Swali?

Swali?

SAMWEL SAINA

New Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2
Reaction score
0
Fafanu chimbuko na asili ya lugha ya kiswahili na eleza kwa mf;Kabla ya kuja kwa wageni katika upwa wa afrika mashariki ni lugha gani ilikua ikitumika enzi hizo?
 
Fafanu chimbuko na asili ya lugha ya kiswahili na eleza kwa mf;Kabla ya kuja kwa wageni katika upwa wa afrika mashariki ni lugha gani ilikua ikitumika enzi hizo?

Bila shaka huko mwanzoni pwani lilikaa peke yake bila mtu yeyote, lugha ya pekee sauti ya upepo na mawimbi ya bahari.

Baadaye kila mmoja alikuja kama mgeni: Labda huko manzoni homo erectus na homo sapiens akielekea kaskazini kutoka asili yake katika Afrika. Walisema wakati ule? hatujui. Baadaye mababu wa Wahadza na Wasandawe walifika na pwani ilisikia sauti za "klik".

Baadaye wageni wengie, akina Wabantu na mababu wa Wasomali walifika. Wakati ule bila shaka walikuwa na lugha zao mbalimbali.

Baadaye wageni wengine kutoka kaskazini walifika kwa mashua na jahazi, kati ya hao ni hasa Waarabu na Waajemi waliocha maneno mengi katika lugha za watu waliotangulia kuunda vyanzo yva lahaja mbalimbali za Kiswahili... (takriban asilimia 30-40 za maneno ya Kiswahili zimetoka kwao)

Baadaye wageni tena Wareno (walioacha maneno machache tu kama vile bendera, meza...) , Wajerumani (walioacha tu "hela" na "shule"), Waingereza walioacha tena maneno mengi.

Tuone kama Wachina wataacha maneno pia..... (walipofika mara ya kwanza miaka 600 iliyopita hawakuacha neno..)

Kila kundi lililofika lilifika kama wageni siku moja.
Lakini sauti ya upepo na mawimbi ya bahari zimeendelea hadi leo.
 
Back
Top Bottom