Swali la Ugomvi: CCM ni kama nini?

Swali la Ugomvi: CCM ni kama nini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,097
Reaction score
43,309
woodroffe_hood1.jpg

Chama cha Mapinduzi unaweza kukifananisha na vitu vingi sana; kwa uzuri na kwa ubaya. Kwa uzuri nitawaachia wengine waseme lakini miaka kadhaa nyuma niliwahi kuifananisha CCM na Buibui mwenye kutandaza utando wake kila mahali kiasi kwamba kila kiingiacho kwenye utandao huo kinanaswa kweli kweli na Buibui anaweza kuhisi mahali popote utando huo unapoguswa. Wakati mwingine buibui hali wadudu wote walioko kwenye utando wengine anawaweka kwa akiba na wengine anawatumia kuwa chambo kwa wengine. Ndivyo nilivyoiona CCM wakati huo.

Jana hata hivyo nimekuwa na wazo la kuifananisha CCM na kitu kingine kabisa. Ninaifananisha na yule mbwa mwitu wa kwenye simulizi za kale aliyejiingiza kwenye nyumba bibi kizee kumtafuna na kujifanya yeye ndiye bibi kizee yule akivaa miwani yake mikubwa (bado nakumbuka picha za kile kitabu! (Little Red Riding Hood). Mtoto yule alishangaa kuona bibi yake yuko tofauti mno na alivyomzoea akabakia kuuliza:

"Bibi mbona macho yako makubwa hivyo"
"Nipate kukuona vizuri mjukuu wangu" alijibu mbwamwitu yule!

Sijui wewe mwenzangu unaifananisha na nini CCM katika mawazo yako. Kwa uzuri au kwa ubaya!
 
ccm ni kama mzazi wako aliyekuzaa,akakulea mpaka utu uzima wako,chunga mdomo wako utapigwa laana.
 
Ayaaaa umenikumbusha kwi kwi kwi! mbona watu wamekuja na mifano mibaya tu? I hope watu wa CCM watatupa mifano mizuri...

mwanakijiji mtu uliyefukuzwa nchini kwa uchochezi bado unaitamani tanzania?

wewe tumikishwa tu na wazungu wako huko.
 
HISTORIA YA CCM TANGU
TANU NA ASP

Imetolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu za Taifa, Mikoa na Wilaya. Inapatikana pia katika kitabu cha Sera za Msingi za CCM
Makao Makuu ya CCM
Dodoma, 2004
HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP
1.0 UTANGULIZI:
    1. Maelezo ya awali
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).
Tendo hilo la kihistoria lilikuwa ni la kuendeleza utamaduni uliokuwa umeanza huko nyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la kujiimarisha katika mapambano. Kwa mfano, ASP kwa upande wa Zanzibar ilitokana na kuungana kwa African Association (AA) na Shirazi Association (SA), tendo ambalo liliunganisha nguvu za wanyonge katika mapambano ya kuundoa usultani na utawala wa kikoloni wa Kiingereza. Kwa upande wa Tanzania Bara, TANU ilitokana na kujibadilisha kwa Tanganyika African Association (TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa.
Kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961 na ule wa Zanzibar kupitia Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, kulifanya TANU na ASP viwe vimekamilisha jukumu la ukombozi wa nchi hizi kutoka makucha ya ukoloni mkongwe na usultani. Hata hivyo, vyama vya siasa hivi viliendelea kukabiliwa na majukumu ya kuendeleza mapambano ya ukombozi katika Afrika na kote duniani; kujenga Tanganyika na Zanzibar huru kiuchumi na kijamii na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa,
Katika mazingira ya ubeberu duniani wakati huo na hali ya unyonge wa mataifa haya machanga, yakielewa kuwa ‘umoja ni nguvu', Tanganyika na Zanzibar zilibaini umuhimu wa muungano, hivyo ziliamua kuungana tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huo ndio uliowezesha kuzaliwa kwa Tanzania. Chini ya Muungano huo, Tanzania iliendelea kuwa na vyama vya siasa viwili, yaani TANU na ASP katika mazingira ya chama kimoja cha siasa. Vyama hivi vilitambua fika kwamba vinahitaji chombo madhubuti cha uongozi katika kutekeleza majukumu yake ya ukombozi kwa ukamilifu hivyo uamuzi ulifanywa rasmi wa kuvunja TANU na ASP na kuundwa kwa Chama Cha Mapinduzi tarehe 5 Februari, 1977.
Katiba ya CCM, katika Azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa wa Pamoja wa TANU na ASP tarehe 21 January, 1977, inaeleza kuwa, (uk. 2-3), "...kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African Union(TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari, 1977 na wakati huohuo kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa Katiba."
Muungano wa TANU na ASP ndio uliowezesha CCM kuwa Chama chenye nguvu, imara na madhubuti, hivyo kuwa Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya juu wa kuwaunganisha Watanzania. Aidha, CCM kimeweza kuwaongoza wananchi katika mapambano ya kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.CCM kimeendelea kupewa dhamana na wananchi ya kuunda serikali na kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wa demokrasia ya chama kimoja hadi sasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania Juni 1992.
 
bila ccm taifa hili halipo ccm ni sawa na nyumba takatifu inayohifadhi watu wake.
 
1.2 Umuhimu wa kuielewa historia ya CCM na Vyama vilivyokitangulia
Historia ya CCM tangu TANU na ASP ina umuhimu wa pekee katika Taifa letu katika kuelewa tulikotoka, tulipo hivi sasa na tunakoelekea. Historia ya nchi yetu haiwezi kukamilika bila ya historia ya vyama hivi vya ukombozi. Historia hutoa mafunzo na ni mwelekezaji pia, kwa hiyo ni wajibu wa Watanzania, hasa wanachama wa CCM kujifunza kutokana na historia yetu. Kazi kubwa na ya msingi inayofanyika katika kujifunza historia hiyo, ni kurithisha dhamira ya kujituma na kudumisha uhuru wa nchi yetu. Hivyo, ili kuendelea kukijenga Chama, na kuimarisha uwezo wa kuendelea kukamata dola barabara kwa namna endelevu, hapana budi ihakikishwe kuwa historia ya CCM inabeba pia jukumu la msingi la kusaidia:-

  • Kujua Chama kilikotoka, mahali kilipo na kinakoelekea katika misingi ya sera, itikadi, malengo na wanachama.
  • Kuunganisha wanachama na kuwaweka pamoja kiimani, kiitikadi na kiutendaji.
  • Wanachama kujitambua, kutambua wajibu na majukumu yao na kujenga moyo wa kujiamini na kujithamini.
  • Kuinua kiwango cha ushiriki wa wanachama wa CCM na wananchi katika kubuni na kutekeleza mkakati na mbinu sahihi za kutetea na kuendeleza Chama na taifa kufuatana na hali ya wakati na mahali.
  • Kuweka misingi ya kufanya tathmini na hivyo kuwa na uhakika katika kufanya maamuzi.
  • Kupanda mbegu bora za upendo, uzalendo na uchungu wa kweli kwa uhai wa CCM na taifa kwa ujumla.

  • Kuwa na majibu sahihi wakati wote kwa hoja mbalimbali zinazotolewa kuhusu Chama Cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla.
  • Kuweka msingi wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine maadili ya msingi wa uhai wa CCM.
  • Kuhifadhi kuweka na kueneza kumbukumbu sahihi ya historia ya Chama, nchi, mchango wa Waasisi na wanachama na kuhakikisha wapotoshaji hawapati fursa ya kueneza uongo.
 
[h=4]1.3 Chimbuko la Historia ya CCM[/h] Pamoja na kwamba Chama Cha Mapinduzi kuwa kilizaliwa rasmi tarehe 5 Februari, 1977, chimbuko lake linaanzia miaka mingi kabla, sambamba na historia ya uhai wa taifa la Tanzania. Mizizi ya historia ya CCM imo ndani ya harakati za kukataa ukoloni na usultani, zilizofanywa na wananchi wa Tanzania. Wahenga wetu kwa pamoja tangu enzi, walionyesha wazi kukataa kwao kutawaliwa. Historia ya Tanzania inao utajiri wa mifano mingi ya harakati hizo japokuwa zilijengwa katika misingi ya ukoo na ujirani, katika wilaya na mikoa mbalimbali hata kabla ya kuundwa kwa vyama vya TANU na ASP.
Wananchi hao waliotutangulia walikataa kunyonywa, kupuuzwa, kubaguliwa, kutawaliwa, kunyanyaswa na kugawanywa katika misingi ya rangi, kabila, dini, jinsia, nk. Utu na uhuru wao ulikuwa na thamani kubwa sana. Hivyo waliamua kupambana dhidi ya udhalimu huo. Baadhi ya mifano ya jitihada za mapambano ya awali ni Vita ya Majimaji huko Umatumbi na maeneo ya kusini, Mbiru huko Upare, Waluguru, Wameru, Wahehe na mengineyo huko Unguja, Pemba, Kanda ya Ziwa na katika jamii za wafugaji. Ari, utashi, uzalendo na dhamira ya kweli ya kutaka kujitawala vilivyojidhihirisha katika harakati hizo, viliotesha mizizi iliyoshikilia uhai wa vyama vya TANU na ASP.
 
0 CHAMA CHA MAPINDUZI
    1. Kuzaliwa kwa CCM
Katika Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba, 1975 Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama kimoja;
"Lakini kwa sababu kuna vyama viwili TANU na ASP, Katiba inazungumza juu ya Chama kimoja, hicho Chama kimoja kwa kweli ni vyama viwili … Siasa ya TANU na ASP ni moja yaani Ujamaa na Kujitegemea. Midhali Katiba ya Tanzania ni ya Chama kimoja, Katiba hiyo inataka hicho Chama chenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kishike hatamu na uongozi wa nchi". (Tathmini ya Miaka 20 ya CCM, uk. 3-4).
Kwa msisitizo huo, Mwalimu alipendekeza kuunganishwa kwa TANU na ASP na kuundwa kwa chama kipya. Pendekezo hilo liliwasilishwa kwa wanachama wa TANU na ASP ili kujadili na kutoa maoni yao. Matokeo ya maoni ya wanachama ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya wanachama walikubaliana na pendekezo la Mwalimu Nyerere. Baada ya kupokea matokeo ya maoni ya wanachama wao, Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU na ile ya ASP, zilikutana na kufanya kikao cha pamoja Oktoba, 1976. Katika mkutano huo iliteuliwa Tume ya Watu 20 iliyopewa jukumu la kutayarisha Katiba ya Chama kipya. Mwenyekiti wa Tume hiyo alikuwa Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake alikuwa Ndugu Pius Msekwa.
Wajumbe wa Tume ya Watu 20 ya kuandaa Katiba ya CCM:-
Kutoka ASP: Kutoka TANU:
1. Sheikh Thabiti Kombo 1. Ndugu Peter A. Kisumo
2. Ndugu Ali Mzee 2. Ndugu Pius Msekwa
3. Ndugu A.S. Natepe 3. Ndugu Daudi N. Mwakawago
4. Ndugu Seif Bakari 4. Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru
5. Ndugu Hamisi Hemed 5. Ndugu Jackson Kaaya
6. Ndugu Rajab Kheri 6. Ndugu Peter S.Siyovelwa
7. Ndugu Asia Amour 7. Ndugu Nicodemus M. Banduka
8. Ndugu Hassan N. Moyo 8. Ndugu Lawi N. Sijaona
9. Ndugu Juma Salum 9. Ndugu Beatrice P. Mhango
10. Ndugu Hamdan Muhiddin 10. Ndugu Basheikh A. Mikidadi
Mkutano Mkuu wa Pamoja wa vyama vya ASP na TANU uliofanyika tarehe 21 Januari, 1977 uliazimia ifuatavyo:-
"Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja wa TANU na ASP tuliokutana leo tarehe 21 Januati, 1977 mjini Dar es Salaam, chini ya uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Rais wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe, Rais wa ASP, kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari , 1977 na wakati huo huo kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa Katiba" (Katiba ya CCM).
Aidha, Azimio hilo lilisisitiza kwamba:
"Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini …" (Katiba ya CCM)
Mkutano Mkuu huo wa pamoja ulipitisha pia Katiba ya CCM na kumchagua Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyekiti wa CCM, Sheikh Aboud Jumbe kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Ndugu Pius Msekwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM.
Azma ya CCM ilikuwa ni kuendeleza mazuri yote ya TANU na ASP na kuyaacha mabaya. Miongoni mwa mazuri yaliyoendelezwa na CCM ni pamoja na:-

  • Kuendelea kuimarisha uhuru wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
  • Kuendelea kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
  • Kuendelea kupanua na kuimarisha demokrasia ndani ya Chama na nchini ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya demokrasia Zanzibar. Katiba ya CCM iliwataka wanachama wake Zanzibar kuwa na viongozi wengi wa kuchaguliwa badala ya uteuzi kama ilivyokuwa chini ya ASP. Kwa kupitia Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, wananchi wa Zanzibar walipata fursa ya kwanza ya kuwachagua Wabunge wao. Aidha, kwa kupitia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1979, Baraza la Wawakilishi liliundwa mwaka 1980 na Wawakilishi kupatikana kwa njia ya kura ya siri.

    1. CCM katika kipindi cha Mageuzi:
CCM kama ilivyokuwa kwa TANU na ASP, kimeendelea kuongoza nchi yetu hata chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa rasmi tarehe 1 Julai, 1992. Changamoto inayoikabili CCM ni kuendelea kuwa chombo cha uongozi katika mazingira haya ya mfumo wa vyama vingi vya siasa na mazingira ya utandawazi bila ya kuwepo Baba wa Taifa.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999 Jijini London katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas. Kifo cha Baba wa Taifa kilikuwa ni pigo kubwa kwa CCM na Taifa letu. Kwa Watanzania, Mwalimu ni maarufu kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa Taifa letu, ni mwanzilishi wa TANU hadi kuleta uhuru; Mwalimu na Mzee Abeid Amani Karume ndio walioasisi Muungano; Mwalimu na Mzee Aboud Jumbe ndio walioasisi CCM; Mwalimu ndiye aliyelijenga na kutuachia Taifa lenye umoja, udugu na mshikamano. Afrika itamkumbuka kama kiongozi shupavu na aliyejitolea mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Afrika. Dunia itamkumbuka Mwalimu kama mtetezi wa wanyonge wa dunia, hasa wa nchi za Kusini. La msingi katika kumkumbuka ni kuendeleza yote mema aliyotuachia.
Chini ya mfumo wa Vyama vingi vya siasa CCM kimeweza kufanya mageuzi makubwa ya kisiasa kiuchumi na kijamii. Mageuzi ya kiuchumi yanaendelea kwa mafanikio makubwa kupitia Ubinafsishaji na mkakati wa Uwezeshaji chini ya mkakati mkuu wa modenaizesheni. Mageuzi ya kisiasa yameibua kuanzishwa kwa vyama 16 vya siasa vilivyosajiliwa. Hata hivyo CCM kimeweza kujiimarisha kisiasa na kiuhalali kupitia ushindi wa chaguzi kuu za 1995 na 2000. Ilani ya Uchaguzi ya 2000 inaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2003 kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania umefikia asilimia 6.5 licha ya hali ya majanga kama vile ukimwi na ukame yanayotishia mafanikio hayo. Kasi hii ni ya juu katika nchi za SADC kwa kipindi hicho.
Aidha CCM inaendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya chuki na msambaratiko wa umoja wa kitaifa, amani na mshikamano. Katika msimamo huo CCM imeweza kufikia MUAFAKA na CUF, hatua ambayo imetoa fursa kwa Zanzibar kurejesha hali ya amani, utulivu na mashirikiano, hivyo kuweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
 
watu hujitahidi sana kuichafua ccm lakini hawajaweza alianza mtei kaishia kuzeeka ccm kaicha,amekuja slaa naye anazeeka na kuiacha nani kama ccm.
 
Tunajifunza nini kutokana na historia ya TANU na ASP? Historia ya TANU na ASP inaonyesha kwamba Chama chetu wakati wote kimekuwa na sifa zifuatazo:
  • kuimarisha umoja;
  • kujenga utaifa na uzalendo;
  • kupanua demokrasia ndani ya chama;
  • kubadilika mara kwa mara kifikra na kimuundo kulingana na wakati;
  • pamoja na kutambua na kushughulikia matatizo ya wananchi.
CCM kinayo nafasi nzuri ya kujifunza mambo mengi mazuri kutokana na historia ya TANU na ASP. Katika kipindi kinachotukabili inabidi CCM kikabiliane na changamoto mbalimbali kwa kutumia mafunzo si tu yatokanayo na historia ya TANU na ASP, bali pia kwa kuzingatia uzoefu wake hadi sasa. Changamoto ya utandawazi na majukumu ya kisiasa, kiuchumi kiutamaduni na kijamii hayana majibu katika historia peke yake. Mada zinazofuata zinatoa fursa ya kutafakari mustakabali, mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo mbele ya CCM ili kiendelee kushinda na kuendelea kuwa Chama Tawala kinachokidhi matakwa ya Watanzania.
 
Ukiwa mitaani ukimuuliza hata mtoto mdogo ccm ni chama gani atatoa majibu yafuatayo.
1. Chama cha mafisadi
2. Chama cha kuzusha ugaidi
3. Chama kinacho iba kura
4. Chama kilichoshindwa kesi nyingi na Tundu lissu.
 
Mimi huwa naifananisha CCM na jino bovu ambalo linastahili kung'olewa wakati wowote..lakini kabla ya kung'olewa napenda mng'oaji aniambie ataweka nini kama mbadala wa pengo!
 
Kweli Mzee Mwanakijiji amejiishia kama ni mcheza mpira basi ni Akwitende (yule mzee aliyecheza Gossage Cup) hivi sasa CECAFA. "kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchukuzi"


 
Ukiwa mitaani ukimuuliza hata mtoto mdogo ccm ni chama gani atatoa majibu yafuatayo.
1. Chama cha mafisadi
2. Chama cha kuzusha ugaidi
3. Chama kinacho iba kura
4. Chama kilichoshindwa kesi nyingi na Tundu lissu.
Msukule ukinywa viroba ni hatari.

 
CCM ni sawa na 'ukoo wa panya' baba mwizi, mama mwizi, mtoto mwizi, babu mwizi, bibi mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mkwe mwizi! By Mh. Nassari:crying:
 
Ccm inafanana na ukoo wa Panya babu mwizi bibi mwizi mama mwizi baba mwizi mjomba mwizi shangazi mwizi watoto wezi wooote ni wezi
 
Back
Top Bottom