Swali la Kizushi juu ya Makampuni anzishwa

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,646
Reaction score
9,622
habari zenu ndugu...nimeona si vyema kukaa na upofu wangu wa kutokujua mambo jinsi yanvyokwenda..swali langu lipo hivi...wale waanzilishi wa makampuni makubwa duniani kama Cocacola,Mercedes Benz.BMW, Ford n.k ambao wengi wao na marehem,je ndugu za(watoto wajukuu,vitukuu nk) wanafaidika vipi na makampuni haya yaliyoanzishwa na ngugu yao?
 
Bado wao ndo wanamiliki makampuni hayo ingawa kwa sasa ni Public Company kwamba yako kwenye masoko ya hisa,

TOYOTA bado inamilikiwa na watoto kama sio wajukuu wa mwanzilishi, Ford hivyo hivyo, kwa kifupi familia zao bado ndo zinamiliki na zinakula matunda, hawa jamaa waliona mbali sana, naweza kusema ni moja kati ya wavumbuzi walio iona kesho,

Ni uvumbuzi utakao ishi miaka na miaka, jamaa waliumiza vichwa sana na si biashara zetu za kibongo za ajabu ajabu mara sijui TOYO mara Tigo Pesa,

Na ukisoma historia zao wate walipita katika vipindi vigumu sana, ikiwemo kufilisika kabisa na baadae kufufuka upya, ila leo hii hawako Duniani lakini kazi zao bado zinatamba duniani na watoto wao wanafadi matunda,

Unapo kuwa unaingia katika ujasirimali ni lazima ujiulize Je katika biashara yangu nikifa nayo itakufa au itadumu milele, Ila kwa business zetu kudumu milele ni kitu kisicho wezekana, BIASHARA YA UCHUUZI NDO NYINGI BONGO SASA MMILIKI AKIFA NA BIASHARA NDO MWISHO WAKE NA IKIJITAHIDI SANA ITAKAA MIAKA MIATATU MINNE INAPOTEA

So kwa kifupi hawa jamaa wakina Thomas Edsoni waliiona Kesho wakati walipo kuwa wanavumbua kazi zao
 
shukran mkuu imekuelewa 100& jambo la msingi sana ni ujasiriamali kufanya kitu cha tofauti(creative) chenye thamani(value) kinachohitajika sokoni (marketable)
 
habari zenu ndugu...nimeona si vyema kukaa na upofu wangu wa kutokujua mambo jinsi yanvyokwenda..swali langu lipo hivi...wale waanzilishi wa makampuni makubwa duniani kama cocacola,mercedes benz.bmw,ford n.k ambao wengi wao na marehem,je ndugu za(watoto wajukuu,vitukuu nk) wanafaidika vipi na makampuni haya yaliyoanzishwa na ngugu yao?

Mkuu Kidarari naunga Mkono mchango wa Mkuu Chasha, ameshajibu ulichotaka kujua, na hili siyo swali la kijinga ni swali linalotoa changamoto kubwa kama alichochangia Chasha kwamba tusiangalie leo bali tuangalie miaka mingi ijayo, je wenzetu wanawaandaa vipi warithi wao? Hapa nimebandika uthibitisho wa Satake Corporation wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa mashine za kusindika mazao maarufu kama SATAKE, huu ni ukoo ambao hivi sasa anaeongoza shirika hili ni mwanamke uzao wa nne kutoa muasisi! Hiyo ni Japan. Tabia ya kurithishana biashara imeenea duniani kote mashariki hadi magharibi tatizo ni hilo bara letu la Africa tu ndiyo tujishangae tunatofautiana sana na wenzetu wa dunia nyingine!! Ukifa Baba kila kitu kinakufa tutafakari tujiandae vipi hata kama ni ka-karakana ka karabati baiskeli tu!!
 
Attachments

  • Back from Hiroshima 181.jpg
    Back from Hiroshima 181.jpg
    711.5 KB · Views: 123
  • Back from Hiroshima 182.jpg
    Back from Hiroshima 182.jpg
    607.3 KB · Views: 121
  • Back from Hiroshima 183.jpg
    Back from Hiroshima 183.jpg
    584.3 KB · Views: 119
  • Back from Hiroshima 184.jpg
    Back from Hiroshima 184.jpg
    594.1 KB · Views: 115
  • Back from Hiroshima 185.jpg
    Back from Hiroshima 185.jpg
    600.9 KB · Views: 106
Mkuu Kubota ni kweli kabisa, Tunatatizo kubwa katika Kurithishana na vilevile aina ya biashara tunazo fanya,

Kwa Tanzania ni Wahindi pekee ndo wanaweza kuendesha biashara za familia vizuri, Wahindi kwao Elimu ya Darasani si ishu sana, that is why unakuta watoto wanashinda madukani na kwenye project zingine za Wazazi wao, Shule zikufungwa wakati watoto wa Wabongo ni kila siku wako mtaani mara viwanja, watoto wa kihindi wako bise kujifunza kwa vitendo kutoka kwa wazazi wao,

Na utagundua kwamba watoto wa Wahindi wengi wqanaishia levo ya chini ya elimu kwa sbabau kwao elimu ya darasani si ishu,

Nakumbuka kuna Mzee mmoja ambaye ni mfanya biashara mzuri sana, aliniita nikawape ushauri watoto wake waliomaliza Form six walikuwa wanataka kujoin Chuo, Kwakweli mimi ushauri nilio toa ni kwamba hawa wtoto wasomee kozi zinazo endana na kazi yako na wakimaliza waje kuendeleza biashara yako pale nguvu zitakapo kuishia,

Cha kusikitisha ushauri wangu haukuzingatiwa kabisa na watoto wakaenda kusoma kozi tofauti kabisa,

SO Wakina SONY bado jamii yake inafaidi matunda kwa sbabau kwanza waliandaliwa kunedeleza biashara za baba, so leo hii hawa jamaa wakifufuka wanaweza furahi sana kuona kazi zao zimepiga hatua sana,

Tanzania Baba akifa kinacho fuatia ni watoto kuwanza kugawana mali badala ya kuendeleza kama familiy business na kusukuma mbele wazo la baba yao, unaweza kuta Baba au mama alikuwa na Mabasi kama kumi basi akifa kila mtu anabeba lake wanagawana hati tairi za hayo mabasi,
 
Ni kweli Mkuu inasikitisha, tunapaswa tujifunze sana kwa waliofanikiwa! Tunaishi na wahindi na waarabu lakini hatujifunzi chochote kwenye mifumo ya maisha yao!! Hilo la jinsi ya kupitisha elimu kwa watoto ndiyo moyo wa kila kitu! Kijijini kwetu kuna waarabu, watoto wao tulisoma nao, jioni sisi tulipokuwa tunakimbizana huku na kule watoto wa waarabu wao walikuwa wanauza dukani, mmoja tulisoma nae, darasani alikuwa wa kawaida na alifeli, hivi sasa ni bepari mkubwa sana, alimegewa mtaji na wazazi wake anafanya biashara kubwa sana. Suala siyo mtaji aliopewa bali ni kwa sababu ya elimu ya biashara aliyorithishwa na wazazi wake humo dukani na mazungumzo yao wanapokunywa gahawa!!

Lakini Mkuu Chasha nimewahi kushuhudia kijijini kwetu mzee mmoja alikuwa tajiri sana na alikuwa akiwahusisha sana watoto wake kwenye biashara zake, watoto wake wakaja kuvuruga mali kwa ubishoo na ulevi na mambo ya guest house, hiyo ilitokea Baba yao akiwepo hai na huyo Mzee alikuja kufa masikini, hii nayo ni changamoto!!
 
wakuu nalizani ni swali la kijinga kumbe limenifungua kufikiri upande wa pili mbele zaidi,tuna safari ndefu kuhakikisha invstment za wazazi zinaendelea kukua baada ya wazazi kufariki.
 
Ni kweli, hapa kwetu Africa/TZ mtu mmoja wake 100 mbali na vimada, watoto ni sawa manispaa ya temeke we unategemea nini? Maprofessa wa uchumi ndio hao hawana ukombozi na elimu zao zaidi ya kukariri na kuongea pumba zenye uchonganishi maeneo ya dini. Kazi kwelikweli
 
Ni kweli Mkuu inasikitisha, tunapaswa tujifunze sana kwa waliofanikiwa! Tunaishi na wahindi na waarabu lakini hatujifunzi chochote kwenye mifumo ya maisha yao!! Hilo la jinsi ya kupitisha elimu kwa watoto ndiyo moyo wa kila kitu! Kijijini kwetu kuna waarabu, watoto wao tulisoma nao, jioni sisi tulipokuwa tunakimbizana huku na kule watoto wa waarabu wao walikuwa wanauza dukani, mmoja tulisoma nae, darasani alikuwa wa kawaida na alifeli, hivi sasa ni bepari mkubwa sana, alimegewa mtaji na wazazi wake anafanya biashara kubwa sana. Suala siyo mtaji aliopewa bali ni kwa sababu ya elimu ya biashara aliyorithishwa na wazazi wake humo dukani na mazungumzo yao wanapokunywa gahawa!!

Lakini Mkuu Chasha nimewahi kushuhudia kijijini kwetu mzee mmoja alikuwa tajiri sana na alikuwa akiwahusisha sana watoto wake kwenye biashara zake, watoto wake wakaja kuvuruga mali kwa ubishoo na ulevi na mambo ya guest house, hiyo ilitokea Baba yao akiwepo hai na huyo Mzee alikuja kufa masikini, hii nayo ni changamoto!!

Mi hadi huwa najiuliza hivi hawa wahindi huwa hawafanyi hivyo hapo kwa red? manake ninapoishi nawaonaga watoto wao wako focused kwenye bizness na sijawahi waona wakifanya vitu kama hivyo, labda pengine sina uzoefu nao sana, ila hata hivyo nahisi wana nidhamu ya matumizi ya kipato chao.
 
Ni kweli Mkuu inasikitisha, tunapaswa tujifunze sana kwa waliofanikiwa! Tunaishi na wahindi na waarabu lakini hatujifunzi chochote kwenye mifumo ya maisha yao!! Hilo la jinsi ya kupitisha elimu kwa watoto ndiyo moyo wa kila kitu! Kijijini kwetu kuna waarabu, watoto wao tulisoma nao, jioni sisi tulipokuwa tunakimbizana huku na kule watoto wa waarabu wao walikuwa wanauza dukani, mmoja tulisoma nae, darasani alikuwa wa kawaida na alifeli, hivi sasa ni bepari mkubwa sana, alimegewa mtaji na wazazi wake anafanya biashara kubwa sana. Suala siyo mtaji aliopewa bali ni kwa sababu ya elimu ya biashara aliyorithishwa na wazazi wake humo dukani na mazungumzo yao wanapokunywa gahawa!!

Lakini Mkuu Chasha nimewahi kushuhudia kijijini kwetu mzee mmoja alikuwa tajiri sana na alikuwa akiwahusisha sana watoto wake kwenye biashara zake, watoto wake wakaja kuvuruga mali kwa ubishoo na ulevi na mambo ya guest house, hiyo ilitokea Baba yao akiwepo hai na huyo Mzee alikuja kufa masikini, hii nayo ni changamoto!!

huyu mzee alikuwa na nia njema ya kuidumisha biashara yake na kukua kupitia kwa watoto wake ila inaelekea hakuwajenga kisaikolojia kuizoea hela na kujua hela iliyoko kwenye biashara siyo yao bali wanatakiwa kuisimamia huku wakhnufaika na return ambayo kiasi fulani ndo kitakuwa kwa matumizi yao na kingine kurudi kwenye biashara
 
Mada nimeipenda na imenifundisha kwa kiasi kikubwa sana na hata wachangiaji wake tangia mwanzo wamechangia kwa nia ya kuelimisha na kunifanya nijivunie kuijua jf na kuzidi kuipenda kwa elimu hii ninayoipata kwa kushare idia. Pia niseme tu wazazi wengi wa kibongo wanakuwa na woga wa kuwashirikisha watoto wao ktk biashara wakiogopa either watawaibia au kuacha shule baada ya kuijua hela wakidhani wanawajenga vizuri kumbe ndo anapalilia akifa afe na biashara zake, pia kwa elimu niliyoipata hapa ni kuplan biashara ambayo yenye uwenzo wa kudumu muda mrefu hasa campuni ambayo siyo lazima mmiliki awe shm ya biashara hali ambayo itaweza kuinufaisha fimilia yangu hapo baadae jipo wanaweza wasiwe na uwezo mzuri wa usimamizi
 
huyu mzee alikuwa na nia njema ya kuidumisha biashara yake na kukua kupitia kwa watoto wake ila inaelekea hakuwajenga kisaikolojia kuizoea hela na kujua hela iliyoko kwenye biashara siyo yao bali wanatakiwa kuisimamia huku wakhnufaika na return ambayo kiasi fulani ndo kitakuwa kwa matumizi yao na kingine kurudi kwenye biashara

Mkuu hilo nalo neno nakubaliana na wewe.
 
Mkuu Kidarari naunga Mkono mchango wa Mkuu Chasha, ameshajibu ulichotaka kujua, na hili siyo swali la kijinga ni swali linalotoa changamoto kubwa kama alichochangia Chasha kwamba tusiangalie leo bali tuangalie miaka mingi ijayo, je wenzetu wanawaandaa vipi warithi wao? Hapa nimebandika uthibitisho wa Satake Corporation wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa mashine za kusindika mazao maarufu kama SATAKE, huu ni ukoo ambao hivi sasa anaeongoza shirika hili ni mwanamke uzao wa nne kutoa muasisi! Hiyo ni Japan. Tabia ya kurithishana biashara imeenea duniani kote mashariki hadi magharibi tatizo ni hilo bara letu la Africa tu ndiyo tujishangae tunatofautiana sana na wenzetu wa dunia nyingine!! Ukifa Baba kila kitu kinakufa tutafakari tujiandae vipi hata kama ni ka-karakana ka karabati baiskeli tu!!

Familia ya Mzee Aikaeli Mbowe wamewezea hilo jambo lakini, ndo maana Club Bilicanas inaendelea hadi hii leo. Kwa hiyo siyo kila familia ya Kiafrika hushindwa kurithisha biashara. Ni wachache wanaowezea lakini wapo. Ufunguo katika mafanikio ya urithishaji ni kumtambua mapema anayeweza katika familia, hata kama ni mdogo kuliko wenzake na kuanza kumshirikisha mapema wenzake wajue mapema kuwa yeye hasa ndo mrithi. Ukisubiri maamuzi yafanywe na ukoo wakati umekufa ujue biashara imekufa hiyo. Unaanza kurithisha ukiwa bado hai. Corporate Succession Planning ndo inavyofanywa hivyo. Hata kama biashara ni gereji ya baiskeli ni muhimu kuanza mchakato wa urithishaji ukiwa bado upo hai.

Mtego wa mila ya kiafrika ya mtoto wa kwanza kuongoza kaya yako ukifa, kwa maana ya kuongoza hata biashara utazoacha ni upuuzi. Unaweza ukute toto la kwanza mburula kweli kweli. Kwa ufunguo ni kutambua anayeweza; hata kama ni mdogo. In fact anaweza hata awe ndugu wa karibu.
 
Wakuu ni kweli wapo wanao weza ila ni wachache sana, Compare na wahindi, na sababu kubwa ni kwamba, kurithisha ni mchakato mrefu sana unachukua hata zadi ya miaka 30,

Tatizo laWabongo ni kwamba tunaanza kutafuta mrithi au msimamizi wa biashara baada ya Mmmiliki kuwa amechoka na anahebu miezi ya kuishi,

Makampuni mengi kama wakina Toyota a wengineo wameweza kufanikiwa kwa sababu wao waliandaa familia zao mapema kuendeha biashara n kwa sasa ni kama ufarume huyu akifa tiyari kuna mwingine na huyo anaye ingia tiyali anacheo kikubwa sana ndani ya Kampuni,

Chukulia Mfano wa CHINA, CHAMA CHA KIKOMONIST CHA CHINA Kina utratibu mzuri sana wa kurithisha kwa sasa viongozi wa juu Ndani ya Chama ndo watakao chukua Nchi baada ya Raisi wa sasa kuachia madaraka, hawakurupuki kuchomoa mtu fom nowhere,

So katika kurithisha ni mchakato mrefu sana ikiwemo wa kumuandaa mrithi kielimu, kisaikolojia, na kazalika,mrith inatakiwa inafika mahali anakuwa nacheo kikubwa my be yeye ndo anakua anamfuatia Mmiliki kwa Cheo, na inafika mahali anaachiwa awe yeye ndo anafanya baadhi ya maamuzi ndani ya Kampuni,

Na ndo wanacho fanya Wahindi, Jaribu kwenda kwenye maduka yao uone, Baba amekaa pembeni mtoto ndo anafanya kila kitu hadi kubagaine Bei, kwa Wabongo ni nadara sana kukuta mtoto anaachiwa, so kwa yule mtoto wa kihindi hata baba akifa leo hakika mtoto aaweza endesha biashara bila tatizo,

Elimu nayo ni muhimu sana, Jaribu kuchunguza watoto wengi wa wahindi kozi wanazo soma Vyuoni, utagundua kwamba hawasomi kwa bahati mbaya, Wengi wao utakuta wanasoma
- Acounting
-Marketing
-Business Managment
-It
-Proqurement
Hizo ndo kozi zao kubwa wanazo soma na hawasomi kwa bahati mbaya, Huwezi kuta mtoto wa kihindi anasoma sijuia Mendeleo ya jamii,mara, History,

Jiulize ni wabongo wangapi wako vyuoni na wazazi wao wana kampuni kubwa lakini watoto wanasoma kozi tofauti kabisa? ni wengi sana,

SO ISHU YA KURITHISHA INA MCHAKATO MREFU SANA NA INACHUKUA MIAKA MINGI SANA NA KAMA WEWE UNA MTOTO NA WEWE NI MFANYA BIASHARA WAKATI NI SASA, UNATAKIWA UANZE KUMWADAAA AKIWA HATA BADO CHEKECHEA,
 
wakuu nalizani ni swali la kijinga kumbe limenifungua kufikiri upande wa pili mbele zaidi,tuna safari ndefu kuhakikisha invstment za wazazi zinaendelea kukua baada ya wazazi kufariki.

Hamnaga swali la kijinga mzee ndio maana mwalimu darasani huwa hamcheki mwanafunzi anapouliza swali.

Uvumbuzi wote ulianza na watu kujiuliza maswali kichwani halafu wakaanza kuchanja mbuga kutafuta ufumbuzi.
 
hamnaga swali la kijinga mzee ndio maana mwalimu darasani huwa hamcheki mwanafunzi anapouliza swali.

Uvumbuzi wote ulianza na watu kujiuliza maswali kichwani halafu wakaanza kuchanja mbuga kutafuta ufumbuzi.

umeongea kweli mkuu
 
JF katika ubora wake! na hapo ndo JF inapochukua hadhi yake!!!
 
habari zenu ndugu...nimeona si vyema kukaa na upofu wangu wa kutokujua mambo jinsi yanvyokwenda..swali langu lipo hivi...wale waanzilishi wa makampuni makubwa duniani kama Cocacola,Mercedes Benz.BMW, Ford n.k ambao wengi wao na marehem,je ndugu za(watoto wajukuu,vitukuu nk) wanafaidika vipi na makampuni haya yaliyoanzishwa na ngugu yao?
Wale bado ndo wana hisa kule na unaweza kukuta wajukuu au watoto ndo wakuu wa makampuni husika
 
Back
Top Bottom