketezwa na madreva kama hawa vilaza!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  JUZI NDIO SIKU GANI?
  Mlikuwa mkitoka wapi kwenda wapi?

  Ukitaka mambo haya yafanyiwe kazi weka uthibitisho wa taarifa zako!...Mimi nipo hatua 30 toka ofisini kwao, naweza fanya lolote nikipata usahihi wa taarifa hizi!
  Vinginevyo KILIMANJARO ni kampuni ya usafirishaji yenye heshima sana kwa route za Dar-Arusha!
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mkuu jamaa akikupa taarifa please pj fanyia kazi kweli hali ya ajali kwa sasa inatisha!yaani zinaongozana sana na karibia zote unaambiwa ni mwendo mkali wa dereva!pia kama ana ticket akutumie coppy yake!sema mie bado nawalaumu abiria kwanini huwa hawawaambii madereva kwamba punguza mwendo!
   
 5. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  juzi maana yake nini?ukienda oficn utajua route,dereva na kondakta wa hilo bus.hii kadhia hutokea sana halafu ukiwapeleka polisi wanahonga,dawa yao ni kuwaanika namna hii ili wajirekebishe!
   
 6. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanasoma Jamiiforum?
   
 7. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama vipi ni kuwatosa tu wapate heshima bahati nzuri route ya Dar-Arusha ina magari mengi tu ya maana. Karibu Dar express!!
   
 8. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama vipi ni kuwatosa tu wapate heshima bahati nzuri route ya Dar-Arusha ina magari mengi tu ya maana. Karibu Dar express!!
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hata kama hawasomi taarifa watazipata tu!jf kiboko we subiri watakurupuka huko waliko kujibu tuhuma.
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaa umenikumbusha ya msekwa kilimbana akaamua kukitoa mwenyewe!
   
 11. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama vipi ni kuwatosa tu wapate heshima bahati nzuri route ya Dar-Arusha ina magari mengi tu ya maana. Karibu Dar express!!
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,523
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  poa mkuu , kwa sababu ilikuwa nipande hii kilimajaro, kweli JF ni kila kitu wajamen.
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Hapo umenena kaka, hii ndo kampuni makini niliyopata kuiona na isiyo nguvu ya soda. Jamaa wako poa, nidhamu ya barabarani ipo juu pamoja na heshima kwa abiria. Safari za uhakika route ya Kaskazini Dar Xpress ndo mpango mzima...
   
 14. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hili la kuzungumza kwa simu wakiwa kwenye mwendo, binafsi niliwahi kulishuhudia kwenye haya mabasi ya Kilimanjaro, nilimuuliza mhudumu akabaki anacheka, sikujibiwa, ingawa dereva nadhani baada ya kutonywa akawa hazungumzi tena mara kwa mara, sometimes wana mwendo mkali, lakini kuhusu huduma kwa abiria naweza kusema wanajitahidi, mawasiliano kati ya dereva na abiria yapo too friendly jambo ambalo sikuwahi kushuhudia kwenye mabasi mengine ya Dar-Ar..

  Ni kampuni nzuri ya usafirishaji wa abiria (Dar-Ar/Ar-Dar) naweza kusema baada ya Dar Express.. Ningeshauri wamiliki wa haya mabasi waweke sanduku la maoni kwenye kila basi na funguo zibaki kwa meneja ili dereva asiweze kupata access ya maoni ya abiria mpaka kwa ruhusa ya meneja, kisha wawe wanaboresha huduma zao kulingana na maoni yatakayokuwa yanatolewa na abiria.
   
 15. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Abiria nao wana wajibu wa kudhibiti madereva wawapo barabarani.
   
 16. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Kwani basi likitoka dar kwenda arusha linatakiwa liende kwa kasi gani (kph)?

  Mie najua 120 kph sio mbaya au kama kama bara bara imenyooka dreva anaweza kwenda mpaka 140 kph.

  Sasa kama gari ikitoka Dar kwenda arusha au vice versa kwa mwenda wa tractor watu watafika kweli?

  Cha maana ni umakini wa Dreva tuu na pia dreva afuate sheria za barabarani. mfano ku overtake katika kona ndo mbaya.

  tatizo sio speed, tatizo barabara zetu ni finyu-- hatuna high ways Tanzania.

  hebu fanya practical, nenda nairobi, panda basi kutoka nairobi kwenda mombasa uangalie speed gari inavyotembea. Nafikiri ni speed 160 hadi 200.

  Watanzania tupiganie ubora wa barabara, hasa tuwe na high way.

  Example. Barabara kutoka Nairobi-Emali -loitokitok mpaka Custom/immigration ya Tanzania ina High way ( 4 ways) while Tarakea mpaka Moshi ni Nyembamba sana na kona mingi sana. (Source EAC and TANROADS).
   
 17. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  a a....inawezekana tulipanda bus moja nn,mm nilipanda jmosi kutoka Ars-Dar, huyohuyo dereva alikuwa anaendesha na alikuwa anaongea na simu kila wakati, na tulipofika sijui panaitwa kisangara gari liliharibika,tulikaa almost lisaa lizima,kutoka hapo mwendo ulikuwa mdundo, kwa kweli nilikuwa siwezi kusafiri na kampuni nyingine kwa route hiyo lakini itabidi nihame, kwa anayemfahamu mmiliki wa hayo mabus na namba yake ya simu atupatie ili aweze kusababishwa kuwafundisha madereva wake kuwa na adabu na roho za watu
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  a a....inawezekana tulipanda bus moja nn,mm nilipanda jmosi kutoka Ars-Dar, huyohuyo dereva alikuwa anaendesha na alikuwa anaongea na simu kila wakati, na tulipofika sijui panaitwa kisangara gari liliharibika,tulikaa almost lisaa lizima,kutoka hapo mwendo ulikuwa mdundo, kwa kweli nilikuwa siwezi kusafiri na kampuni nyingine kwa route hiyo lakini itabidi nihame, kwa anayemfahamu mmiliki wa hayo mabus na namba yake ya simu atupatie ili aweze kusababishwa kuwafundisha madereva wake kuwa na adabu na roho za watu
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Pole best!
  Ningejua ile tiketi ni ya basi hilo ningeifanya nap-kin dakika ileile!
  Itabdi sasa urudi na Ngorika ile ya mchina!
   
 20. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Nenda sasa hapo ofisini kwao na utupe yaliyojiri, Preta ameishakupa details na hauna haja ya kuigeuza hiyo ticket nap-kin.
  Tunasubiri utujuze......
   
Loading...