Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Amani iwe kwenu.
Ikumbukwe tu Chadema iliasisiwa na Mzee Mtei ambaye ni muumini wa siasa za kibepari na ndiokisa kilichomfanya kuondoka kwenye serikali ya Mwl.Nyerere.
Mabadiliko tunayoyaona sasa hasa ya kukaribisha wanasiasa ambao misimamo yao kisiasa bado ni ya kisoshalist,haikanganyi au sera zilishabadilika?
Wabunge na mgombea uraisi walinadi sera ya elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu bure,na sio mkopo.Ikumbukwe haya ni mambo ambayo Mtei alipinga akiwa waziri wa fedha...alikataa kugharamia huduma za jamii bure hali iliyopelekea kujiuzulu.Hata hivi karibuni alinukuliwa akimuonya raisi Dr.Magufuli kuwa "anafanya kazi vizuri ila asiige siasa za Nyerere"...Je Chadema inapingana na maono ya Mwasisi?
Je, Lowasa na Kingunge wangefuata sera za majimbo?.. Je, wangekubali serikali tatu ambazo walipinga?
Ninamaliza kwa kuuliza ni lini chadema walizitupa siasa za kibepari?...au Je Kingunge anaamini katika ubepari?
Nawasilisha kwa majadiliano.