Barelawyer
Senior Member
- Oct 11, 2012
- 195
- 68
Vipi kuhusu wahindi??
wao upande wa ukeni wanapeleka mahari upande wa uumeni!!..
imekaaje hiyo
wao upande wa ukeni wanapeleka mahari upande wa uumeni!!..
imekaaje hiyo
Watu wakishamsahau Mungu na habari zake ndio huanza kuwaza mada kama hizi. Inasikitisha zaidi wazo kama hili linatoka kwa mwanamke, huyu nadhani hajui uthamani na yeye kuitwa mtu mke.
Mimi ni Mkristo na biblia inasisitiza sana jambo la mahari, ninaamini hata wenzetu Waislamu watakuwa na mafundisho yenye kueleza umuhimu wa mahari.
Mahari huonesha uthamani wa mwanamke na ni kama shukrani kwa wazazi wa mwanamke kwamba walikutunzia vyema kiumbe ambaye wewe(mwanaume) umemuona afaa kuwa mke.
Hata kabla dini hazijaingia kwenye mila zetu, bado familia za kiumeni zilikuwa zinatoa mahari, na wakati huo mtoto wa kike alikuwa anachumbiwa akiwa bado mdogo.
Ndoa ilikuwa ni sehemu ya kudumisha urafiki, mshikamano baina ya koo na koo au familia na familia.