System aliyoitegemea Lowassa ilivurugwa na Kikwete!

System aliyoitegemea Lowassa ilivurugwa na Kikwete!

Uda

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
811
Reaction score
623
Ni ukweli usiopingika kuwa Lowassa ameanza harakati za kuusaka urais muda mrefu pengine toka 1995.

Mwaka 2005 akimsindikiza Kikwete, Lowassa alijiwekea mizizi au tuseme alitengeneza mtandao ambao ulimuingiza Kikwete madarakani na kumfanya yeye kuwa waziri mkuu.

Baada ya kutemwa uwaziri mkuu system ya Lowassa iliendelea kuwa madarakani kwa muda mfupi kabla ya Kikwete kuanza kuivuruga na kuisambaratisha kabisa.

Mpaka tunafika 2015 Kikwete alifanikiwa kabisa kuiondoa system ya Lowassa serikalini.

Nadhani alifanya hivi kwa maandalizi ya kumkata katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya CCM pengine kwa maelekezo maalum

CHADEMA na Team Lowassa wamedanganyika na kile kilichoitwa nguvu ya waziri mkuu bila kujua ilishafutiliwa mbali.

Wengi wa wakurugenzi na wakuu wa taasisi ambao waliwekwa na Lowassa walishatemwa siku nyingi.

MaDC na MaRC loyal kwa Lowassa walishatemwa siku nyingi.

Kwa hiyo ile nguvu ya mamba baharini haipo kwani bahari ilishakaushwa.

Kwa sasa Lowassa amebakia na usanii tu kuaminisha watu kuwa ana mahusiano na system kumbe hamna kitu ni maigizo tu.

Hili laweza thibitishwa na kauli kinzani kutoka UKAWA. Mbowe anasema lindeni kura wakati Lowassa alisema pigeni kura na kazi ya kuzilinda aachiwe, hizi ni sentensi mbili kinzani kutoka katika taasisi moja.

Vijana wanapaswa kutambua Lowassa hana influence yoyote kwenye chama au serikali kwa sasa, makapi ya Lowassa yako nje na yanajaribu kurudi ndani ili kuweka mirija ya kula hela zetu tu.

Im so disappointed with CHADEMA baada ya kuuvaa mkenge huu wa kihuni ambao unaenda kuirudisha nyuma miaka 20.

Wafikirie waliohamia CHADEMA au UKAWA na uhusiano wao na CCM au serikali in the past 5 years ndio utanielewa.

Kwa sasa CHADEMA wajikite katika kampeni za ubunge zaidi ili kuokoa jahazi..operesheni ya siku nne...mission impossible!
 
Sasa si ufurahi kimya kimya ?unamweleza nani na kwa nia gani?mkubali msikubali CCM Tz haijapata Kuwa na upinzani wa kiwango hiki tangu uchaguzi wa vyama vingi.Hadi sasa CCM hawana uhakika wa kushinda Ndo maana wanatengeneza goli la mkono.Jiulize wanaogopa nini watu wakikaa Mita 200?Hata wakiponea chupu chupu ha watakuwa na Kiburi cha madaraka tena.Lowassa kawapa funzo hawatakaa wasahau.Mungu akisimamia upande wa haki hakuna binadamu wa kupinga.Viva Lowassa viva.
 
Nakubaliana na mantiki yako ya lowassa kuleta upinzani kwa ccm just like Mrema na ninakubaliana na mantiki yako ya kwamba ccm imefunzwa adabu kwa tishio feki!

Lakini kuna issue ya Upinzani kuvurugika na kuanza upya kwa kuwa umewekeza kwa lowassa kama lowasa lakini haujaweza kumtumia lowasa kuchukua viti vingi vya ubunge...wabunge wa chadema wako hoi katika kampeni majimboni.
 
Lawrance Masha alishatemwa kitambo!

Sumaye hakuwa na ubavu kwa merry Nagu

Kingunge aliwekwa pembeni!

hawa ndio watu uliowamaanisha kwenye hoja yako au bado unaendelea na orodha? akili zako ni finyu kuliko akili za konokono.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa lowasa ameanza harakati za kuusaka urais muda mrefu pengine toka 1995.

Mwaka 2005 akimsindikiza kikwete lowassa alijiwekea mizizi au tuseme alitengeneza mtandao ambao ulimuingiza kikwete madarakani na kumfanya yeye kuwa waziri mkuu.

Baada ya kutemwa uwaziri mkuu system ya lowassa iliendelea kuwa madarakani kwa muda mfupi kabla ya JK kuanza kuivuruga na kuisambaratisha kabisa.

Mpaka tunafika 2015 JK alifanikiwa kabisa kuiondoa system ya lowassa serikalini.

Nadhani alifanya hivi kwa maandalizi ya kumkata katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya ccm pengine kwa maelekezo maalum

Chadema na Team lowassa wamedanganyika na kile kilichoitwa nguvu ya waziri mkuu bila kujua ilishafutiliwa mbali.

Wengi wa wakurugenzi na wakuu wa taasisi ambao waliwekwa na lowassa walishatemwa siku nyingi.

MaDC na MaRC loyal kwa lowassa walishatemwa siku nyingi.

Kwa hiyo ile nguvu ya mamba baharini haipo kwani bahari ilishakaushwa.

Kwa sasa lowassa amebakia na usanii tu kuaminisha watu kuwa ana mahusiano na system kumbe hamna kitu ni maigizo tu.

Hili laweza thibitishwa na kauli kinzani kutoka UKAWA...Mbowe anasema lindeni kura wakati lowassa alisema pigeni kura na kazi ya kuzilinda aachiwe.hizi ni sentensi mbili kinzani kutoka katika taasisi moja.

Vijana wanapaswa kutambua lowassa hana influence yoyote kwenye chama au serikali kwa sasa....makapi ya lowassa yako nje na yanajaribu kurudi ndani ili kuweka mirija ya kula hela zetu tu.

Im so disappointed with Chadema baada ya kuuvaa mkenge huu wa kihuni ambao unaenda kuirudisha nyuma miaka 20.

Wafikirie waliohamia Chadema au Ukawa na uhusiano wao na CCM au serikali in the past 5years ndio utanielewa.

Wewe ni mwongo. Mamba hawakai baharini labda bahari ya CCM
 
Umeandika kama una haki miliki ya Tanzania.F.Y.I Hata JK hana haki miliki,na mbaya zaidi anaweza kuvuruga kila mfumo,lakini hawezi kufuta mahaba waliyonayo Watanzania katika mioyo yao!!Kwa kuwa JK alivuruga mfumo uliomweka akidhani anamkomoa ENL anajikuta amekumbatia mzinga wa nyuki!!..LOWASSA ANATOSHA.
 
Magufuli 55% lowasa 41% others 4%.MPs ccm 48% including nominated,opposition 52%. Ni naomba iwe hivyo na serikali itawajibika kwetu wananchi.

Ni fikra nzuri ambazo hata mimi naziombea ili tu tuweze kuidhibiti serikali.

lakini sad story ni kwamba wabunge wa UKAWA wako hoi unless UKAWA waje na final new strategy!
 
Umeandika kama una haki miliki ya Tanzania.F.Y.I Hata JK hana haki miliki,na mbaya zaidi anaweza kuvuruga kila mfumo,lakini hawezi kufuta mahaba waliyonayo Watanzania katika mioyo yao!!Kwa kuwa JK alivuruga mfumo uliomweka akidhani anamkomoa ENL anajikuta amekumbatia mzinga wa nyuki!!..LOWASSA ANATOSHA.

Wewe unaleta ushabiki sasa!
 
Inaelekea unajua just a tip of an iceberg.
Wenzako wanahaha Lumumba kuweka mambo sawa lakini wameshindwa.
Aliekuambia amekujaza hewa.
Ukweli ni kwamba watu wa lowasa wapo wengi sana. Wamebaki CCM kimkakati.
Jiulize kwanini kikwete hajavunja baraza la mawaziri hadi leo?
 
Makongoro Mahanga bado ni waziri au?
 
Back
Top Bottom