Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,740
- 40,864
(Picha ya kwanza msaada wa gari lililotolewa na Prof. Muhongo jimboni kwake)
(Moja ya magari yaliyotolewa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani kusaidia wagonjwa)
(Gari la wagonjwa, Marekani)
Chini video inayoonesha baadhi ya mambo yaliyomo katika magari ya kisasa ya wagonjwa; ukiondoa kitanda na ving'ora!
Nimejikuta najiuliza swali hili leo baada ya kutafakari mambo kadha wa kadha. Kuna magari ya kuzima moto (fire trucks) na tumeona mara kadhaa viongozi mbalimbali wakitoa zawadi au misaada ya magari ya kusafirisha wagonjwa (ambulance trucks) kwa ajili ya kusaidia huduma hiyo. Lakini mara kadhaa tumeona watu wanapata ajali au mtu anahitaji huduma hiyo lakini mara nyingi anategemea usafiri binafsi kuweza kuwahishwa hospitali. Na nina uhakika wa kutosha kuwa hatuna huduma ya air ambulance (helikopta zinawahi eneo la tukio la ajiri na kuwachukua wajeruhiwa ambao wanahitaji kuwahishwa zaidi hospitali kuliko kwa kutumia barabara).
Je, ni sheria gani inasimamia huduma hii? Je, huduma hii ni ya watu binafsi au ni vizuri kutegemea kampuni binafsi kufanya huduma hii ya kwanza ya dharura (EMS)? Je, wale wanaotoa huduma - kama wale wanaopewa magari ya wagonjwa) wana utaalamu gani au wamepata utaalamu wapi wa kutoa huduma hiyo? Je, ni taasisi gani inasimamia uandikishwaji na usahili wa watu wanaotoa huduma hii?
Chukulia kwa mfano wa kile kinachoitwa "gari la wagonjwa"; je, gari hilo lina vifaa gani vya kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa? Au linaitwa "gari la wagonjwa" kwa sababu lina kitanda tu na ving'ora? Na kama gari hilo linaweza kuwa na vifaa vya kisasa je, wanaolitumia wamepata mafunzo wapi ya kutumia vifaa hivyo?
Lakini swali jingine ni je, halmashauri na miji yetu ni ni mingapi imejaribu hata kuwa na dispatch unit inayoongoza magari ya wagonjwa; kwamba mtu akiita au kupiga simu nani anapokea ujumbe, na gari gani inaamuliwa kwenda wapi na nani? Je, ni kwa jinsi gani magari hayo yanahusiana na hospitali zilizoko karibu? Kuna mawasiliano yoyote?
Maswali yote haya yana umuhimu wake katika kufanikisha huduma ya dharura na uokoaji pale inapohitajika.
Au tumeamua kuendelea kuombea tu watu wasipatwe na majanga na kuwa yakitokea basi wasipate madhara makubwa? Lakini vipi wale ambao wanapata magonjwa ya ghafla wakiwa majumbani kwao, kazini au barabarani; vitu kama shinikizo la moyo au yabisi wanaweza kupatiwa msaada vipi?