Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 9, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mara zote wakiulizwa kuhusu mambo mbalimbali wanasema 'hawana fedha' na kuwa serikali ni maskini. Tumeona migomo ya madaktari, walimu na tishio la migomo ya wafanyakazi. Tumeona jinsi ambavyo wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa "serikali haina fedha" -sikiliza kwa makini majibu ya mawaziri Bungeni wanavyorudia suala hili. Wanasema "serikali ikiwa na uwezo" au "tunaendelea kutafua fedha kwa ajili ya mradi huo; tena za ndani na za 'washirika wa maendeleo'".

  Kila ukiwauliza mengi ambayo hayaendi vizuri jibu lao ni "serikali yetu haina fedha" au "hali ngumu". Sasa leo hii serikali hii hii ambayo "haina uwezo" inadai ati iko tayari kwenda vitani. Wale ambao tulikuwepo wakati wa vita vya Uganda tunakumbuka gharama kubwa (great toll) ya vita ile kwa maisha ya wananchi hadi vijijini. Hakuna ambaye kwa namna yake hakusikia maumivu (pinch) ya vita. Na vita ilipokwisha gharama yake kwenye uchumi wetu na maendeleo ya watu wetu haikuweza kurudishwa kwa urahisi. Kwa karibu miaka minne (miwili ya vita na ile ya reconstruction) ilisababisha nchi yetu kurudi nyuma zaidi ya ilipokuwepo. Ni kweli tulishinda vita lakini kwa gharama kubwa sana siyo tu ya fedha bali pia ya watu.

  Kwa wanaokumbuka historia ya Uganda mojawapo ya matukio ya vita ni vita ya kuichukua Lukuya (Battle of Lukuya) ni hapa kiasi cha wanajeshi wetu kiliposhtukizwa na wanajeshi mamluki wa Libya na kujikuta kinarudishwa nyuma kabla ya Brigedi ya 201 na 208 kujipanga upya na kuwashambulia mamluki hao na kuwashinda na kusafisha njia ya kwenda Kampala (baada ya kuchukua Entebbe na Jinja). Gharama ya fedha tu serikali ya Museveni ndio iliweza kuilipa Tanzania mwaka 2007! Ikumbukwe kuwa vita ya Uganda inakadiriwa kuigharimu Tanzania dola milioni 1 kwa siku na hizo zilitoka mifukoni mwetu (hatukuwa na wajomba). Leo hii tumepiga kelele kulipa dola laki moja kwa Symbion kwa siku. Fikiria Wamarekani kwenye vita ya Iraq walikuwa wanaunguza dola bilioni 1 kwa siku!

  Nikiangalia hali hiyo najiuliza; hivi kweli kina Lowassa na wengine wanaoshabikia vita wanafikiria kweli gharama yake? Hivi kuna mtu amewahi kuuliza Tanzania ilipoteza askari wangapi vita ya Uganda? Hivi watu wanajua kuwa ili jeshi letu liende vitani ni lazima wale wote waliokuwa reserve nao wawe reactivated? Yaani kabla ya kwenda Vitani itabidi kwanza tuongeze askari wote kutoka kama 30,000 waliopo sasa hivi na kufikia angalau 150,000 hivi kuweza kushinda vita. Hawa tutakaowachukua wengi ndio wasomi wenyewe na wafanyakazi maofisini watabadilishwa na nani? Ikumbukwe kwenye vita ya Uganda hawakwenda JWTZ tu bali Mgambo, Polisi, Magereza na wale waliopewa mafunzo ya haraka haraka. Je tuko tayari kuleta "draft" ya kulazimisha wanaume wote wenye miaka 18 na zaidi kuingia kambini? au watu wanafikiria ni "JWTZ" ndio litaenda vitani wakati wengine tunacheza ping pong na kuchat kwenye JF juu ya maendeleo ya vita?

  Ninachopinga kabisa na ninaona ni mambo ya hatari ni kuzungumzia masuala ya vita bila kuonesha fikara na hekima. Kabla haujaamua kwenda vitani jipe nguvu kwanza. Na hakuna nguvu kubwa zaidi kama nguvu ya kiuchumi. Lakini jambo jingine ambalo labda wengine wameshafikiria ni vikosi vyetu vitakula nini? Au watu wanafikiria wanajeshi wakienda vitani wanapewa zile ration tu? Pamoja na gharama nyingine zote je bado tutaweza kulilisha taifa letu wakati wa vita? Wapo ambao hawajui kuwa njaa ya mwanzoni mwa miaka ya 1980 sehemu kubwa pia ni matokeo ya vita ya Uganda? Je tuko tayari kula dona na yanga tena na kurudishwa kwenye ration kwa taifa zima na mambo yale ya duka la kaya? au watu wanafikiria wataendelea kula nyama choma jioni wakati vita inaendelea?

  Tusianze kupiga ngoma za vita (we shouldn't beat the drums of war) kama hatuko tayari kuingia vitani. Ni uzembe na reckless na binafsi naamini viongozi wote watatu (Lowassa, Membe na Sitta) wanatia shaka kama wana hekima na busara ya kuwa viongozi wa taifa letu. Kiongozi hata mwenye uwezo kiasi gani ni lazima asite linapokuja suala la vita na siyo kusita kwa sababu ya woga lakini kusita kwa sababu ya kujua analiita taifa lake kufanya nini. Na anapozungumza vita awe na uhakika kabisa (absolute confidence) kuwa hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuepuka vita hiyo.

  Kwa mara nyingine nawasihi watu wanaoshabikia vita kama njia ya "kulinda mipaka yetu" wafikirie kwa hekima kuwa zipo njia nyingine nyingi zaidi za kufanya hivyo ikiwemo mazungumzo na mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa. NI LAZIMA TUMALIZE NJIA ZOTE ZA AMANI (siyo mazungumzo tu) kabla hatujasema "we have had enough, we are preparing for war) na binafsi naamini kama tutaonesha hekima ya kutumia njia zote na busara ya kuepuka vita siku ikiitwa vita kweli kabisa tunaweza kwenda siyo kujihami tu bali kuiona Malawi kama tishio na kuanzisha an offensive assault ili kuliondoa tishio hilo mara moja na daima.

  Nashauri vichwa vilivyotulia vizungumza lugha ya amani sasa hivi na kutuliza hizi ngoma za vita na mbiu za mapigano. Maana kama sasa hivi tu wanahangaika kulipa mishahara na kulisha taifa letu, sijui itakuwaje WAKATI WA VITA!


  MMM
   
 2. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nani kasema Serikali haina pesa?

  Za kulipa mishahara walimu na madaktari ndio hakuna....
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Vita would make sense if all diplomatic efforts to resolve the problems fail. Tukienda kama njia ya kupiga kampeni za 2015 itakula kwetu.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Umeongea ukweli mtupu MM
   
 5. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Serikali makini inatafuta njia za kumaliza tatizo kabla ya kuingia vitani,serikali isiyokuwa na uwezo wa kulipa madaktari na walimu inataka kuingia vitani kabla ya kupata suluhu.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hakuna vita za kuzuka zuka tu karne hii,kumbuka UK wana interest zao kule na ndege na RIG zilizopo kule ni za UK.huwezi kupiga kule maana wakubwa wamekaa pale wanataka gesi na labda mafuta!pia sisi lazima twende tukapitishe bakuli usa au uk,watatupa masharti magumu sana na kuona tuna rasilimali kibao sana na tumeshindwa kuzitumia sababu(ufisadi) na mikataba mibovu kabisa kuwahi kutokea,watatubana hapo na kuacha UN waje waamue wakati wale wakiendelea na utafiti!!hakuna vita hata siku moja miaka hii!!
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nadhani hukuwasikia vizuri viongozi we2. Wamesema kama itabidi kufika huko itabidi kuingia vitani. Sasa jiulize kama hizo njia zingine zimeshindikana unatemegea tukae kimya? Kuwa Mzalendo wewe.
   
 8. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu MMM definetly uko sahihi,kwa uchumi wa sasa wa Tz wa kila kiongozi anawaza kujichotea kila
  anachoona kiko karibu yake,na kupiga kelele kuwa serikali haina pesa kwa kila jambo la muhimu, je
  tunawezaje kuingiza nchi vitani ktk mazingira ya ufisadi uliokithiri?kitakachotokea hata pesa itakayotengwa
  kwa ajili ya hiyo vita itachakachuliwa.Ilivyo ni kwamba Joyce Banda amesoma UDHAIFU wa serikali yetu na
  uongozi uliopo sasa.Ili kuiponya nchi yetu tusithubutu kuingia vitani tuwaachie Malawi ziwa lao.
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  MMM serikali yetu ni sikivu sana na kwamba epembuzi yakinifu umeshafanyika ukiwahusisha wataalamu wetu wa wizara zote, hivyo tunapenda kuwatoa wasiwasi wananchi na kuwahakikishia wanachi wetu wawe na amani chini ya serikali ya Mheshimiwa Dr*3, Alhaji JK.

  Mheshimiwa Dr atakua na ziara hivi karibuni amewasafiri kwenda kuomba msaada na hivyo vita hivi vitakua historia!!! Maana wafadhili wameapa kutusaidia kwa nguvu zao zote, ila sijui usalama wa mafuta na gesi yetu pamoja madini
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hawakutakiwa kuzungumzia masuala ya vita at all. Siyo katika hatua hii hata kikao cha kwanza cha "njia nyingine" hakijafanyika! Si wamepanga kukutana Augusti 20? so haraka yao ya nini?
   
 11. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Uzalendo wa kutetea ziwa ili kuua watanzania kwa njaa baada ya vita? maliasili ngapi tunazo kwenye hii
  nchi na haziwasaidii watanzania?isipokuwa mafisadi wachache? THINK TWICE!!!!!!!
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Watanzania kweli ni wagumu kuelewa. Membe na LOWASA wamesema ikibidi tutatingia vitani, hapo nini hakijaeleweka? acheni kupotosha kauli za viongozi.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijagusa sauala la "ziwa lao". Tusubiri mazungumzo yaamue kwani Tanzania haijawahi hata mara moja kukubali kuwa Ziwa Nyassa lote ni la Malawi.
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Serikali inapiga mkwara tu lakini uwezo wa vita hakuna.

  Hadi leo bado tunaugulia maumivu ya vita ya Kagera.
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ni sawa kabisa. Lakini kama upo nyumbani kwako halafu mtu anatoka huko na kudai hapo nyumbani kwako ni kwake na anaingia ndani akitaka umpishe ili aendelee kutumia nyumba yake - je wewe unayeamini upo nyumbani kwako unatakiwa kufanya nini?
   
 16. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Si Malawi wala Tanzania ambayo ipo tayari kwa vita. maneno ya 'vita' 'vita' ni kawaida kutolewa pale ambapo nchi mbili au zaidi zinapotofautiana. USA na USSR walitupiana maneno sana kwa miaka mingi (cold war) lakini hawajawahi kuanzisha vita tunayoisema hapa.
  Nadhani waziri wa mambo ya nje alisomeka vizuri tu. labda kama tuna yetu vichwani mwetu.
   
 17. m

  manucho JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MMM umelonga mzazi ila haya magoigoi(viongozi anzia top) hata uyaambie nini mwingine utamsikia 'Liwalo na Liwe' mwingine utamsikia 'Tuko tayari kuingia vitani' mwingine 'hatuna uwezo wa kuwalipa madaktari' baadae unasikia 'mishahara ya wabunge imepanda mpaka 11m kwa mwezi' n.k.
  Hawa magoigoi ni kwamba kila mtu na lwake they're not on the same page ndiyo maana kila mtu anachumia tumboni kwake mpaka anajisahau kama yuko kazini akikurupuka arudi kazini ndiyo unaanza kusikia kila mtu anapayuka kivyake.

  Hela wanayo ila ni ya kujilipa na kuiba kwa wao wachache as individual siyo kwa faida ya nchi.

  Kagame hapo Rwanda anakwenda kuiba Congo kwa faida ya nchi haya manyang'au yanakwiba ndani ya nchi yanapelek nje ya nchi.

  Hata uyaambie nini hayakuelewi coz tayari yameshachanganyikiwa laana inawatafuna
   
 18. m

  manucho JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
   
 19. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kwanza nimekugongea like kwani nahisi umeniibia maswali yangu, ila sio mbaya kwani ujumbe umefika, pili nijuavyo Mimi hazina kuu imebakia na coins tuu na noti za jerojero wanaposema tuingie vitani sijui wanalitakia nini taifa hili, Wenzetu Malawi wako vizuri kiuchumi na wana support ya Uk majirani zetu Kenya wanaweza kutumia mwanya huo kudai Kilimanjaro waganda nao kudai bukoba tutatokea mlango gani hapo? Maana hata milango ya emergency Inatia mashaka ila sababu kiranja mkuu ni matonya labda atatusaidia ila inaweza ikawa ni Aibu ya karne kuchapwa na mwanamke. Mzee mwanakijiji nachukulia taadhari yako Kama changamoto kwani ubabe kwa kutegemea kuzungusha bakuli na utegemee kushinda vita ni adithi isiyo sikilizika wakianza Mimi nakuwa mkimbizi mapema kabla hayajanikita ya gadafi
   
 20. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Historia inaonyesha kwamba watawala wengi wanaposhindwa kuongoza kwa weledi na kuzidiwa na makelele pamoja na malalamiko ya wananchi huwa wanatafuta njia ya kutuliza lawama za failure, na hasa inapotokea scapegoat issue kama hili la mpaka basi wanajua wananchi wengi wasiojua repercussion watajikoki nyuma yao, mfano mzuri ni Argentina ilipoamua kwenda vitani dhidi ya UK mwaka 1982 kugombania visiwa Falklands. Sioni tofauti kati ya utawala wa Argentina ya kipindi hicho kwa kuangalia matatizo yanayowakumba raia na uwezo wa serikali kutatua matatizo hayo kwa hapa kwetu.
  Huoni sasa hivi hata humu ndani wale wote wapinzani wa chama cha kijani wanapiga matarumbeta ya vita?!!!
   
Loading...