Synovate: Vinara tisa urais 2015

Synovate: Vinara tisa urais 2015

It is in the public domain now and should be accessible on demand.
Mi nimeipata kwa njia ninazo zijua mimi, ukitaka nitakutumia na wewe
Nimeridhika kua wana 95% of confidence, sample ya 2000 people
Rural and urban area reflective, gender balanced na standards zingine zote

Tunajua mipango ya huu utafiti wenu fake! Wa kupika. Malengo vilevile tunayajua. Na walicholipwa na kuahidiwa wafanya utafiti tunakijua. Mtaumbuliwa soon!
 
Wanajaribu kudanganya umma, nadhani mimi sio mmoja wao ya watakodanganyika kirahisi hivi.
 
Jamani hawa wanaojiita watafiti wa Synovate ni moja ya taasis inayomilikiwa na CCM.Kazi yao nikupotosha umma wa Tanzania na kueneza propaganda chafu,chondechonde wananchi tupuuzeni utafiti ambao hauendani na hali halisi huu ni upuuzi mtupu wa CCM wanazidi kuendesha propaganda za udini na kikabila ili kuwa gawa waTanzania ili waendelee kututawala.
 
"Izo" ni kitu gani?

Unataka kuongelea elimu wewe? Ungejua lolote kuhusu elimu ungejua utafiti bila sample space, methodology na margin of error ni hadithi tu.

Hivi si vitu vipya useme hamna standards. Gallup has been doing this for over 77 years.

Judging from your comment I doubt you even know what Gallup is.

tehetehe, unajua nyie mnaojiita wasomi mnajichekesha. Owk unajua hesabu so?margin of error and so forth, misamiati mizitomizito unamwambia nan? uko unakowasemea 60% ya population n degree holder, apa form4 hajui kusoma wala kuandika wacha kuelewa. it seems you dont know where and who are you?
 
tehetehe, unajua nyie mnaojiita wasomi mnajichekesha. Owk unajua hesabu so?margin of error and so forth, misamiati mizitomizito unamwambia nan? uko unakowasemea 60% ya population n degree holder, apa form4 hajui kusoma wala kuandika wacha kuelewa. it seems you dont know where and who are you?

Wapi nimejiita msomi?

Kwa taarifa yako mimi ni anti-usomi kuliko Pol Pot. Rekodi yangu hapa JF ya kukataa wabunge kuchujwa kwa degree na mifano yangu iliyomuweka rais mstaafu wa Brazil Lula Inacio Da Silva pamoja na Harry Truman wa Marekani na Waziri Mkuu John Major wa Uingereza kama mifano ya kuigwa ingawa hawana shahada hata moja utaelezea zaidi kwamba mimi sishabikii usomi, bali matokeo ya kazi ya mtu.

But that doesn't mean I must always dumb down the narrative to the lowest common denominator, lest we all grunt like invalids. I would rather challenge mediocrity and idiocracy.

Go figure.

Idiocracy_movie_poster.jpg
 
Hivi mtu unawezaje kuandika habari yooooote hii, na kuweka asilimia zooote hizo, bila kutoa sample space ilikuwa vipi (watu wangapi, kutoka wapi etc) na methodology iliyotumika ( wamepewa questionnaires, wamepigiwa simu etc).

Gazeti lina mhariri hili?

Tutajuaje kama sample space si madarasa mawili ya shule moja ya sekondari yanayojumuisha wanafunzi waliojichokea na kujaza questionnaires randomly kama sehemu ya adhabu ya utovu wa nidhamu?

NB: The original post has been updated with more details since this post demanded a better explanation.

Unapoandika utafiti wako,kumbuka asilimia lazima ziendane na namba ya sample uliwahoji,otherwise iwe inajulikana na watu unawaandikia utafiti huo.
 
Unapoandika utafiti wako,kumbuka asilimia lazima ziendane na namba ya sample uliwahoji,otherwise iwe inajulikana na watu unawaandikia utafiti huo.

Ndio hapo nashangaa watu wanaandika asilimia zote hizi bila ya kuweka asilimia hizi ni za watu wangapi (what is 100%?)

Otherwise utafanywa utafiti wa watu wawili, muandishi na mkewe, halafu tutaambiwa Watanzania 100% wanaipenda CCM.
 
nacho amini kuna watu watajitolea kufanya kufanya utafiti na tutapata matokeo mazuri juu ya hali ya siasa hapa nchini
 
Mkuu Regan Morgans, kama haya ni matokeo ya utafiti, sasa hii ya wewe kuuliza kama jee ni kweli, unamaana unamashaka na utafiti huu wa Synovate?.




Kwa kusaidia tuu, sio tuu ni kweli kabisa kuwa EL anaanza kukubalika
zaidi, bali baadhi ya Watanzania wanaanza kuukubali ukweli kuwa EL ni jembe la ukweli!.

Haya maroroso tunayoyashuhudia katika kuporomoka kwa elimu yetu ni baadhi tuu ya matokeo ya serikali dhaifu ya JK kuitelekeza mipango ya EL na shule za kata ili kumkomoa, sasa imejikuta yenyewe ndio inakomoleka na kufikia 2015, EL atakuwa juu kabisa on top of the charts ili kufungua tuu njia na kunyoosha mapito ya "the chosen one!".

" Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Yeye ndie ule mwamba wa Kaskazini unaozungumziwa kwenye maandiko mbalimbali kuwa
"Wewe ni mwamba, juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!".

Pasco.

Kaka kaka!!acha kutumika kaka,kwel kufel kwa wanafunzi ni swala la kuunda tume?hivi huyu jamaa ako ndo kaona sululisho?tume kuchunguza nin sasa
Hajui walim wako ktk mgomo barid au vp,hajui shule za serikal zimeekwa rehan na hao hao yy akiwa anamilik shule za alpha,kwanin anaeka biashara ktk elim?au hujui miundombinu ya shule za serikal?vip malimbikizo na mishahara ya walim?kaka swala la kukosekana mitaala vp?
Kaka umesahau kbsa jamaa yupo ktk serikal miaka zaid ya 25a?kafanya nin zaid ya kuiba mali za umma..
Kaka sisi vijana kaka,ukila leo mil 10 hizo hazikupelek popote zaid ya kupata nuksi na mikos toka kwa watz na zitarudia familia yako siku moja


Don't expect honestly from cheap people!!don be cheap
 
Kaka kaka!!acha kutumika kaka, ukila leo mil 10 hizo hazikupelek popote zaid ya kupata nuksi na mikos toka kwa watz na zitarudia familia yako siku moja

Don't expect honestly from cheap people!!don be cheap
Mkuu Mwakichi, kumbe Pasco wa jf anatumika?!, analipwa milioni 10 ambazo hazimpeleka popote zaidi ya kupata nuksi na mikosi (kama ile ajali!), na na kuirudia familia yake!.

Haya, nimekubali kama niko cheap kwa kulipwa milioni 10, hivyo nisiwe cheap, nitapaswa kulipwa ngapi?.
Pasco.
 
Naomba nisaidiwe, nini maana ya mfumuko wa bei?

Maana binafsi nadhani anaposema gharama za maisha kupanda ni amezunguka kwenye kuelezea matokeo ya mfumuko wa bei!!
Au ninakosea wakuu?


Halafu ndio wanakuja na maneno kuwa

"..njaa ndio imeongoza ikifuatiwa na gharama za maisha kupanda,
....rushwa na mfumuko wa bei havichukuliwi kama ni tatizo kwa watanzania kama ilivyojitokeza mwaka 2011"

Naona kama majibu yanaweza kutofautiana kutegemea na aina ya watu wanaohojiwa hivyo sidhani kama inaweza kuwa projected kuwa matokeo yako applicable kwa wote!!
 
Sikubaliani hata kidogo na matokeo niliyoyaona gazeti la leo la mwananchi kwani hao waliotolewa wote ni kwasababu ya kujuana na urafiki na kupigiana promo, mimi nasema huo ni utafiti feki mimi DEOGRATIUS KISANDU ndiye ninaye ongoza mpaka sasa kwa asilimia 35% lakini ukweli umefichwa.

Umeshikiwa akili wewe
 
Sikubaliani hata kidogo na matokeo niliyoyaona gazeti la leo la mwananchi kwani hao waliotolewa wote ni kwasababu ya kujuana na urafiki na kupigiana promo, mimi nasema huo ni utafiti feki mimi DEOGRATIUS KISANDU ndiye ninaye ongoza mpaka sasa kwa asilimia 35% lakini ukweli umefichwa.


Dx: Bipolar Disorder, manic episode.

Rx: 1. Psychotherapy
2. Benzodiazepine
3. Lithium
 
Nina wasiwasi na utafiti huu hasa kukubalika kwa Pinda. Pinda ni mwoga mno ambaye hana hata uthubutu wa kufanya maamuzi yanayofanya na naibu waziri. Hakuna lolote la maana ambalo amewafanyia watanzania. Umaharufu huu kaupataje?
 
WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.

Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).

Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.

Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.

Utafiti huo unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajabadilika tangu 2011katika taasisi za Serikali ukisema haionekani kama kuna utashi wa kisiasa kupambana na tatizo hilo katika taasisi hizo kama Jeshi la Polisi na Mahakama ambazo zimeonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.

Katika utafiti huo, polisi ndiyo inayoongoza kwa rushwa baada ya asilimia 33 ya watu waliohojiwa kulitaja jeshi hilo, ikifuatiwa na Mahakama asilimia 16 na sekta ya afya ikiwa na asilimia 16.

Utafiti huo umeonyesha matatizo makubwa yanayoikabili nchi kwa sasa ni njaa, gharama za maisha, umaskini, migogoro ya kidini na ukosefu wa ajira.

“Asilimia 50 wametoa maoni kuwa njaa ni tatizo kubwa ikifuatiwa na gharama za maisha asilimia 44, migogoro ya ya kidini asilimia 43 na ukosefu wa ajira asilimia 34.”

“Inamaanisha kuwa rushwa na mfumuko wa bei havichukuliwi kama ni tatizo kwa Watanzania wengi kama ilivyojionyesha mwaka 2011,” inaeleza taarifa ya utafiti huo.

Wananchi wameeleza kuwa mambo muhimu ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya afya kwa asilimia 24, elimu asilimia 21, ajira asilimia 18, chakula asilimia 17 na miundombinu asilimia 16.


Source: Mwananchi

kweli kama huoni na una macho,huwezi ona hata ukionyeshwa, hivi kweli unaweza je kusema Magamba wanakubalika na uchafu wote unaoendelea kufanyika hapa nchini??
else, you are not a natural citizen of this country, kweli mshasahau ya muhimbili na wagonjwa kufa bila hatia?
ya walimu kuteswa kwa kutokupewa maslahi on time na yanayokidhi maisha yao?
kweli kwa wanafunzi kupigwa mabomu ya machozi kwa kudai mikopo?
na je kupe mabwe pande mlisha sahau???????
vpi hao wanaochinjwa na kupigwa risasi kila kukicha?
na serikali iliyopo madarakani wala haitoi tamko kana kwamba kila mtu ni Rais wake mwenyewe???
wacheni uhuni kutuzuga na kutupotezea maboya, hizi sio zama za bendera na upepo, kajipangeni mlete taarifa inayoeleweka,

kwa hyo magamba wamepanda kwa kukubalika kwa 1%??
hehhehhehe, hii Synovate naweza kusema ni taasisi inayomilikiwa na sisiemu, kwa muonekano tu lazima mtu uwaze hivyo.
 
ninapokosa imani na watafiti hawa inakuwa ngumu kuamini utafiti wao.
[FONT=courier
new]WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza
kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015,
Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao
unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa
angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa
anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia
tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25
ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo
mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka
juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa
alizopata katika utafiti uliotangulia.

Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa
Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7)
na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4)
na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).

Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia
tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na
Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki
katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa
kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni
ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya
wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia
moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka
kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka
jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na
kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya
Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama
uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka
2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama
chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.

Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu
10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia
asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema
imepungua na asilimia tano hawajui.

Utafiti huo unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajabadilika
tangu 2011katika taasisi za Serikali ukisema haionekani kama kuna utashi
wa kisiasa kupambana na tatizo hilo katika taasisi hizo kama Jeshi la
Polisi na Mahakama ambazo zimeonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.

Katika utafiti huo, polisi ndiyo inayoongoza kwa rushwa baada ya
asilimia 33 ya watu waliohojiwa kulitaja jeshi hilo, ikifuatiwa na
Mahakama asilimia 16 na sekta ya afya ikiwa na asilimia 16.

Utafiti huo umeonyesha matatizo makubwa yanayoikabili nchi kwa sasa ni
njaa, gharama za maisha, umaskini, migogoro ya kidini na ukosefu wa
ajira.

“Asilimia 50 wametoa maoni kuwa njaa ni tatizo kubwa ikifuatiwa na
gharama za maisha asilimia 44, migogoro ya ya kidini asilimia 43 na
ukosefu wa ajira asilimia 34.”

“Inamaanisha kuwa rushwa na mfumuko wa bei
havichukuliwi kama ni tatizo kwa Watanzania wengi kama ilivyojionyesha
mwaka 2011,” inaeleza taarifa ya utafiti huo.

Wananchi wameeleza kuwa mambo muhimu ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele
ni pamoja na sekta ya afya kwa asilimia 24, elimu asilimia 21, ajira
asilimia 18, chakula asilimia 17 na miundombinu asilimia
16.
[/FONT][FONT=Times New
Roman]
[/FONT]

Source:
Mwananchi
 
Wamejitahidi kuchakachua asilimia za Dr. Slaa wakabakiwa na 17%! Yaani alipopambana na reigning president alikuwa juu, leo hii ashuke! Synovate acheni kutumiwa bana semeni ukweli halisi maana mmejua tofauti na kuonyesha Dr anaongoza wananchi wangewadharau maana huo ndio ukweli ambao hata kipofu anauona.

"Hii ndio Bongo land kila kitu lazma kiongezewe chumvi"
 
Back
Top Bottom