Swali ya Wanaume wenye ndoa swala la Mahari mnalionaje?linepitwa na wakati au ?

It depends na interpretation ya hao unaowapelekea mahari I guess!!!
 
Mahari kitu gani, wazazi kuendekeza njaa sasa. Nilimkomalia mke wangu hakuna kutoa mahari. Baba mkwe aligoma ila badae akaingia laini. Msitoe mahari.
 
Dawa ni kutia mimba aafu unawambia kama mnataka kuniuzia mwanenu kaeni naye basi! Mambo gani ya kuuziana watu mpaka leo? Watu wenye wakija kwetu ndugu zetu wanawafukuza wanajaza wa kwao tu! Lazima wazazi waachane na hizi mila za kufirisi vijana. Na wazazi wanaolazimisha mabinti zao kuolewa kwa harusi acheni hizo! Mnatuingiza wanenu kwenye madeni yasiyokuwa na msingi.
 
Mimi wazazi wangu walikataa na ninaona Kama vimepitwa na wakati vile.Nia yake ninini haswa?
Hahahaha waliona mbali aisee.. Jamaa wanaweza kuja kudai chao.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hakuna kitu kama hiki kinachonikera kwenye jamii tena usukuma wanataka ng'ombe kumi na kuendelea...
 
Mahari ni desturi iliyopitwa na wakati!

Ni kumkamua mwanaume na kumdidimiza mwanamke!

Haitawezekana nikulipie(nikununue) halafu ndani ya nyumba tuwe sawa(gender balance)...never!

Sikuwahi kufurahia mahari kwani nilitoa kiasi kikubwa kipindi bado nahitaji kujijenga,wakati mwingine inajenga hisia mbaya kwa wakwe na kujikuta mzito kusaidia upande wa mke(hasa wanapodai mahari kubwa)
 
Watu wakishamsahau Mungu na habari zake ndio huanza kuwaza mada kama hizi. Inasikitisha zaidi wazo kama hili linatoka kwa mwanamke, huyu nadhani hajui uthamani na yeye kuitwa mtu mke.
Mimi ni Mkristo na biblia inasisitiza sana jambo la mahari, ninaamini hata wenzetu Waislamu watakuwa na mafundisho yenye kueleza umuhimu wa mahari.
Mahari huonesha uthamani wa mwanamke na ni kama shukrani kwa wazazi wa mwanamke kwamba walikutunzia vyema kiumbe ambaye wewe(mwanaume) umemuona afaa kuwa mke.

Hata kabla dini hazijaingia kwenye mila zetu, bado familia za kiumeni zilikuwa zinatoa mahari, na wakati huo mtoto wa kike alikuwa anachumbiwa akiwa bado mdogo.
Ndoa ilikuwa ni sehemu ya kudumisha urafiki, mshikamano baina ya koo na koo au familia na familia.
 
kwa utaratibu wa zamani lilikuwa ni jambo zuri sana hasa kujenga ushirikiano wa wazazi,na ili binti aolewe inatakiwa awe mwenye maadili,kwa hiyo inapotokea wazazi wamemlea binti yao vizuri hadi akafikia wakati wa kuolewa ilionyesha kuwa ni vizuri kutoa zawadi fulani kwa wazazi wa binti kuwapongeza kwa kazi waliyofanya,na kimsingi haitakiwi kulipwa yote ni kiasi fulani tu cha gharama iliyotajwa,lakini siku hizi tafsiri yake imebadilika,watu wanapanga mahali utadhani ng'ombe anathaminishwa mnadani au kama vile kuikomoa familia ya muoaji,na wanakomalia pesa iliyotajwa lazima ilipwe yote,hapa hakuna mila tena ni kimaslahi zaidi, jamii inatakiwa ielimishwe kuhusu suala hili.
 
Hili jambo halijaanzishwa na wanadamu bali ni utaratibu uliowekwa na Mungu kwa wale wenye imani na dini. tatizo ni pale wanadamu wanapolifanya kama sehemu ya kujipatia mali zaidi toka kwa mkwe, hapo ndio kwenye tatizo linalohitaji mjadala na sio kuondoa kabisa suala la mahari. ila kwa wale wasio na imani za dini wanaweza wasione umuhimu wake.
 
Kwangu mimi ni dini zaidi...sio kumnunua bali ni kama zawadi ya mke mtarajiwa.
 
Heshima sana, sikubali kupewa mke bila kutoa 'kazawadi'. Hasa kale kasikokwisha, yaani deni linaendelea tu kuwepo!
 
Mimi wakwe zangu walikataa nisimlipie binti yao mahari...

Basi mm nkachelea kimoyomoyo nkakumbuka ile methali "akunyimaye mbaazi....."

Hii kitu imepitwa na wakati.
 
Heshima sana, sikubali kupewa mke bila kutoa 'kazawadi'. Hasa kale kasikokwisha, yaani deni linaendelea tu kuwepo!

wazazi wa siku hizi hawataki tena hayo. Wanapanga mahali kubwa aafu wanataka utoe cash na ziishe zote na uthaminishe na bei ya ng.ombe wa mnadani. Zamani ilikuwa wakisema ng.ombe watatu basi mnapeleka mmoja na kuwaambia waliobaki tutamalizia. Siku hizi imegeuzwa kama mtaji wa watu kutokea na omba pasiwe na kijana wa kiume asiyeeleweka watataka wewe ndo uwe mtaji wake wa kutokea kimaisha.
 
Ila jamani wazazi wakulelelee mama watoto wako,, wakusomeshee kwa shida hadi mnakuja kukutana vyuoni sijui maofisini binti ameshaiva na kupendeza we bado hutaki kutoa shukrani..

Unafikiri hizo million sijui moja,2 au 3 za mahali zinarudisha gharama zote walizopitia...

MKATA KIU naoa binti wa kinyaturu nimepigiwa hesabu ya ngombe, sijui vikorokoro gani lakini nimetoa kwa raha zote japokuwa kuna vitu wananidai na shemeji yangu alishanielekeza nisimalize deni siku ya mahali,, la sivyo ningeclear kila kitu,, unafanya mchezo nini na kukuziwa ubavu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom