Majibu yenu haya nitayatoa kwenye gazeti next week....
Mwanakijiji, naikataa CCM kwa sababu moja kubwa... siyo tu imepoteza dira, haina sifa wala uhalali wa kuitwa chama cha siasa. Hakikutimiza, hakiendeshwi na hakiheshimu miiko na masharti yaliyoambatana na uanzishwaji na uendeshaji wa mfumo wa vyama vingi. CCM ni serikali, ni bunge na ni mahakama vyote kwa pamoja na hii imepelekea nchi kuendeshwa si kwa kufuata katiba bali miongozo ya CCM.
Kwa maana nyepesi ni kwamba CCM iko juu ya katiba na ndiyo maana wabunge wanaotokana na CCM, wanaweza kuamriwa kutanguliza maslahi ya CCM mbele ya Taifa na wao wakitikia hewala bwana. CCM iko juu ya utawala wa kisheria na ndio maana hadi leo vyombo vya dola vinawagwaya wahalifu wanaovunja sheria mradi tu ama wana uhusiano wa kimaslahi au ni viongozi wa CCM.
CCM imekuwa pasipoti, kimbilio na hifadhi ya mafisadi, wahujumu uchumi, matapeli, wala rushwa na watoa rushwa na kila aina ya adui wa usitawi wa taifa mradi kwa namna fulani wanainufaisha CCM. Viongozi karibu wote wa CCM, tangia kwenye kata hadi taifa wamepatikana kwa njia isiyo halali, hivyo CCM imetokea kuwa kama taasisi ya kulindana kwa watu wenye tabia zinazoshabihiana.
Kwa tabia hii CCM imeweza kuwa kivutio kwa watu wenye malengo sawa wanaotanguliza utii wa kinafiki katika kutetea na kulinda maslahi yao kwa njia yoyote ile. Salama ya kikundi hiki ni umoja wao katika kuhakikisha kinang'ang'ania madarakani kwani bila dola hakiawezi kudumu hata kwa masaa ishirini na nne, sawa na siku moja. Ukweli ni kuwa si rahisi kwa mabadiliko yoyote kutokea ndani ya kikundi hiki.
Mwanakijiji, naichukia CCM na sina matumaini yoyote yale kuwa hili zimwi linaweza siku moja kubadilika, hapana hiyo ni ndoto kama ya Alnacha. CCM ni saratani inayolimaliza taifa na mpaka siku itakapotokomezwa, nchi haiwezi kusitawi wala kuwa salama...ni swala la muda tu. CCM ni gari lililozeeka na halihitaji tena matengenezo yoyote ile, ni kuvunjwa vunjwa labda kwa njia hiyo tutaambulia "scrap metal".