SYNOVATE & REDET 'kupika' taarifa ya hali ya kisiasa nchini

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
705
440
Taarifa nilizozipata kutoka Idara ya Mawasiliano(Somewhere) inaeleza kuwa Serikali imejipanga kujisafisha na kashfa za mchafuko wa hali ya kisiasa na ukiukwaji mkubwa wa haki za Binaadam uliofanywa na Polisi hivi karibuni katika mikoa ya Morogoro na Iringa.
Mkakati huo ni kuwa,Taasisi hizo mbili zitafanya utafiti na baadaye kutoa majibu ya kuisafisha serikali kama vile;
1. Ripoti itaonyesha kuwa Hali ya amani ya Taifa ni zaidi ya 98% (Kulingana na vyombo vya usalama na baadhi ya Raia watakaohojiwa)
2. Ripoti yao itaonyesha kuwa bado watanzania wengi wana imani na Serikali iliyopo kwa zaidi ya 90%
3. Ripoti itaonyesha kuwa bado wananchi wana imani na wanaonyesha ushirikiano na kwa Jeshi la Polisi kwa zaidi ya 88%
4. Ripoti itaonyesha kuwa chama cha Mapinduzi bado kinapendwa na wananchi wengi walio vijijini kwa 95% huku mijini Chama hicho kikikubalika kwa 85%
5. Ripoti hiyo itaonyesha kuwa Wananchi wengi bado wanamkubali Rais Kikwete kwa 91% dhidi ya Katibu mkuu wa CHADEMA Mhe.Dr.Slaa ambaye ataambulia 9% tu.
Ripoti hiyo itagusia pia masuala ya uwajibikaji wa wabunge na bunge kwa ujumla, kupungua kwa hali ya rushwa nchini;NK.

Ripoti hizo zitatolewa na kupelekwa hata kwa nchi wafadhili kwa lengo la kuwahakikishia kuwa bado Tanzania iko salama na Amani ya kudumu bado ipo.

My take:
Hizi taasisi zikikubali kutekeleza 'Mkakati' huo zitakuwa zimepoteza credibillity ya kuitwa taasisi.
 
Tuanze kuwabandikia data za watu waliuawa kwa kuchukua sheria mkononi. Au walioteswa kinyama. Naanza

Dr Stephen Ulimboka.
 
CCM's political machination has long proved malfunctioned, of coz in a big time style! BTW REDET na Dr. Bana walishapoteza sehemu kubwa ya credibility hasa 2010 na 2011....so kwao ni "liwalo na liwe".

Strategists wa CCM wamefika mwisho wa ukomo wao. Wakati huo huo wananchi tumekataa kuoshwa akili zetu iwe kwa kauli au picha au fedha chafu (rushwa). Muda huu CCM wanatapa tapa na kurusha silaha zao za mwisho zenye nguvu nazo ni kutumia taasisi za serikali kama TISS, Majeshi, Bunge, vyombo vya habari kutafuta uhalali wa utawala wao dhalimu. Nazo zinaelekea kushindwa kwa kishindo cha tsunami.

Wakabidhi nchi hii kwa amani na ustaarabu, that's all left for them.
 
Mkuu Mallya ahsante kwa taarfa ila hebu niweke waz Jk anakublka kwa asilimia 91 dhidi ya dr. Slaa 40% kimahesabu napata utata! Hebu sahsha habar yako sehmu nyng 2!
 
Zama za kupika kupika zishaisha......magamba yajiandae kwe the hegae tu....mkama na nape watafanywa kama alivyofanywa katibu mukk wa chama cha BAGBO wa ivory coast
 
Jana hawakujifunza kwa msajili wa vyama vya siasa nchin Tendwa?

Tutawasikia huko tuendako, kama walimuona Tendwa akitendwa kwa kunyolewa bila kutia maji, itakuwa bora kwao kuanza kutia maji iwe nafuu yao, kinyume na hapo watanyolewa mazimamazima wakiwa wakavu vichwani mwao.
 
Hawa jamaa can prove anything with statistics except the truth. Ukweli hawataji kabisa!
 
Benson Bana nasikia ameshaandaa hiyo ripoti atawapatia tu waisome mbele ya wanahabari.
 
Jana hawakujifunza kwa msajili wa vyama vya siasa nchin Tendwa?

Tutawasikia huko tuendako, kama walimuona Tendwa akitendwa kwa kunyolewa bila kutia maji, itakuwa bora kwao kuanza kutia maji iwe nafuu yao, kinyume na hapo watanyolewa mazimamazima wakiwa wakavu vichwani mwao.

Mkuu kati ya Siku ambazo John Tendwa hatazisahau kwenye maisha yake ni jana!.. Alikuwa kwenye wakati mgumu kuliko siku nyingine yoyote!..
 
Kama wanaweza kupika matokeo ya uchaguzi mbele ya macho ya watu sembuse hizo za utafiti?
 
Back
Top Bottom