Kaka namna unavyofikiri wewe ni tofauti sana na watu wengi, kwa hiyo hapa sana sana watakushangaa tu kwa kuuliza swali hili. Lakini ni swali la msingi kabisa, yeah ni kwanini wapige kelele??!! Jibu la haraka haraka ni mazoea tu. Wengi wetu tunafanya mambo mengi kimazoea na ndiyo maana tunachanga fedha nyingi kwa ajili ya harusi si kwa sababu tunahitaji sana hizo harusi bali ni mazoea tu.