Naona usipo andika chochote utaulizwa huko
sasa inabidi uandike tu hata kama unajichanganya changanya
Mara hajaanza kazi,mara anaenda kwa kasi.....unahangaika sana
Makala
Kwa nini Magufuli hajaanza kufanya kazi?
Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la
438
30 Dec 2015
MTU unaponunua eneo kwa ajili ya shamba au ujenzi vitu vya kwanza kabisa ambavyo unaangalia ni kitu gani kinatakiwa kufanyika kwanza kabla ya kuanza kwa kilimo au ujenzi. Kama eneo ni jipya kabisa bila ya shaka ni lazima uhakikishe mipaka iko sawa sawa, na kufanya uamuzi wa wapi patatumika kwa ajili ya nini na kwa vipi. Kama ni ujenzi wa nyumba basi utafanya uamuzi wa wapi nyumba yenyewe itajengwa na wapi vitu vingine vitakuwepo kwa kulinganisha na nyumba.
Na kabla ya kuanza kazi yenyewe kubwa kabisa utakalofanya ni kusafisha shamba – kama eneo ni la kilimo. Kama shamba lilikuwa linatumika tayari ni lazima uangalie kama utalitumia walivyolitumia wengine au utabadilisha matumizi yake ya zao unalotaka kulima kulinganisha na waliotangulia. Ni lazima usafishe shamba kwa ajili ya kilimo hata kama ulikuwa unalitumia kabla; hii ni kuhakikisha kuwa mazao mapya yanaandaliwa vizuri ili kuhakikisha mavuno unayotarajia.
Hadi hivi sasa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli hajaanza kazi; bado hajaanza kulima au kujenga. Amekabidhiwa ardhi kwa ajili ya kuihudumia kwa miaka mitano ijayo. Jambo la kwanza analolifanya na ambalo limemfanya achelewe kuanza kazi anayotaka ni lile la msingi; kusafisha shamba kwanza kabla ya kuanza kupanda mbegu anazotaka yeye kwa kutumia watalaamu wake.
Hii haina maana aliyekuwa kabla yake hakulima vizuri au hakusimamia shamba vizuri lakini ina maana tu kuwa sasa hivi kuna mkulima mwingine na y eye ana vipaumbele vyake. Kama mkulima aliyetangulia anaona kana kwamba mwenzie hafuati nyayo zake hili si jambo la kutolea maelezo; kila mtu kwa zamu yake na kwa nafasi yake. Hii ni zamu na nafasi ya Magufuli.
Kazi hii ya kusafisha kwa kiasi kikubwa ilioneshwa katika lile tukio la kusafisha siku ile ya Uhuru. Usafi ule haukumaanisha kuwa watu walikuwa hawasafishi (labda kweli walikuwa hawasafishi) lakini pia kulikuwa kunamaanisha juhudi zozote za kufanya usafi huko nyuma hazikuwa na matokeo yaliyotarajiwa. Hivyo, Magufuli anapokuja na wazo la kufanya usafi taifa zima alikuwa anatuma ujumbe tu kuwa hatuwezi kuishi na kuwa na maisha ya kufurahia kama hatuko safi; na hasa kama tumezungukwa na uchafu. Na sote tuliona jinsi gani nchi nzima kweli ilikuwa inahitaji usafi!
Hadi hivi sasa kwa kuangalia ambacho Magufuli amekifanya hadi hivi sasa hakuna shaka kabisa; kazi yake hasa itaanza baada ya bajeti ijayo. Miezi hii sita hadi wakati huo itatumiwa kwa kiasi kikubwa kusafisha na kupanga serikali na uongozi wake. Ni kwa sababu hiyo ni lazima watu wajiandae kiakili kuwa katika kutimiza lengo hilo la kupanga na kusafisha serikali kuna watu watang’oka, kuna watu wataenda kwenye ajira binafsi na tusije kushangaa baadhi ya watu ni lazima wang’oke kama kweli tunataka kujipanga vizuri.
Magufuli hadi hivi sasa ameshatuma ujumbe kuwa hakuna mti mtakatifu; kila kisiki kitaangaliwa na kile kinachotakiwa kung’olewa kitang’olewa. Ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono Rais katika juhudi hizi. Hadi hivi sasa bado watu hawajashtuka vya kutosha. Kama nilivyosema huko nyuma kuwa hii siyo siku ya jana; leo ni siku mpya na ambaye bado anadhani hii ni jana inabidi tumsaidie atambue kuwa hii ni siku mpya.
Magufuli atasafisha, atang’oa, atahamisha (vinavyostahili) lakini jambo moja la uhakika ni kuwa hakuna mahali ambapo hapataangaliwa kwa karibu. Kwa watu ambao tumefurahia kuingia kwa Magufuli jambo jingine ni lazima tuliseme kama tunataka tuwe wakweli. Magufuli hawezi kulima kama alivyolima mwingine; hapaswi kupanda alivyopanda mwingine; na hapaswi kusimamia shamba kama alivyofanya mwingine. Anaingia akiwa na malengo yake, vipaji vyake, mitazamo yake na malengo yake. Kama anataka kuona mazao ambayo ataweza kusema ni ya kwake kweli basi ni lazima awe tayari kutengeneza anavyotaka yeye na kuhakikisha anasimamia ili wengine wasimharibie.
Rais Kikwete kama kuna kitu watu walikuwa wanakisema ni kuwa “anaangushwa na wasaidizi wake”. Ilifika mahali watu walikuwa tayari kulaumu watu wengine wote isipokuwa Kikwete. Hadi siku ile John Mnyika wakati huo akiwa Mbunge wa Ubungo aliposimama bungeni na kusema kuwa taifa limefikishwa hapa kutokana udhaifu wa wengi lakini kubwa ni “udhaifu” wa Rais Kikwete. Kusema kweli Jeshi linasimama au kuanguka na Amiri Jeshi Mkuu wake! Huwezi kulaumu askari wa chini, brigedi moja au kushindwa kwa pigano moja hata kama mwisho wa siku Amiri Jeshi Mkuu haongozi jeshi vizuri wakati wa vita.
Hatutampa anasa hiyo Magufuli; hatutalaumu watendaji wake, hatutawasingizia watu wa chini; yeye ndiye atakayebeba lawama zote pale ambapo mambo yatatokea na yeye akachelewa kuchukua hatua au akaja na mtindo ule ule wa aliyemtangulia. Tutamnyoshea kidole na kusema kama ni udhaifu wake.
Lakini pia tutamuunga mkono na kumpongeza. Kama mavuno yatakuwa mazuri na ya kuridhisha kwani hata asafishe vipi, hata akate visiki vingi, hata achimbue wapi na wapi mwisho wa siku tutapima kwa matunda tu. Kuna faida gani kusafisha shamba, kupalilia, kufyeka, kukata miti, kuweka mbolea n.k kama mwisho wa siku mavuno yake yatakuwa mabaya?
- See more at:
Raia Mwema - Kwa nini Magufuli hajaanza kufanya kazi?