Marhaban bial'asdiqa'.
Natumai nyote mu buheri wa afya Jumapili ya leo.
Hivi jamani, eti kwa mama mzazi wa kijana kumwuliza mpenzi wa kike wa huyo kijana wake kuhusu uwezo wake [kijana] wa kitandani ni swali linalofaa kweli?
Mimi naona ni swali ambalo halifai kabisa na linaloingilia faragha ya kijana.
Kwa nini mama mtu atake kujua uwezo wa kugegeda[na] wa kijana wake?
Yeye hayo yanamhusu nini hasa?
Sasa labda mimi sijui...pengine ni kawaida kwa wamama kudadisi mambo kama hayo kuhusu watoto wao wa kiume, hivyo ningependa kusikia mitazamo ya wengine ikoje.
Manake yawezekana mimi nikawa naona haifai kabisa ilhali ni jambo la kawaida hususan kwa wamama.
Nakaribisha maoni yenu.