Swali ya Wanaume wenye ndoa swala la Mahari mnalionaje?linepitwa na wakati au ?

Vipi kuhusu wahindi??
wao upande wa ukeni wanapeleka mahari upande wa uumeni!!..
imekaaje hiyo
 
Watu wakishamsahau Mungu na habari zake ndio huanza kuwaza mada kama hizi. Inasikitisha zaidi wazo kama hili linatoka kwa mwanamke, huyu nadhani hajui uthamani na yeye kuitwa mtu mke.
Mimi ni Mkristo na biblia inasisitiza sana jambo la mahari, ninaamini hata wenzetu Waislamu watakuwa na mafundisho yenye kueleza umuhimu wa mahari.
Mahari huonesha uthamani wa mwanamke na ni kama shukrani kwa wazazi wa mwanamke kwamba walikutunzia vyema kiumbe ambaye wewe(mwanaume) umemuona afaa kuwa mke.

Hata kabla dini hazijaingia kwenye mila zetu, bado familia za kiumeni zilikuwa zinatoa mahari, na wakati huo mtoto wa kike alikuwa anachumbiwa akiwa bado mdogo.
Ndoa ilikuwa ni sehemu ya kudumisha urafiki, mshikamano baina ya koo na koo au familia na familia.

usasa ukipitiliza ndo utaona watu wanapinga mahari
 
Mahari ni nzuri na inaleta maana pale tu ikiwa kwa kiwango kinachopatikana kwa urahisi kwa mtoaji na kikiwa katika mlengo wa kuunganisha hizi familia/pande mbili zaidi kuliko kufikiria kupata faida katika hii transaction.
 
Kuna sehemu nimewahi kushuhudia inatolewa mahali ya TZS 60,000. sio kwamba watoaji ni maskini la hasha! Ni itifaki tu ilikuwa izingatiwe.
 
Mahari ni moja ya tamaduni ambazo zimepitwa na wakati na ndizo zinazochangia kutokuwepo na usawa wakati wengine wakitetea ziko hata katika vitabu vya dini wanasahau vitabu hivyohivyo vya dini vilisema mwanamke atakuwa chini ya mme na hata hivi vikundi vinavyotetea maswala ya usawa wa jinsia kwa makusudi wanakwepa kuzungumzia maswala ya mahari kama kulelewa au kufundishwa watoto wote wa kike na kiume walipata matunzo hayo huwezi kuniambia nilipie kiasi fulani na bado ukataka tuwe na maamuzi sawa kwa kifupi wanawake wanatakiwa kuanza kupigania vitu kama hivyo viondolewe kama kweli wanataka usawa
 
Kati ya vitu vinavyochekesha kwa watetezi wa mahari ni hizo ngonjera eti binti ametunzwa, amesomeshwa na bla bla kibao! Hivi mnataka kusema kuwa wazazi wa mvulana hawajamtunza wala kumsomesha?! Na kwa wanaokimbilia kwenye Bible, kiasi cha mahari ya kwenye Bible kilitajwa kabisa wala siyo huu uchuro wa ng'ombe 20 au milioni kadhaa za shilingi...
 
mimi nikitaka kuoa nitatoa mahari,haya mambo ya kutokutoa ni uhuni tu na kutaka kupoteza heshima ya mwanaume ndani ya nyumba,mana hawa wanawake wa siku hizi walivyo na kiburi sasa usipotoa si ndio utakoma?
 
Kati ya vitu vinavyochekesha kwa watetezi wa mahari ni hizo ngonjera eti binti ametunzwa, amesomeshwa na bla bla kibao! Hivi mnataka kusema kuwa wazazi wa mvulana hawajamtunza wala kumsomesha?! Na kwa wanaokimbilia kwenye Bible, kiasi cha mahari ya kwenye Bible kilitajwa kabisa wala siyo huu uchuro wa ng'ombe 20 au milioni kadhaa za shilingi...
 
Hakuna kitu kizuri kama kufuata procedure hata ndani ya jamii unaheshimika,wewe katoe mahari acha short cut ndugu yangu
 
Nilimsikia Diva wa clouds fm akisema yeye bila million 500 haolewi!!nikasema sasa hii mahari unaoa rais
 
Back
Top Bottom