System aliyoitegemea Lowassa ilivurugwa na Kikwete!


Nyerere hakuwa BEPARI CHAFU kama MBOWE na LOWASSA.TANU haikuwa kama Chadema.Ukoloni haukuondolewa madarakani kwa FUJO,VURU,ZOMEAZOMEA NA MAANDAMANO BALI Nguvu ya HOJA.Chadema ni mojawapo ya chama cha ki-BOGUS Kuwahi kutokea Tanzania kikiwaweka pamoja vijana wala ngada,viroba na bange
 
Makongoro Mahanga bado ni waziri au?
Makongoro kajiuzuru uwaziri siyo kuvunja baraza la mawaziri. Hata hivyo kwa post yako dada ni ngumu kumjua mtu anawaza nini! Ndo maana unaona unaibuka uzushi mara Lubuva ni shemeji yake Lowassa n.k. Laiti tungekuwa tunajua hata walioko kwenye system wanawaza nini basi tungekuwa na majibu yanayostahili. Usimwamini binada ana tabia ya kubadilika. Yawezekana Kikwete aliondoa waliokuwa watu wa Lowassa tunaowajua mimi na wewe. Lakini pia upo uwezekano wa watu kumuunga mkono Lowassa kimyakimya bila kujulikana kwa wakubwa wao. Tuache tarehe 25 ituletee matokeo haya mambo mengine tuyaache
 
Hatuangalii syatem sisi, tunamwangalia lowassa na Ukawa nzima..nyie mnaotegemea system subirin muone kama itawapa kura...kura ni nguvu ya umma..peopleeeeez power...mshadata sa hizi..Ukawa ikulu..na bao la mkono mwaka huu..tumelithibiti...
 

Mkuu kunajambo ambalo hulipendi kulisikia nalo ni Rais mpya ajaye ni DR JOHN POMBE MAKUFURI...

Pole maana huo ndyo ukweli, mwambie na jirani yako hvyo, ili mjiandae kisaikolojia,
 

Mpaka sasa ccm ipo hoi bin taaban,hawana uhakika adui yao yupo nje ya chama au wanae ndani ya chama!Rejea kauli ya mgombea urais wao akiwa Bukoba,"ktk msafara wangu kuna watu mchana wapo ccm na usiku wapo ukawa",jiulize pia ile team ya ushindi ya watu therathini na ushee ipo wapi sasa ivi?
Kete waliyobaki nayo ccm ni kwenye kuhonga mawakala na kuiba kura ndio maana hawataki kabsa kusikia habari za wananchi kukaa mita 200 kusubiri matokeo ilihali wanajua sheria haikatazi,amani bila haki ni mazingaombwe.
Kwa kiasi kikubwa Lowassa kawajeruhi na hawana uhakika wa ushindi hata kidogo.
 
watanzania mna akili fupi na ni mazuzu mnaosahau haraka sana hata kama mmevuliwa nguo hadharani,,
lowasa asingekua na nguvu angepindua mtokeo ya mmbe kule Dodoma na kukaribia kuipasua nchi...amuoni jinsi
navoitesa serikani yenu licha yakua na ogans zote za utawa,,,,,,,meshasahau madhila mlofayiwa yooteeeee,,,
 
Mkuu kunajambo ambalo hulipendi kulisikia nalo ni Rais mpya ajaye ni DR JOHN POMBE MAKUFURI...

Pole maana huo ndyo ukweli, mwambie na jirani yako hvyo, ili mjiandae kisaikolojia,

Sina tatizo na Magufuli kuwa rais kwani anafadhali kuliko JK ambaye ni rais wangu, atakuwa rais wangu kwa uhalali? hilo moja, la pili je wabunge wa ccm watakuwa wengi vilevile na kwa njia isiyokubalika? Hapo ndio wasiwasi wangu ulipo kwani wabunge wengi wa ccm hawajui wajibu wa mbunge ndani ya bunge wao wanachojua ni kucheza kama serekali, wachache sana kama akin Deo Filikunjombe RIP, Ester Bulaya ndio walikuwa wanajua nini jukumu la mbunge.
 
Lowassa rais wa tz

Mkuu, urais, atauona kwenye tv, magazet, jf na kwenye mkutano wa kampeni, ila kwa ikulu pale magogoni, hapana, labda kwa mualiko wa rais mteule dr john pombe makufuri,

Najua hutaki kusikia ila ukweli ndo huo..jiandae kisaikolojia mkuu
 
Hiyo nguvu ya uma iko wapi, acha kudanganya watu, ni nguvu ya mafisadi, nguvu ya uma iliondoka na Dr.Slaa, iliyopo ss hivi ni nguvu ya viroba.


Ni kama unaongea ukweli vile.Japokuwa binafsi nasubiria matokeo ya people's power baada ya 25
 
UDA well said...watu wanaopingana na ukweli mimi sipendei hatakupoteza mda wangu. waache watajua taehe 25
 
I'm curious. Nini hasa kilichofanya Kikwete aamue kuvunja mtandao "uliojengwa na Lowassa" ambao ndio uliomuingiza yeye madarakani? Tuseme alikwishapiga hesabu zake mapema akiwa na lengo la "kummaliza Lowassa" mara tu baada ya kufanikiwa kuwa rais kwa msaada wa mtu huyohuyo aliyemuaminisha kuwa na urafiki naye? Kwamba baada ya hapo Lowassa hatakuwa na manufaa tena kwake? Inawezekana kuwa JK ni muumini wa falsafa za Niccolo Machiavelli za kutumia watu kufanikisha malengo/maslahi binafsi kisha kuwatupilia mbali - hata kuwaangamiza? Kwamba kwake suala la urafiki, uswahiba na hisia za aina hiyo hazina nafasi katika utu wake? Ndio maana anaweza kudumisha tabasamu na bashasha mbele ya umma hata kama behind the scenes anaagiza watu wanaotishia maslahi yake, ya familia yake na ya utawala wake kufanyiwa maovu?

Mleta mada umefurahia Kikwete "kuuvunja" mtandao wa Lowassa. Ingekuwa vyema basi pia ungetoa ufafanuzi ni kwa malengo gani na kwa maslahi ya nani? Ni sisi Watanzania ndio wanufaika au ni mchezo wa kuzidiana kete (battle of wits) kati ya wanamtandao - tena mmoja akiwa ndiye mjuzi (JK) na mwingine akitumika kama zoba (EL)? Majuzi mzee Butiku alilalamika kuwa CCM na serikali yake vimeharibiwa na hao "wanamtandao". Naona ukweli unadhihirika kwenye mada kama hii. Sawa. Inawezekana, katika mchezo wa wanamtandao, Lowassa keshamalizwa nguvu na JK na hivyo CHADEMA imeingia mkenge na kupoteza. Hii ina mana gani kwetu wananchi? Tukubali kuendelea kuwekwa poni na magwiji wa mtandao?

Ninachokiona ni mchezo uleule ukiendelezwa na JK kupitia Magufuli. Naye anatumiwa kama kete tu ya kukirudisha madarakani chama ambacho sasa kinadhibitiwa kikamilifu na upande wa JK kwa falsafa ileile ya Machiavelli. Inawezekana hata teuzi nyingi zilizofanywa muda mrefu na karibuni ni sehemu (game plan) ya mchezo huo. Na si Magufuli tu. Marehemu Mtikila, Dk Slaa, mama Maria, mzee Mwinyi, n.k. nao wameshawekezwa kwenye mkakati huo. Hivyo, kati yao wote hakuna aliyekuwa na au mwenye ubavu wa kuleta mabadiliko ya maana katika mfumo na uendeshaji wa chama na serikali.

Kwangu mimi, hii ni sababu tosha ya kuiondoa CCM madarakani ili kuinusuru nchi kuwekwa rehani na watu wenye maslahi binafsi pekee, wasio na chembe ya uzalendo wala utu. Ni bora kuanza kwa kuvunja "spell" ya "CCM mtandao" - hata kwa kumtumia aliyekuwa mmoja wao ambaye wamemzidi kete na kumfanya zoba na ambaye, naamini, anaweza kudhibitiwa kirahisi zaidi ndani ya mabadiliko. Hii itafanya, kwanza, CCM yenyewe ijisafishe kwa dhati na, pili, watakaokuwa madarakani watambue kuwa umma umeshachukua mamlaka yake ya kudhibiti watawala bila hofu kwa kutumia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Hatuwezi kuacha taifa liendelee kuendeshwa kwa falsafa za Machiavelli.
 
Mkuu kunajambo ambalo hulipendi kulisikia nalo ni Rais mpya ajaye ni DR JOHN POMBE MAKUFURI...

Pole maana huo ndyo ukweli, mwambie na jirani yako hvyo, ili mjiandae kisaikolojia,

Mkuu umepata wapi huu uhakika??? Nijuze.
 
Hii inafikirisha juu ya nani hasa wa kuitoa ccm madarakani!

Unaweza kuwa sahihi but why yeye jk kafanya hvyo? Pia sio kuwa lowassa ni mzuri sana bali ccm imechokwa sana na tunatengeneza base ya kupata vuliongozi wazuri kutoka chama chochote kile kwa baadae. Natunataka kuwaaminisha wale wanao dhani hii nchi bila wao haita enda kuwa itaenda na wananchi wakiamua jambo linawezekana, na nilazima viongozi wasikilize matakwa ya wananchi.
Pia tunataka kuwa saidia ccm wakajipange vzr kiwe chama kizr kwa baadae nasio mfumo wa ukoo walio nao saiz kutuletea watoto na wajukuu zao ambao hata shida hawazijui kabisa
 
Unaitwa Uda na registered October 20!!
That speak volumes...

BS !!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…