ceekay
JF-Expert Member
- Dec 22, 2011
- 413
- 156
Mimi ninasafiri sana kati ya Dar - Moshi - Arusha kwa basi tajwa hapo juu. Leo tarehe 20 December 2016, mimekuta mfumo mpya kwenye ofisi yao ya Moshi, unalipa Tshs 3,000 na kukatiwa tiketi ya Arusha (Hakuna kulipa ndani ya basi kwa konda). Mfumo huu ni mziri (tena sana).
Kitu kilichonifanya kuandika uzi huu, ni pale basi ilipofika. Kondakta na dereva wa basi lilipofika wakasema "Hakuna nafasi!!! Nafasi zimejaa!!!". Hilo jambo likasababisha abiria kuanza kusukumana tukiwa hatuamini kinachoendelea. Dereva alipoona hilo na yeye akaja kuanza kusukuma abiria ili wasiingie. Nikajiuliza maswali kadhaa:
1 - Kilimanjaro Express ninayoijua mimi ndio kuna utaratibu mbovu hivi? Je ni kwa kuwa ni kipindi cha sikukuu wakiwa wanaamini kuwa watapata tu abiria?
2 - Kwanini ofisi ilikatisha tiketi kuzidi nafasi zilizopo kwenye gari husika?
3 - Haki ya abiria iko wapi hapa?
It's very [HASHTAG]#sad[/HASHTAG], Kilimanjaro Express badilikeni