Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
hivi mnakunawaga na akili gani giza likiingia!!!!tupia gari zilizotolewa na Mh Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini maoni yaendelee
ninavyojua mimi na uzoefu wangu ni kuwa wabongo wanazikuta ambulance hospitali,sijawahi kuona ambulance inamfata mtu mtaan au nyumbani,ni kwamba ukizidiwa hospitali ya chini unakimbizwa muhimbili au bugando na ambulance(kama una bahati hiyo).
mengine wataelezea wadau
Uko right.
Nimewahi kumpeleka mgonjwa mmoja hospital na ambulance fulani, ilikuwa ni majanga!
Safari ilianzia Moshi kwenda Arusha. Tulianza saa moja kamili na tulifika saa tano kasoro.
Njiani tuliishiwa mafuta mara mbili na tukalazimika kubadilisha gari, japo kampini ilikuwa ileile.
Nilijuta kwenda na yule muingereza, niliona aibu mpaka basi!
Kampuni jina Kubwa, Makao makuu south Afrika! Huduma ni ghali acha, malipo kwa dola mzee.
Bahati nzuri wazungu insuarance zao ziko vizuri sana. Japo kila wakati tukiwasiliana nilitamaani ardhi ipasuke niingie, all the time insurance wana keep contact na wao ndio wana initiate calls.
Ambulance za Tanzania kazi yake ni kukumtoa mgonjwa hospitali moja kumpeleka hospitali nyingine yenye huduma zaidi.
Sijawahi kuona zikibeba wagonjwa toka majumbani.
Mzee Mwanakijiji
Maswali mazuri sana
Je, wato huduma wanajua matumizi ya gari na vifaa na wanajua kwanini linaitwa gari la Wagonjwa?
Kwa kudokeza tu, gari la wagonjwa lina maana nyingi sana.
Kwanza, huduma ya kwanza ya mgonjwa akiwa eneo kutoka kwa watu wa 'dispatch'
Pili, huduma ya kwanza ya dharura ndani ya gari mgonjwa akielekea hospitali
tatu mawasiliano na kituo gari linapoelekea ili kuwajuza wataalam dharura inayokuja
nne, kuhakikisha hakuna uchelewashi wa safari kwa foleni za barabarani
n.k.
Pili, Je, kuna mahali katika halmashauri mtu anaweza kupiga simua na kupata huduma
Siku za nyuma ilikuwa ndiyo na tuliwahi kutumia baadhi. Huduma hiyo ikafa
Gari la wagonjwa halikai hospitali, linakaa maeneo ambayo likihitajika linapatikana kwa uharaka
Tatizo la gari la wagonjwa ni sehemu tu ya matatizo mengi yasiyoonekana kwasababu yamefunikwa na mambo ya siasa ya kutoa magari bila kujua yanatumikaje na ynasaidia vipi
Kwa mfano, utapiga wapi simu Tanzania kupata huduma ya dhararu kama 'poison control centre'
Matokeo ya hayo mtu akipata 'ajali' ya sumu watu wanashindilia maziwa ambayo kuna baadhi ya sumu ni kama vile unasaidia kuziingiza mwilini.
Ni hoja nzuri inayohitaji mjadala na hao viongozi wafungue macho
Ukipata dharura nyumbani kwako unatakiwa kuita Bajaji au Bodaboda ikuwahishe kwenye a Near by Health Centre (Mungu jalia iwe na Ambulance)Kwa hiyo kama mtu akipata emergency nyumbani kwake, kitu kama anapata stroke au amechomwa kisu mnafanyaje kuwahi hospitali au hili ndilo linaelezea ile tunayosikia mara nyingi "alifia njiani" si kwa sababu ya jeraha lenyewe au janga bali kwa sababu alikosa huduma ya kwanza kwa haraka?
Mkuu hii mada ni muhimu sana kwa Taifa.Nimeuliza hili kwani wiki chache nyuma Rais naye alitoa msaada wa magari ya "wagonjwa" kiasi kwamba inashangaza kama alimaanisha kwa ajili ya kusaidia kuwaokoa watu wanaoopata dharura
au kweli ni la kubeba wagonjwa - toka hospitali moja kwenda nyingine -
na siyo kwa ajili ya kuwahisha watu hospitali.
Yaani ni kinyume kabisa.ninavyojua mimi na uzoefu wangu ni kuwa wabongo wanazikuta ambulance hospitali,sijawahi kuona ambulance inamfata mtu mtaan au nyumbani,ni kwamba ukizidiwa hospitali ya chini unakimbizwa muhimbili au bugando na ambulance(kama una bahati hiyo).
mengine wataelezea wadau
Yaani ni tatizo kubwa kweli.Vipi kuhusu CPR?
Inafundishwa mashuleni siku hizi?
Mimi sikumbuki kabisa kama ilikuwa inafundishwa enzi nikiwa bado mwanafunzi wa msingi na upili.
Na hata hao wato huduma ya dharura wanao huo ujuzi kweli?
hata huko marekani ukiondoa Madaktari wachache wengi hawajui CPR....CPR sio neno tu ni kazi nzito.Vipi kuhusu CPR?
Inafundishwa mashuleni siku hizi?
Mimi sikumbuki kabisa kama ilikuwa inafundishwa enzi nikiwa bado mwanafunzi wa msingi na upili.
Na hata hao wato huduma ya dharura wanao huo ujuzi kweli?