Swali la Yesu ambalo linakufunga mdomo

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,299
3,411
Siku moja Yesu katika harakati zake ,Wayahudi hasa mafarusayo wale ambao hawakumuelewa hasa kuhusu Asili yake ,aliwatandika Swali ambalo liliwaziba mdomo

Hawa Wayahudi walikuwa wanajifanya wanayaamini maandiko asilimia 100, Na Yesu alikuwa hasumbuani nao Sana anawatandika kwa maandiko

Kisa kinaanzia hapa

LUKA 20

41Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi:
‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia
43mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’
44Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?”

WAYAHUDI walikuwa na doubt Sana kuhusu hasa Uungu wa Yesu, Sasa kuwafunga midomo anawarejesha katika Moja ya Kitabu wanachokiamini yaani Zaburi

Zaburi 110
1 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.

Lakini Zaburi ina andiko hili ambalo lashahabihana na Hilo

Zaburi 45:7
Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

Kwa Yesu kuwapiga Wayahudi kwa Maandiko haya walipoonesha mashaka kuhusu Uungu wake ,

Mathayo ndiye Kaelezea vzr hiki kisa

Mathayo 22

44 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia,
mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
45Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?”
46Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.

MWISHO INAONESHA KABISA WALIZIBWA MIDOMO NA ANDIKO LINASEMA

Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
 
Wale watu wa mihadhala maandiko kama ilo uwa wanayaruka kama hawayaoni.
Wajinga sana hao watu.
Huwenda wewe ndiyo mjinga,aliyelia msalabani 'mungu wangu mbona umeniacha' ni nani!?..aliyesema 'sikutumwa Ila kwa kondoo waliopotea wa Israel' ni Nani!?..katumwa na nani!?..mwerevu wewe endelea kuamini fundi seremala alikua mungu
 
Swali hilo rahisi sana, Yesu ni mwana wa Daudi kimwili, na ni Bwana wa Daudi kiroho.

Kwa njia ya kimwili Yesu ni mwana wa Daudi sababu Yesu alizaliwa toka kwenye uzao wa Daudi. Soma Mathayo 1 kuendelea

Kwa njia ya kiroho Yesu ni Bwana wa Daudi sababu, Yesu ni Mungu Muumba wa mbingu na nchi, hivyo alifanyika kuwa mwanadamu kupitia uzao wa Daudi ili aje kutuokoa wanadamu toka kwenye dhambi Jackwillpower
 
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Kumtoa kafara mwanae wa pekee Kwa ajili ya dhambi za watu badala ya kumtoa kafara shetani

Haki ya mungu Kuna kitu hakipo sawa hapa
Haujawai sikia baba kafa akimuokoa mtoto wake kama umewai sikia , huo unaitwa upendo
 
tulishakatazwa kuchangia mijadala ambayo mwisho wa siku huishia kutukanwa Mungu wetu na mtume wetu
 
Huwenda wewe ndiyo mjinga,aliyelia msalabani 'mungu wangu mbona umeniacha' ni nani!?..aliyesema 'sikutumwa Ila kwa kondoo waliopotea wa Israel' ni Nani!?..katumwa na nani!?..mwerevu wewe endelea kuamini fundi seremala alikua mungu
Aliyelia ni Yesu Kristu mwenye umbile la kiubinadamu, na alilia kuonesha maumivu aliyopata ndio tunayopata sisi wanadamu, pale aliondolewa uungu auvae uanadamu ili kweli maana ya kuukomboa ulimwengu idhihirike.

Kama Yesu Kristu angeendelea kubaki na uungu wake, hakika nakwambia, tena nakwambia na wenzako wote wenye mawazo kama yako wasikie, wasome, na wajue, HAKUNA YEYOTE AMBAYE ANGETHUBUTU KUMSOGELEA NA KUMSULUBISHA, hayupo.

Kwani kabla ya kumsulubisha walishamuona wakamuuliza wewe ndie Yesu Kristu wa Nazareth, akawajibu mimi ndie, WOTE WAKARUDI NYUMA WAKAANGUKA CHINI, bila yeye kuwagusa au kuwapuliza popote.
 
Siku moja Yesu katika harakati zake ,Wayahudi hasa mafarusayo wale ambao hawakumuelewa hasa kuhusu Asili yake ,aliwatandika Swali ambalo liliwaziba mdomo

Hawa Wayahudi walikuwa wanajifanya wanayaamini maandiko asilimia 100, Na Yesu alikuwa hasumbuani nao Sana anawatandika kwa maandiko

Kisa kinaanzia hapa

LUKA 20

41Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi:
‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia
43mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’
44Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?”

WAYAHUDI walikuwa na doubt Sana kuhusu hasa Uungu wa Yesu, Sasa kuwafunga midomo anawarejesha katika Moja ya Kitabu wanachokiamini yaani Zaburi

Zaburi 110
1 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.

Lakini Zaburi ina andiko hili ambalo lashahabihana na Hilo

Zaburi 45:7
Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

Kwa Yesu kuwapiga Wayahudi kwa Maandiko haya walipoonesha mashaka kuhusu Uungu wake ,

Mathayo ndiye Kaelezea vzr hiki kisa

Mathayo 22

44 ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia,
mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
45Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ anawezaje kuwa mwanawe?”
46Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.

MWISHO INAONESHA KABISA WALIZIBWA MIDOMO NA ANDIKO LINASEMA

Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.

Em
Muuweni shetan na huyo yesu wenu
 
Aliyelia ni Yesu Kristu mwenye umbile la kiubinadamu, na alilia kuonesha maumivu aliyopata ndio tunayopata sisi wanadamu, pale aliondolewa uungu auvae uanadamu ili kweli maana ya kuukomboa ulimwengu idhihirike.

Kama Yesu Kristu angeendelea kubaki na uungu wake, hakika nakwambia, tena nakwambia na wenzako wote wenye mawazo kama yako wasikie, wasome, na wajue, HAKUNA YEYOTE AMBAYE ANGETHUBUTU KUMSOGELEA NA KUMSULUBISHA, hayupo.

Kwani kabla ya kumsulubisha walishamuona wakamuuliza wewe ndie Yesu Kristu wa Nazareth, akawajibu mimi ndie, WOTE WAKARUDI NYUMA WAKAANGUKA CHINI, bila yeye kuwagusa au kuwapuliza popote.
Uharo tu
 
Back
Top Bottom