Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
a. Wale kina dada/mama wanaweza kuwa wako huru kuwa na mapenzi na mabosi wao au wametumiwa kwa sababu ya uhusiano wa kikazi uliopo na ilikuwa vigumu kwao kukataa au kuacha?
b. Mwanamke ana njia gani ya kudai malezi ya mtoto kwa njia za kisheria (kupitia ustawi wa jamii) bila wakati huo huo kuweka hatarini ajira yake?
c. Kama bosi anahama kwenda sehemu nyingine kikazi na kusababisha mahusiano yale kuvunjika (au ya mbali) mwanamke mwenye mtoto ana namna gani ya kudai malezi au kuendelea na mahusiano na mtu ambaye siyo bosi wake tena?
d. Mtoto anayezaliwa katika mahusiano ya namna hiyo anaweza vipi kuanza kudai kumjua baba yake hasa kama baba hakumkubali au mama hakumwambia kwa kuhofia ama kumtibua mzazi mwenzie au kujikuta anamdhalilisha?
e. Mababa ambao ni mabosi na wamezaa nje ya ndoa zao, wanatakiwa kulazimishwa na sheria kuhakikisha wanahudumia watoto wao wengine kama vile kukata mishahara yao na kulazimisha watoto wawe kwenye bima zao za afya?
MMM