Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani?

Waandishi wengine wavumilieni bure tu maana wanaandika kwa kutaka sifa.
Miaka ya Mwalimu wakati kuna suala tete mobilisation ya kitaifa alikuwa anaandika mwenyewe tahriri ya habari ili jamii tuwe na msimamo mmoja.

Sasa hili la Mwanakijiji kutaka kuonekana kupinga kila kitu kinamwonesha in a different light.
Aidha ni mwoga, au ni fifth columnist au analipwa kufanya hivyo.
Kwa vyovyote vile hali ya kiuchumi ya Tanzania leo ni much better off kuliko 1978, na vile vile kama vita itazuka, wapenda nchi wataenda mbele.

Makala kama hizi za Mwanakijiji kwa kweli zinaonyesha mtu mwenye akili inayomfaa yeye mwenyewe na hali ikiwa mbaya zaidi mpakani, itachukuliwa kuwa inamsaidia adui.
Isome vizuri heading ya thread hii kisha usome na bandiko lote jinsi lilivyo. Malawi wanatudharau sana kama kauli ile ya Lowasa imetoka kwa mtu mwenye uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi yetu.
 
Nashukuru,lakni wakati ukifika kila ulio mtaja hapo juu ndio utajua nafasi yake,ukishajua nafasi zao ndio uje uniulize tena ni Nani Amiri Jeshi Mkuu.SISI NI WATU WA VITENDO KWA MASLAHI YA NCHI NA WATU WAKE BILA KUJALI KUNA WANANCHI WAJINGA NA MTAILA KAMA WEWE
Badala ya kutukana jibu hoja tu. Mwanajeshi asiyejua amri halali inatolewaje na nani anaitoa huyo hatufai. Nenda kajiunge na makampuni binafsi ya ulinzi . Yako mengi tu sasa
 
Isome vizuri heading ya thread hii kisha usome na bandiko lote jinsi lilivyo. Malawi wanatudharau sana kama kauli ile ya Lowasa imetoka kwa mtu mwenye uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi yetu.

mkuu naomba nikuulize maswali machache unayajua matamko/amri wanayopewa askari kwenda vitani?unazijua ngazi za amri na hamasa ngazi kwa ngaz toka juu hadi chini za kijeshi hasa wakati wa kwenda vitatani?
 
Badala ya kutukana jibu hoja tu. Mwanajeshi asiyejua amri halali inatolewaje na nani anaitoa huyo hatufai. Nenda kajiunge na makampuni binafsi ya ulinzi . Yako mengi tu sasa

unaijua amri halali ni ipi?na unajua amri halali ya kwenda vitani inatowaje na wakati gani?...upuuzi wako unakutesa sana pole sana
 
Katiba ya JMT imelieleza wazi hili. Akina Sitta, Membe na Lowasa wangeyasema hayo waliyoyasema nje ya Bunge tungeomba wakamatwe, washtakiwe na wafungwe bila faini!
 
Badala ya kutukana jibu hoja tu. Mwanajeshi asiyejua amri halali inatolewaje na nani anaitoa huyo hatufai. Nenda kajiunge na makampuni binafsi ya ulinzi . Yako mengi tu sasa

Kwa sisi tuliopitia mafunzo ya kijeshi tunajua kwamba ukijua nia na madhumuni ya adui, na unajua kwamba lengo ni kukuangamiza, kitu cha kwanza ni kumiminia risasi kichaka hicho.
Kuuliza baadaye.
Moral is: adui is dead you are alive.
 
Isome vizuri heading ya thread hii kisha usome na bandiko lote jinsi lilivyo. Malawi wanatudharau sana kama kauli ile ya Lowasa imetoka kwa mtu mwenye uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi yetu.

Hilo andiko limekaa ki-fifth columnist.
No proud Tanzania will swallow that!
You may be.
 
Wakatinihuu najua itakuwa vigumu kwako kujitambua katika jambo ili lakini pia nafasi yako katika medani kijeshi ni ya kiwango gani?.Hivyo kukurupuka kwako juu ya mada hii ni uelewa mdogo.Umbumbu wa War studies and Strategies nalo ni tatizo na kama upo jeshini revist the background of the Israel vs Arabs wars,1st and the 2nd WWs.
 
Last edited by a moderator:
unaijua amri halali ni ipi?na unajua amri halali ya kwenda vitani inatowaje na wakati gani?...upuuzi wako unakutesa sana pole sana
Soma ibara ya 32 ya Katiba ya JMT. Sio Lowasa wa kutuambia Wanajeshi wako tayari kiakili. Kawaandaa yeye? Siku za hivi karibuni Wenyeviti wa Kamati hizi za Bunge wamekuwa wakifanya kazi si zao hata kidogo. Wanajipa mamlaka na madaraka ambayo hawana hata kwa kanuni za Bunge!
 
Katiba ya JMT imelieleza wazi hili. Akina Sitta, Membe na Lowasa wangeyasema hayo waliyoyasema nje ya Bunge tungeomba wakamatwe, washtakiwe na wafungwe bila faini!

ndugu hatuta fika popote kama nakuuliza hili unajibu lile,ndio unazihirisha wewe ni mpuuzi,hujui na hujui kama hujui,fahamu kwanza kama ufahamu upate kufahamishwa ili ujue usilolijua.byebye
 
Sijagusa sauala la "ziwa lao". Tusubiri mazungumzo yaamue kwani Tanzania haijawahi hata mara moja kukubali kuwa Ziwa Nyassa lote ni la Malawi.

Mkuu, Kawawa na Chief Mhaiki walishawahi kukubali kuwa ziwa lote si letu. Hizi zilikuwa kauli zao za Bungeni miaka ya sitini. Kuna mtu alifanya research juu ya mgogoro huo miaka ya nyuma sana na iliwekwa hapa JF in Pdf formatt.
 
KT0183.jpg

Mara zote wakiulizwa kuhusu mambo mbalimbali wanasema 'hawana fedha' na kuwa serikali ni maskini. Tumeona migomo ya madaktari, walimu na tishio la migomo ya wafanyakazi. Tumeona jinsi ambavyo wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa "serikali haina fedha" -sikiliza kwa makini majibu ya mawaziri Bungeni wanavyorudia suala hili. Wanasema "serikali ikiwa na uwezo" au "tunaendelea kutafua fedha kwa ajili ya mradi huo; tena za ndani na za 'washirika wa maendeleo'".

Kila ukiwauliza mengi ambayo hayaendi vizuri jibu lao ni "serikali yetu haina fedha" au "hali ngumu". Sasa leo hii serikali hii hii ambayo "haina uwezo" inadai ati iko tayari kwenda vitani. Wale ambao tulikuwepo wakati wa vita vya Uganda tunakumbuka gharama kubwa (great toll) ya vita ile kwa maisha ya wananchi hadi vijijini. Hakuna ambaye kwa namna yake hakusikia maumivu (pinch) ya vita. Na vita ilipokwisha gharama yake kwenye uchumi wetu na maendeleo ya watu wetu haikuweza kurudishwa kwa urahisi. Kwa karibu miaka minne (miwili ya vita na ile ya reconstruction) ilisababisha nchi yetu kurudi nyuma zaidi ya ilipokuwepo. Ni kweli tulishinda vita lakini kwa gharama kubwa sana siyo tu ya fedha bali pia ya watu.

Kwa wanaokumbuka historia ya Uganda mojawapo ya matukio ya vita ni vita ya kuichukua Lukuya (Battle of Lukuya) ni hapa kiasi cha wanajeshi wetu kiliposhtukizwa na wanajeshi mamluki wa Libya na kujikuta kinarudishwa nyuma kabla ya Brigedi ya 201 na 208 kujipanga upya na kuwashambulia mamluki hao na kuwashinda na kusafisha njia ya kwenda Kampala (baada ya kuchukua Entebbe na Jinja). Gharama ya fedha tu serikali ya Museveni ndio iliweza kuilipa Tanzania mwaka 2007! Ikumbukwe kuwa vita ya Uganda inakadiriwa kuigharimu Tanzania dola milioni 1 kwa siku na hizo zilitoka mifukoni mwetu (hatukuwa na wajomba). Leo hii tumepiga kelele kulipa dola laki moja kwa Symbion kwa siku. Fikiria Wamarekani kwenye vita ya Iraq walikuwa wanaunguza dola bilioni 1 kwa siku!

Nikiangalia hali hiyo najiuliza; hivi kweli kina Lowassa na wengine wanaoshabikia vita wanafikiria kweli gharama yake? Hivi kuna mtu amewahi kuuliza Tanzania ilipoteza askari wangapi vita ya Uganda? Hivi watu wanajua kuwa ili jeshi letu liende vitani ni lazima wale wote waliokuwa reserve nao wawe reactivated? Yaani kabla ya kwenda Vitani itabidi kwanza tuongeze askari wote kutoka kama 30,000 waliopo sasa hivi na kufikia angalau 150,000 hivi kuweza kushinda vita. Hawa tutakaowachukua wengi ndio wasomi wenyewe na wafanyakazi maofisini watabadilishwa na nani? Ikumbukwe kwenye vita ya Uganda hawakwenda JWTZ tu bali Mgambo, Polisi, Magereza na wale waliopewa mafunzo ya haraka haraka. Je tuko tayari kuleta "draft" ya kulazimisha wanaume wote wenye miaka 18 na zaidi kuingia kambini? au watu wanafikiria ni "JWTZ" ndio litaenda vitani wakati wengine tunacheza ping pong na kuchat kwenye JF juu ya maendeleo ya vita?

Ninachopinga kabisa na ninaona ni mambo ya hatari ni kuzungumzia masuala ya vita bila kuonesha fikara na hekima. Kabla haujaamua kwenda vitani jipe nguvu kwanza. Na hakuna nguvu kubwa zaidi kama nguvu ya kiuchumi. Lakini jambo jingine ambalo labda wengine wameshafikiria ni vikosi vyetu vitakula nini? Au watu wanafikiria wanajeshi wakienda vitani wanapewa zile ration tu? Pamoja na gharama nyingine zote je bado tutaweza kulilisha taifa letu wakati wa vita? Wapo ambao hawajui kuwa njaa ya mwanzoni mwa miaka ya 1980 sehemu kubwa pia ni matokeo ya vita ya Uganda? Je tuko tayari kula dona na yanga tena na kurudishwa kwenye ration kwa taifa zima na mambo yale ya duka la kaya? au watu wanafikiria wataendelea kula nyama choma jioni wakati vita inaendelea?

Tusianze kupiga ngoma za vita (we shouldn't beat the drums of war) kama hatuko tayari kuingia vitani. Ni uzembe na reckless na binafsi naamini viongozi wote watatu (Lowassa, Membe na Sitta) wanatia shaka kama wana hekima na busara ya kuwa viongozi wa taifa letu. Kiongozi hata mwenye uwezo kiasi gani ni lazima asite linapokuja suala la vita na siyo kusita kwa sababu ya woga lakini kusita kwa sababu ya kujua analiita taifa lake kufanya nini. Na anapozungumza vita awe na uhakika kabisa (absolute confidence) kuwa hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuepuka vita hiyo.

Kwa mara nyingine nawasihi watu wanaoshabikia vita kama njia ya "kulinda mipaka yetu" wafikirie kwa hekima kuwa zipo njia nyingine nyingi zaidi za kufanya hivyo ikiwemo mazungumzo na mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa. NI LAZIMA TUMALIZE NJIA ZOTE ZA AMANI (siyo mazungumzo tu) kabla hatujasema "we have had enough, we are preparing for war) na binafsi naamini kama tutaonesha hekima ya kutumia njia zote na busara ya kuepuka vita siku ikiitwa vita kweli kabisa tunaweza kwenda siyo kujihami tu bali kuiona Malawi kama tishio na kuanzisha an offensive assault ili kuliondoa tishio hilo mara moja na daima.

Nashauri vichwa vilivyotulia vizungumza lugha ya amani sasa hivi na kutuliza hizi ngoma za vita na mbiu za mapigano. Maana kama sasa hivi tu wanahangaika kulipa mishahara na kulisha taifa letu, sijui itakuwaje WAKATI WA VITA!

MMM
mkuu mimi sio siri watu wengi wanataka tuingie vitan ila baada ya kusoma haya maandish yako..nadhan ni busara na ni lazima tuepuke vita...umeongea ukweli mtupu!!
 
Wakatinihuu najua itakuwa vigumu kwako kujitambua katika jambo ili lakini pia nafasi yako katika medani kijeshi ni ya kiwango gani?.Hivyo kukurupuka kwako juu ya mada hii ni uelewa mdogo.Umbumbu wa War studies and Strategies nalo ni tatizo na kama upo jeshini revist the background of the Israel vs Arabs wars,1st and the 2nd WWs.

usilete porojo za historia na siasa katika hili.Naseama nyie wamalawi tutawapiga kwa dk 30 tu,we bwabwaja maneno mia hapa jf mim kitendo kimoja ulingon
 
Last edited by a moderator:
mkuu mimi sio siri watu wengi wanataka tuingie vitan ila baada ya kusoma haya maandish yako..nadhan ni busara na ni lazima tuepuke vita...umeongea ukweli mtupu!!

mkuu chukulia malawi amegoma kufikia mwafaka katika meza ya usululishi na anazi kurusha ndege zake what next?
 
Mzee Mwanakijiji huwa nakueshimu sana lakini leo umeongea pumba.Taaluma yako ya uandishi wa makala huishie huko huko.Wala hujui lolote juu ya Jeshi na hasa JWTZ,wala hujui hasa chanzo kilichokuwepo cha vita kati ya TZ na UGANDA,sanasana utaeleza ni mipaka lakini chanzo hadi kuwa mipaka ilikua nini hujui unaishia kubwabwaja.Labda ni kwambie jambo la msingi,kama mnatuchokoza mkazania hatutaweza kufanya lolote eti hatuna hela,tayari mmefeli vita,kwa taalifa tutawapiga ndani ya dk 30,naongea kama mmoja wa JWTZ,we kaongelee kwenxe magazeti mi ntaongea kwa vitendo,subiri utaniambia

Hapo kwenye red, sioni kama ni maneno yatokayo kwa mtu ambaye anajua hasa maana ya heshima ni nini....Inawezekana kabisa Mzee Mwanakijiji ameongea mambo usiyoyapenda lakini hilo halimfanya afanane na hayo maneno kwenye red.
Mimi nimependa alivyoongea, maana amejenga hoja nzito, lakini sikubaliane naye kwa sababu na mimi nina mtazamo tofauti na wa kwake, pamoja na kutofautiana huko bado siwezi kutumia maneno kama uliyoyatumia wewe dhidi yake.

Angalia hayo maneno kwenye green....huna unachokijua kuhusu Vita. Unanikumbusha mzee mmoja mwaka 2001 na moja wakati Marekani inakusanya wanajeshi wake kuwapeleka Afghanistan....yule mzee alisema "kwanini wamarekani watumie majeshi mengi na silaha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kwenda kupigana huko Afghanistan? Si wangempeleka Rambo tu, au hata Komando John?" Yule mzee alukuwa anaongea kitu anachokiamini na si kuwa alikuwa anaburudisha.
Ninaposoma hayo maneno kwenye green nahisi yule mzee alikuwa ni wewe.
Unajiita kuwa wewe ni JWTZ halafu unakuja hapa ku-comment mambo ya ajabu ajabu......ulitakiwa kuwa kimya na kusubiri amri tu...Sababu hata hoja ya kwenda vitani hatuna, nyaraka zipo wazi kuwa Ziwa si la kwetu....ni kupitia mezani ndipo tunaweza tukapata ushindi wa hoja na kutwaa sehemu ya Ziwa kinyume na hapo tunaweza kushinda vita sasa lakini documents tukashindwa kuzibadilisha, suala likaoenekana kupo then miaka kadhaa baadaye mgogoro ukaibuka tena.

Hivi unaua kuwa askari huwa haajiriwi ili kutumia akili bali kutenda (and sometimes to follow orders).
The JWTZ I knowna ambapo nimekulia hawezi kuandika uliyoyaandika.
 
Last edited by a moderator:
ndugu hatuta fika popote kama nakuuliza hili unajibu lile,ndio unazihirisha wewe ni mpuuzi,hujui na hujui kama hujui,fahamu kwanza kama ufahamu upate kufahamishwa ili ujue usilolijua.byebye
Natumaini umenielewa. Unaweza kuendelea vizuri na "UanaJeshi" wako kama utajikita zaidi kwenye ULINZI wa TAIFA letu badala ya kutanguliza VITA. Vita inapoanza wanakufa RAIA wengi kuliko wanajeshi.
 
Mkuu, Kawawa na Chief Mhaiki walishawahi kukubali kuwa ziwa lote si letu. Hizi zilikuwa kauli zao za Bungeni miaka ya sitini. Kuna mtu alifanya research juu ya mgogoro huo miaka ya nyuma sana na iliwekwa hapa JF in Pdf formatt.

With all Due respects your highness Superman would you please rephrase the words highlighted in red?
Una maanisha si ziwa lote? au hatuna sehemu katika ziwa tunayomiliki?
 
Last edited by a moderator:
Makanyaga leo nimemshanga sana MM, huyu jamaa sikujui kuwa ni mpuuzi kiasi hiki,Namwambia tena kupitia kwako,Sisi(wapigangaji) hatuangalii matakataka ndani ya serikali kipindi hiki,tunachoangalia ni adui tu,Tutawapiga malawi kwa muda wa dk 30 na hapo ndipo mtakapo tuheshimu

Mkuu vita haipiganwi kwa maneno bali ni vifaa na mbinu
Sasa mtawapiga kwa muda wa dakika 30 kwa kutumia zile helicopter zinazoanguka zenyewe alizoleta Sailesh Vathlani
Acha hizo watu tunazungumzia mustakbali wa taifa na sio ushabiki
mpaka sasa wamalawi wa meshachukua ziwa lote na exploration inaendelea kama kawaida
Isitoshe wana support ya USA nas UK labda nyie mupate support ya Iran kama mlivyowasaidia kuregister meli zao
 
Mzee Mwanakijiji huwa nakueshimu sana lakini leo umeongea pumba.Taaluma yako ya uandishi wa makala huishie huko huko.Wala hujui lolote juu ya Jeshi na hasa JWTZ,wala hujui hasa chanzo kilichokuwepo cha vita kati ya TZ na UGANDA,sanasana utaeleza ni mipaka lakini chanzo hadi kuwa mipaka ilikua nini hujui unaishia kubwabwaja.Labda ni kwambie jambo la msingi,kama mnatuchokoza mkazania hatutaweza kufanya lolote eti hatuna hela,tayari mmefeli vita,kwa taalifa tutawapiga ndani ya dk 30,naongea kama mmoja wa JWTZ,we kaongelee kwenxe magazeti mi ntaongea kwa vitendo,subiri utaniambia

Kwani nyie JWTZ mnajua shida nyie? kwenu nyie maisha ndio bora, ndo maana hutakaa usikie JWTZ inalilia mshaha mdogo kama polisi.
 
Back
Top Bottom