Swali kwa wanaume waliooa tu

Swali kwa wanaume waliooa tu

ukiona hasira inakuzidi nguvu tafuta bia tu, piga mbili kwanza kichwa kikae sawa halafu ongea na mtu aliekukwaza, lazma muafaka upatikane kwa amani kabisa.. hata ukikwazana na mama watoto kapige bia rudi home, ukimwona lazma utamshushia mabusu, atabaki anashangaa tu..

IT WORKS FOR ME.

Kuna makosa mengine lazima upaniki. Na bia haishuki.
 
kama nilikuwa nimemchoka
''eeeh Mungu unipe nini mimi.''
talaka kisha nawahi kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa
 
Scanerio zote 2 ni usaliti ndani ya ndoa na jambo hilo kila mtu ana maamuzi yake na kutegemea na amerukwa akili kiasi gani, kwa hiyo ukitegemea majibu ya wadau hutopata aina moja ya maamuzi. Hivi hujawahi kusikia mtu ameuwa kwa jambo hilo? Hujawahi kusikia mtu amemwacha mke wake kwa hali hiyo? Hujawahi kusikia mwingine akimsamehe mke wake na kuacha maisha yaendelee, mwingine anaweza kuacha leo na akamrudia mke wake kesho nk nk kama yamekukuta chukua maamuzi unayoona yanastahili
 
'Scenario' namba moja:
Unarudi nyumbani toka mizunguko yako ya kila siku, unafika nyumbani hamadi unakutana na mke wako anakusaliti na mwanaume mwingine nyumbani kwako.

'Scenario' namba mbili:
Unapata taarifa kuwa mke wako wa ndoa anakusaliti, unafanya uchunguzi na kujiridhisha ni kweli anafanya hivyo. Na ushahidi unao.

Sasa naomba uniambie, wewe utafanya nini ukikutana na 'scenario' moja wapo hapo juu. Yani nataka uniambie ile 'immediate action' utakayoichukua ndani ya dakika moja unaposhuhudia suala hilo.
Sitaki uniambie utafanya nini baada ya siku au week au miezi kupita baada ya kitendo hiko.

Nadhani nimeeleweka.
Niliwahi kuambiwa na baba yangu kuwa siku zote unatakiwa uwe mtulivu wakat Wa hatar hvyo hata. Mm itanibidi nitulie kabla ya kuchukua uamuzi
 
Scenario 1:
Nitawapongeza kwa ujasiri walionao kugegedana ndani kwangu.

Scenario 2:
Nitawajulisha kuwa nimefaham mambo yao.

Conclusion.
NITAMFUKUZA.
Ndani kwako au kwenu?ukichukia ondoka wewe
 
Niliwahi kuambiwa na baba yangu kuwa siku zote unatakiwa uwe mtulivu wakat Wa hatar hvyo hata. Mm itanibidi nitulie kabla ya kuchukua uamuzi

Sawa sawa mkuu.
 
Jamaa nitamblacklist na huyo mshenzi atarudi kwao. Mbaya zaidi kufanyia katika nyumba yangu. Nikiwa na panga hapohapo kumfyeka huyo dume
 
Dawa yake muache aendelee akiwa nje ya kwako
 
Scenario 1:
Nitawapongeza kwa ujasiri walionao kugegedana ndani kwangu.

Scenario 2:
Nitawajulisha kuwa nimefaham mambo yao.

Conclusion.
NITAMFUKUZA.

Nakama ikiwa nyumba ni ya mwanamke.
Utapataje ujasili wa kumfukuza ?
 
'Scenario' namba moja:
Unarudi nyumbani toka mizunguko yako ya kila siku, unafika nyumbani hamadi unakutana na mke wako anakusaliti na mwanaume mwingine nyumbani kwako.

'Scenario' namba mbili:
Unapata taarifa kuwa mke wako wa ndoa anakusaliti, unafanya uchunguzi na kujiridhisha ni kweli anafanya hivyo. Na ushahidi unao.

Sasa naomba uniambie, wewe utafanya nini ukikutana na 'scenario' moja wapo hapo juu. Yani nataka uniambie ile 'immediate action' utakayoichukua ndani ya dakika moja unaposhuhudia suala hilo.
Sitaki uniambie utafanya nini baada ya siku au week au miezi kupita baada ya kitendo hiko.

Nadhani nimeeleweka.
Kuna mambo mpaka yatokee ndo unajuwa cha kufanya....
 
Nakama ikiwa nyumba ni ya mwanamke.
Utapataje ujasili wa kumfukuza ?
Hahahaha Mkuu, hii mada ni kwa wanaume waliooa sio wavulana walioolewa au wanaolelewa (MARIO).
 
Kama nimezaaaa nae nitamuacha kistaarab yaani bila watu kujua kilichotokea ili kuficha aibu kwa watoto.

KAMA sijazaa nae
Nitafunga mlango
Napiga simu polisi waje wawachukue wazinzi wote wakawaweke ndani
Then nawaita wazazi wake waje wamtoee lokapu waondoke nae
 
hata tukwambia haitakusaidia kwa chochote maana kila mtu ana kiwango chake cha udhibiti wa hasira,
 
Kwa scenarios zote mbili,
1. Nikimkuta jamaa anamwaga uno kwa mke wangu, kiuhalisia nitasononeka sana, nitanyongea ila sitafanya maamuzi ya pupa. Nitawaacha wamalize mambo yao, ila kwa upande wangu kuna vitu kadhaa vitabadilika, kama ratiba ya chakula na sitamfukuza.
2. Nitamuonesha ushahid nilionao ili ajue kwamba najua anachokifanya nyuma ya mgongo wangu.
 
Back
Top Bottom