System ya magufulification nimeanza kuitumia katika familia yangu

chagga land

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Posts
394
Reaction score
95
ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika familia yangu naenda kutoa maamuzi yafuatayo:-moja,nitafuta sherehe zote ambazo zilitakiwa kufanyika na kusherehekewa nyumbani kwangu kuanzia za kiserikali na za kidini na fedha nilizokuwa zimepangwa zitaelekezwa kwenye matumizi yenye uhitaji mkubwa kama elimu.mbili,nguo zitanunulia mara moja tu kwa mwaka na zile ambazo zilikuwa zikanunuliwe fedha zake zitapelekwa kwenye kwenye kununua dawa za kujikinga malaria.tatu,ninaenda kufuta matumi ya umeme wa TANESCO na fedha ambazo tungekuwa tunalipia TANESCO tutazikusanya kidogo kidogo na kwenda kununua solar power.nne, ninaenda kuondoa bomba la maji la DAWASCO na tutajibana ili tuweze kuchimba kisima chetu.nne,nimefuta safari zisizokuwa za lazima,na fedha zilizokuwa zitumike kwenye safari zitapangiwa matumizi mengine ambayo ni pamoja na kulipia madeni ya familia tunayodaiwa.
 
Unafanya kama utani, lakini uchambuzi wako una mantiki endapo utaufanyia kazi kama ulivyouchambua. Matumizi mengi Tunayoyafanya ukiyaangalia kwa umakini huwa hayana faida kimaendeleo.
 
Mh!nguo mara moja kwa mwaka?Labda itaaply kwa wazazi ila si watoto ni ngumu.Huwez mnunulia mwanao nguo mara moja kwa mwaka
 
Big up Mkuu...! Kuna jamaa juzi alifanya Ukaguzi wa kushtukiza jikoni kwa mama watoto wake akakuta mizagazaga kibao akaamua kupunguza pesa aliyokuwa anaiacha home ili itumike kwa manufaa mengine.
 
Hiyo pesa unayosevu kwenye matumizi yasiyo ya lazima, mpelekee mchepuko wako mkuu,

Utakuwa umefanya vema saana,
 
Mkuu angalia usije kimbiwa na familia yako yote
maana wataoweza himili huo mziki ni wachache...

ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika familia yangu naenda kutoa maamuzi yafuatayo:-moja,nitafuta sherehe zote ambazo zilitakiwa kufanyika na kusherehekewa nyumbani kwangu kuanzia za kiserikali na za kidini na fedha nilizokuwa zimepangwa zitaelekezwa kwenye matumizi yenye uhitaji mkubwa kama elimu.mbili,nguo zitanunulia mara moja tu kwa mwaka na zile ambazo zilikuwa zikanunuliwe fedha zake zitapelekwa kwenye kwenye kununua dawa za kujikinga malaria.tatu,ninaenda kufuta matumi ya umeme wa TANESCO na fedha ambazo tungekuwa tunalipia TANESCO tutazikusanya kidogo kidogo na kwenda kununua solar power.nne, ninaenda kuondoa bomba la maji la DAWASCO na tutajibana ili tuweze kuchimba kisima chetu.nne,nimefuta safari zisizokuwa za lazima,na fedha zilizokuwa zitumike kwenye safari zitapangiwa matumizi mengine ambayo ni pamoja na kulipia madeni ya familia tunayodaiwa.
 
Hahahahaha na matumiz ya kula chakula cha usiku na mkeo usisahau!!
 
Mh!nguo mara moja kwa mwaka?Labda itaaply kwa wazazi ila si watoto ni ngumu.Huwez mnunulia mwanao nguo mara moja kwa mwaka

hapa kazi tu! nitamshawishi mke wangu ili aweze kuwashawishi watoto na familia kwa ujumla nadhani after five years nitaleta feedback hapa JF
 
Angalia tu watoto wasijeonekana kama hawa wazazi aisee wakati upo
 
ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika familia yangu naenda kutoa maamuzi yafuatayo:-moja,nitafuta sherehe zote ambazo zilitakiwa kufanyika na kusherehekewa nyumbani kwangu kuanzia za kiserikali na za kidini na fedha nilizokuwa zimepangwa zitaelekezwa kwenye matumizi yenye uhitaji mkubwa kama elimu.mbili,nguo zitanunulia mara moja tu kwa mwaka na zile ambazo zilikuwa zikanunuliwe fedha zake zitapelekwa kwenye kwenye kununua dawa za kujikinga malaria.tatu,ninaenda kufuta matumi ya umeme wa TANESCO na fedha ambazo tungekuwa tunalipia TANESCO tutazikusanya kidogo kidogo na kwenda kununua solar power.nne, ninaenda kuondoa bomba la maji la DAWASCO na tutajibana ili tuweze kuchimba kisima chetu.nne,nimefuta safari zisizokuwa za lazima,na fedha zilizokuwa zitumike kwenye safari zitapangiwa matumizi mengine ambayo ni pamoja na kulipia madeni ya familia tunayodaiwa.

Usisahau kufuta bajeti ya mpango wa kando
 
kwenye mambo ya msingi huduma itaendelea kama kawaida mkuu

Hahaha mkuu hapo hakuna kubana matumizii enh?? Umenifurahishaa na nililijua hu mtego ni mgumu kwako!! Hongeraa! Na mm nipo nyumaa yako
 
Big up kwa kuiheshimu BIA.,. Ningeshangaa ...
 
usisahau na kurudi kwa kushtukiza unaweza kumkuta mke wako anapotea kama makontena yale
 
Back
Top Bottom