Syria watungua ndege ya Israel

More Updates

IDF wametoa video inayoonyesha drone ya Iran ikiingia kwenye Anga la Israel na Israel kuidungua....

Pia ikionyesha jinsi Israel ilivyoshambulia kambi ya jeshi inayoamimika kwamba hiyo drone ndo imetoka
6bf6cd53120dc186c21cc08fd603c134.jpg


Na mpaka sasa air defenses nne za Syria zimeharibiwa pamoja na sehemu nyingine za kijeshi za Iran na Syria
Uongooooo
 
yani kutungua ndege ya miaka ya 1970 ni kitu Cha kujisifu kweli!!!! Tena hiyo ndege imekua ikishambulia Mara kwa Mara...Halafu mnajisifu wakati ndege moja imeirushia makombora 10 utafikiri mlikua mnaua Simba vile
kwani ndege ya miaka ya 70 hua inageuka inakua baiskeli?! Syria nao ni wapuuzi kama wanatumia makombora 10 kutungua baiskeli
 
Wakuu sijui kama kuna kitu mmekielewa, huyu jamaa anajiita ELUNGATA amehamisha uzi wangu kama ulivyo na kuunganisha kwake, afu mbaya zaidi uzi wangu umepotea kwenye mazingira yasiyojulikana. Nawaomba wakuu mnisadie kiufundi.

Uzi wangu ulikuwa unakichwa cha Habari kinachosema
SYRIA WAR:KIMENUKA TENA NI MCHEZO WA KUTUNGUANA TUU.
 
Wakuu sijui kama kuna kitu mmekielewa, huyu jamaa anajiita ELUNGATA amehamisha uzi wangu kama ulivyo na kuunganisha kwake, afu mbaya zaidi uzi wangu umepotea kwenye mazingira yasiyojulikana. Nawaomba wakuu mnisadie kiufundi.
Unataka tukusaidieje?
 
Ni breaking news,asubuhi na mapema leo drone kutoka syria iliingia anga la golan inayokaliwa na israel,kutafuta waasi wa syria.
Israel wakaitungua,na pia wakashambulia uwanja wa ndege wa T-4 ilipotokea drone.
Syria wakafyatua makombora ya kutungulia ndege na kuipiga ndege ya israel ambayo imeangukia israel japo ruban kapona japo majeruhi.
Israel wanalipa kisasi mida hii wanashambulia damusca na syria wanajibu mapigo kwa kufyatua makombora kuelekea golan.

====================

Ndege vita ya Israeli imeanguka baada ya kutunguliwa na Jeshi la Siria(Syrian Ant-AirCraft) baada ya shambulizi dhidi ya maeneo(Targets) ya Irani ndani ya Siria.

Marubani wa wili waliokuwa ndani ya ndege vita F-16 walifanikiwa kutoka ndani ya ndege na kutua salama kwa parachuti Kaskazini mwa Taifa la Israeli, inasemekana wamefikishwa hospitalini.

Israeli imesema ndege vita F-16 imefanya mashambulizi kadhaa kwa kujibu mapigo kitendo cha Irani kumshambulia Israeli kwa Drone ambayo walifanikiwa kuidhibiti.

Siria wamefanya shambulizi hilo kutokana na kitendo korofi cha Israeli.

Jeshi la Israeli limesema helicopter ya jeshi ilifanikiwa kudhibiti Drone ya Irani iliyosafiri kutoka Siria na kupenya mpaka Israeli.

"Drone hiyo iliingia eneo la Israeli na ikawa mikononi mwetu", Brig Gen Ronen Manelis Msemaji wa Jeshi la Taifa la Israeli (IDF).

Jeshi la Israeli (IDF) limesema kwa kujibu mapigo wakaamua ku-target harakati za Irani(Inasemekana ni military base) ndani ya Siria. Jeshi la Israeli likaendelea kusema mpango uliopangwa kufanyika ndani kabisa ya eneo la Siria umefanikiwa.

fbef942f6d95eb6e2a799373b10e67b9.jpg


Sauti za tafadhali zilisikika kwenye maeneo ya Israeli Kaskazini na kwenye vilima vya Golan kutokana na shambulizi la anga lililofanywa na Siria.

Wakazi wa maeneo karibu na tukio wamesema wamesikia milipuko kadhaa kwenye maeneo karibu na mipaka ya Jordan na Siria.

6b7f5c8365a07558effa7fd66fd9a340.jpg


Chombo cha habari cha Taifa la Siria kimenukuu chanzo cha habari kwa kusema ulinzi wa anga umefanya shambulizi kujibu mapigo kitendo korofi cha Israeli dhidi ya military base siku ya Jumamosi.

Irani na Urusi ni washirika wakubwa wa Raisi wa Siria Bashar AL Assad, ambao mjeshi yao yamekuwa yakipambambana na Waasi tangu 2011 nchini Siria.

11/2017,Usalama wa Magharibi waliiambia BBC kwamba Tehran (Irani) wameanzisha permanent military base nchini Siria.


Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameonya kwamba Israeli haitakubali huo mpango kufanikiwa.

f8edde6fecfd5b1ebbc6275ef8cb416b.jpg


Source:Israel jet crashes amid Syrian fire - army
WE JAMAA(ELUNGATA) UDUKUZI ULIOUFANYA NA KUUPOTEZA UZI WANGU INATHIBISHA UBOYA NA UDHAIFU SANA KIFIKRA.
 
Back
Top Bottom