Swali kwa Wanaopinga Mwendo wa Magufuli na Serikali Yake

Swali kwa Wanaopinga Mwendo wa Magufuli na Serikali Yake

Kama kweli ni mzalendo nahitaji vitu vitatu toka kwake....
1.Arudie mchakato wakatiba mpya ile ya WARIOBA na siyo ya CCM yakutetea viongozi.
2.Aamru JECHA wa tume ya uchaguzi akamatwe na kufikishwa mahakamani na matokeo ya uchaguzi Zanzibar atangazwe mshindi wake.
3.Ile miswada ya gesi ifumliwe maana ilipitishwa kama kwa shinikizo la mtu mwenye hofu ya kitu fulani na siyo kwa maslahi kwa taifa.
AKITEKELEZA HAYO YOTE NITAMWEKA KWENYE KUNDI LA WAZALENDO.
_4.jpg
 
Sawa MM, nimekusoma. Kwakuwa sie wengine hatukumchagua wala kumuunga mkono basi italazimu tuwe tunaomba kibali cha kumkosoa kutoka kwenye nyie mliomchagua. Better still, mtuhamishie nchi nyingine maana tulimkataa 'muokozi' wa taifa letu!!

Uchaguzi umeisha, kampeni zimeisha, mshindi kapatikana. Sherehe na nderemo za ushindi ziishe ile tujenge nchi. Sio busara kunyoosheana vidole kwa sasa. Pia tambua, hakuna mwenye haki ya kumuamlia mwingine amkosoe/asimkosoe fulani. Wanaomkosoa Magufuli wana haki kikatiba, hata kama hawatakuwa sahihi katika maoni yao.
Mfano, mpaka sasa kumekuwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu kuhusiana na uvunjaji wa makazi holela. Serikali inayoshindwa kupima viwanja wa kutosha kwa ajili ya makazi ya watu wake na ambayo kwa miongo mingi imeshindwa kuondoa urasimu katika taasisi zake za ardhi, haina 'moral authority' ya kuwavunjia watu nyumba. Hakuna asiyependa kiwanja kilichopimwa. Suala ni vinapimwa vingapi na vinatolewa kwa utaratibu gani. Hapa mheshimiwa rais wangu angeanza na kupima viwanja vya kutosha na kuvitoa hata kwa mkopo ili na wanyonge wafaidike na angeondoa urasimu halmashauri na wizara ya ardhi. Ndipo baada ya miaka 3 akianza kubomoa makazi holela tungemuelewa. Kubomoa nyumba ni rahisi sana kuliko kumuuzia mtu kiwanja kilichopimwa katika hiz serikali zetu za kiaAfrika.

Umeandika kitu cha maana sana sio hawa jamaa wanashangilia tu bila kufikiri
 
Kuna kauli ya kuipeleka tz kuwa nchi ya kipato cha kati,kwa mwenendo huu,wa serikali hii iliyopo,ambayo haina uwezo wa kumpa mtanzania huduma ya umeme wa uhakika kuwasha taa tatu,kuchaji simu pengine na tv tu kwa siku je hiko kipato cha kati tunafika kwa mwenendo upi?

Mfumo uliopo ni wakumuogopa Magufuli:

Wengi wa watu wanatenda kwa kumuogopa rais kama ilivyokuwa kwa hayati Moringe sokoine,alikuwa mkali sana ila ilivyoondoka na kuogopwa kwake kukazikwa rasmi,hata sasa watendaji wanatenda kwavile yeye Magufuli yupo madarakani,akiondoka?

Je, unafikiri inatakiwa ichukue muda gani kuifanya nchi iwe ya kipato cha kati? Rais ametimiza siku 60 tu za madaraka
Kama kuna wanaotenda kwa kumuogopa, na majukumu yanatekelezeka basi huu ndiyo wakati wa namna hii ya kutenda kazi, kwa sababu namna nyingine haziwezi kuleta matokeo, watu wameishi kwa mazoea kwa muda mrefu.

Lakini, swali la msingi hujajibu kwa usahihi. (ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?)

Jitahidi ujibu hili, usitoke nje ya mada.
 
Me nadhani mipango ingeanza kwa kuipima hii nchi japokuwa ni ngumu angalau ile mikoa potential au ktk baadhi ya maeneo, yan inatakiwa iwepo master plan ya nchi hii, na itekelezwe, maeneo ya wafugaj yajulikane, kilimo, viwanda makazi mashule nk, na haya yote yaweze ku forecast miaka ming ijayo sio 2020 wakat wa uchaguz, na wakupima wasiwe hawa maafisa ardhi wetu njaa hawana exposure yoyote ya dunia inapangwaje kulingana na resources, nchi za watu unakuta miji ya 1800 lkn kila kitu kiko kwenye plan, najua kuna majibu rahis kwamba plan zipo, cha ajabu kila cku bomoa bomoa
 
Ukishamaliza kupanga matumiz ya ardhi ndo ije mipango ya huduma za jamii na ile ya uchumi katika muda mrefu, wa kati na mfupi.
 
Hatutarajii kila mtu aone mambo ambayo rais Magufuli kafanya. Hivyo baki na ujinga wako...CCM mbele kwa mbele.
Wewe ndio unachangia ccm ionekane mbovu
Je, unafikiri inatakiwa ichukue muda gani kuifanya nchi iwe ya kipato cha kati? Rais ametimiza siku 60 tu za madaraka
Kama kuna wanaotenda kwa kumuogopa, na majukumu yanatekelezeka basi huu ndiyo wakati wa namna hii ya kutenda kazi, kwa sababu namna nyingine haziwezi kuleta matokeo, watu wameishi kwa mazoea kwa muda mrefu.

Lakini, swali la msingi hujajibu kwa usahihi. (ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?)

Jitahidi ujibu hili, usitoke nje ya mada.

Umenielewa nilichokiandika? Ndani ya siku sitini kuna mabadiliko ya mfumo? Kitu gani ambacho unaweza sema hapa papo sawa kwa uwepo wa Pombe madarakani?

Ni wazi wewe ni shabiki tu wa matokeo ila siyo mtu makini unaetaka vyanzo vipate tiba ili kuwezesha matokeo chanya yasiyotegemea flani yupo madarakani ama lah!
 
Sababu kubwa hasa ya wao kumpinga Raisi Magufuli wala haihusiani na yale anayoyafanya bali ni chuki binafsi tu ambayo wanayo dhidi ya Raisi Magufuli kama biandamu na pili dhidi ya Chama chake cha CCM, hakuna kitu ambacho Raisi Magufuli atafanya ambacho watamuunga mkono, kwa kifupi ni wafuasi wa fisadi Lowasa na lengo lao kubwa ni kutaka fisadi Lowasa wao abakie relevant kwenye siasa za TanZania na ndiyo maana wanakesha wakiomba Miungu yao ili tu Raisi Magufuli ashindwe kwa maana kuna watu wengi sana TanZania leo hii hasa wale waliompigia kura fisadi Lowasa wanasema kwamba anayoyafanya Raisi Magufuli fisadi Lowasa kama angeshinda Uraisi asingethubutu na wala asingeweza kuyafanya hata tu theluthi yake!

Hapo umeongea ukweli mtupu kiongozi barbrosa.

Hebu ona kibaraka huyu aliyetumia miaka zaidi ya kumi kutahadharidha wananchi dhidi ya fisadi nguli, kupitia maandamano na operation Sangara.
Ol over sudden naye akanaswa- Mara oooh kaulimbiu zikabadilika.
Mtu kama huyu ni wa kupuuuza tu
Labda nikuulize swali Mzee Mwanakijiji,
Kwani Magufuli amefanya nini?
Kukusanya mapato ni kazi ya kila siku! Hata Kikwete alijivunia kutoa mapato kutoka bilioni 177 hadi bilioni 970 na wafuasi wake walimpongeza kweli huku wakimponda Mkapa! Huyu JK aliongoza mapato mara 7 zaidi! Magufuli naye ameongeza na watu harakaharaka wameanza kufanya yaleyale waliyofanya kwa Kikwete!

Nikuulize mleta mada; Magufuli kafanya nini?

Nyie wakati Kikwete alipokuwa "rais fresh" kisha akasuluhisha mgogoro wa Kenya, akateuliwa mwenyekiti wa AU akawika kimataifa si mlimsifia usiku na mchana? Leo ni kama mmebadili mlo kutoka wa mchana kwenda wa usiku ndani ya nyumba ileile!

Mimi naanza na sipepesi juu ya hili nampinga kwakusema kuwa; Sera yake ya bomoa bomoa ina makosa mengi kiufundi! Pia kama siyo utapeli Mbona hakuinadi ili watu wamchague huku wakijua kuwa tutapambana na bomoa bomoa? Kama alivyoinadi sera ya mahakama ya ufisadi?

Nikuulize tena kwa mara ya tatu; Magufuli kafanya nini?
 
Wanaohoji amefanya nini JPM majibu ni Hays: Anezuwia fedha kutuamulia bali akili zetu zitumike. Ameanza kuthibitisha kuwa wakosaji wachukuliwe hatua stahiki. Ametuonyesha kuwa tunaweza wenyewe kupanga kipi tufanye kipi tusifanye. Ameonyesha kuwa familia inapaswa kuonekana wazi nani baba,mama na mtoto. Majukumu ya baba,mama na mtoto ni yapi. Amethibitisha baba timamu hasubiri baba wa kambo amwamrie nini cha kufanya. Luna mjibu hoja kaeleza kwa ufasaha mkubwa kuwa kwa sasa Shamba linaandaliwa. Bajeti ijayo mbegu za JPM zitaanza kupandwa. Wenye hekima watasubiri mavuno ili kupima uwezo wa utendaji wa JPM. Tatizo lipo "kwetu tunaoamini katika kuzungusha mikono na kipato kiongezeke kwa kusena tu"
 
Anawabomolea wanyonge nyumba badala ya kuwawezesha kujenga zilizo bora na mahali salama, Tunahitaji awape dignity wanyonge

Ameteua Waislamu wachache katika baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu, ni matumaini yangu hatowapa wadini sababu ya kunong'ona katika teuzi zake huko mbeleni
Iiish! la, da! mkuu salama lakini!

Nijulie hali
 
Home



Ndugai kuweka hadharani Kamati za kudumu Bunge
NA AUGUSTA NJOJI
7th January 2016

n2(2).png

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Spika wa Bunge, Job Ndugai (pichani chini) amesema anatarajia kutangaza kamati za kudumu za Bunge Januari 20, mwaka huu, mjini Dodoma, huku akisema ataziunda kuendana na wizara zilizoundwa na serikali.


Akizungumza na Nipashe, mjini hapa jana, Ndugai alisema hata hivyo hadi sasa bado hajaunda kamati hizo na hajui idadi itakavyokuwa kwa kila kamati, isipokuwa zitapungua idadi ili ziendane na wizara zilizoundwa na Rais John Magufuli.

“Kamati zitaundwa Dodoma na zitaendana na wizara zilizoundwa na serikali na vitaanza vikao vyake kabla ya kikao cha pili cha Bunge kuanza Januari 26, 2016,” alisema.

Katika Bunge lililopita la 10, ziliundwa kamati za kudumu za bunge 16, ambapo kulikuwa na wizara 30.

AZUNGUMZIA AFYA YAKE

Katika hatua nyingine, Ndugai alisema afya yake kwa sasa ni nzuri na kwamba sababu ya yeye kwenda India kutibiwa ni kutokana na uchovu wa pilikapilika za kampeni za uchaguzi mkuu uliopita hali iliyofanya mwili kukosa nguvu.

“Kwa sasa nipo ofisini nikitekeleza majukumu yangu baada ya kurudi kutoka India.

Kwa kweli namshukuru Mungu naendelea vizuri, kikubwa kilichokuwa kinanisumbua ni uchovu na mwili kukosa nguvu na hii imetokana na kutopata muda wa kupumzika,” alisema Ndugai.

Ndugai alienda kutibiwa India mwanzoni Disemba, mwaka jana na kurejea nchini Disemba 30, mwaka jana baada ya kupatiwa matibabu.

CHANZO: NIPASHE

My take
''Talks the talk but does not walk the talk''

1. Zuio la kusafiri kwenda nje linamgusa?
2. Ilikuwa ziara binafsi ya matibabu au iligharamiwa na serikali?
3. Zile MRI za Muhimbili zilizotengenezwa ni kwa kundi gani la jamii?
4. Hivi hatuna wataalamu wa kutibu uchovu nchini?
5 Wataalam wetu wa afya wanawezaje kutibu moyo, kisukuari, kiharusi n.k.?
6. Mtaalamu gani alitoa referal ya uchovu wa mwili kutibiwa nje ya nchi?
7. Ni kifaa gani cha uchunguzi kilichokosekana nchini?
8.Uchovu unaotokana na harakati za uchaguzi binafsi unatusa vipi sisi?
9. Kila mbunge akiamua kwenda kutibua uchovu, hazina itabaki na nini?
 
Last edited:
Magufuli anakurupuka katika uongozi wake. Jambo ambalo linakera wengi ni kuhusu Bomoa bomoa. Ni jambo zuri lakini amekurupuka mno.

Kwa sasa inapaswa kuangalia namna ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na ndio wimbo wapinzani walikuwa WANAIMBA KATIKA KAMPENI. Na pia ndio maana watu wengi walijiunga na upinzani kwa kutaka mabadiliko ya kiuchumi. lakini unapombomolea mtu nyumba katika kipindi hiki unampa umasikini wa hali ya juu kabisa.

Watu waliichukia CCM kutokana na miaka yote kushindwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi wake. na ndio maana wengi walijiunga na upande wa upinzani na kufanya uchaguzi kuwa mgumu sana kwa upande wa chama tawala.

Tuna changamoto nyingi ambazo zipo katika jamii ndizo serikali tulitarajia wataanza nazo. Hata katika kampeni Rais Magufuli hakutoa ahadi ya kuwa akichaguliwa, serikali yake watabomoa nyumba za makazi ya watu katika hali hii ambayo inawaacha wananchi wakikosa sehemu za kuishi. Huenda ndio moja ya sera ya CCM uchaguzi uliopia, lakini mbona hawakuisema katika kampeni ili tujue kabla??

Ni serikali gani hii isiyo na huruma kwa wananchi wake??????
kwanza uamuzi wa kuvunja makazi ya bondeni jpm ameukuta. ulikua uamuzi wa awamu ya jk yeye anatekeleza tu. watu waache kulalamika kama fani. wanalalamika matatizo na wanalalamika suluhisho.
 
kwanza uamuzi wa kuvunja makazi ya bondeni jpm ameukuta. ulikua uamuzi wa awamu ya jk yeye anatekeleza tu. watu waache kulalamika kama fani. wanalalamika matatizo na wanalalamika suluhisho.

Kwa hiyo kama ulikuwa ni uamuzi wa utawala wa JK, je yeye hkuwa na Tingatinga kipindi hicho hadi akashindwa???

Tunacholalamika sisi ni utaratibu unaotumika kaika bomoabomoa ni mbovu. kama ni fidia na viwanja Mabwe pande walipewa wa bonde la Msimbazi, lakini leo wanaguswa hadi wa Mbezi, Boko, keko, Kinondoni na hadi Mikoani ambako hawakuwa na fidia yoyote. Na pia ni zoezi la kushitukiza ambalo linawaacha wananchi wakilala nje kwakukosa makazi.

Hivyo kinachofanyika ni ubabe kwa kuwa serikali ina uwezo wa kufanya watakacho, lakini haki ya binadamu haitendeki hapa.

Serikali ingepaswa kuanza na matatizo yanayotukumba wananchi tulio wengi hapa Tanzania na siyo kwa jambo kama hili ambalo lina wagusa wachache lakini tunasikitika wengi kutokana na maamuzi yasiyo na ubinadamu.
 
ushindi mzuri ni ule wa kipyenga cha mwisho.mi bado nasubiria maana mbwembwe nimishazoea ila sipingi chochote mpaka sasa.labda nishauri escrow ni jipu kubwa jipya jipya lenye usaha mwingiii.tafadhali litumbueni upesi.
hilo tunamuachia lissu mkuu,...anashughulikia
 
Kwa yeyote anaye ona Mh Rais JPM anakosea au anamkera ni vyema akakaa kimya kwa sababu muda huu ni wa kuwatumikia wananchi na si longolongo.
Rais tutamsapoti na tutamuunga mkono ili wananchi waneemeke
 
Swali la Ugomvi: Kwa wale ambao hawakubali mabadiliko ambayo yanaongozwa na Magufuli na Serikali yake ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?
Swali hili linakuwa gumu zaidi kwa watu aina ya Mmawia...
.hawatajibu hoja na badala yake utaona vioja na mafananisho.
 
Swali la Ugomvi: Kwa wale ambao hawakubali mabadiliko ambayo yanaongozwa na Magufuli na Serikali yake ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?

Uliza kitu gani ambacho hajakifanya na hawezi kukifanya

Uliza ni kitu gani cha msingi zaidi ambacho sisi tungekifanya...ambacho ndio root cause ya kila kitu

Tusingefanya haya yote...Ila tungetanguliza katiba mpya ya wananchi ambayo ndiyo ingekuwa msingi wa kufanyika haya yote
 
Back
Top Bottom