Swali kwa Wanaopinga Mwendo wa Magufuli na Serikali Yake

Swali kwa Wanaopinga Mwendo wa Magufuli na Serikali Yake

Labda nikuulize swali Mzee Mwanakijiji,
Kwani Magufuli amefanya nini?
Kukusanya mapato ni kazi ya kila siku! Hata Kikwete alijivunia kutoa mapato kutoka bilioni 177 hadi bilioni 970 na wafuasi wake walimpongeza kweli huku wakimponda Mkapa! Huyu JK aliongoza mapato mara 7 zaidi! Magufuli naye ameongeza na watu harakaharaka wameanza kufanya yaleyale waliyofanya kwa Kikwete!

Nikuulize mleta mada; Magufuli kafanya nini?

Nyie wakati Kikwete alipokuwa "rais fresh" kisha akasuluhisha mgogoro wa Kenya, akateuliwa mwenyekiti wa AU akawika kimataifa si mlimsifia usiku na mchana? Leo ni kama mmebadili mlo kutoka wa mchana kwenda wa usiku ndani ya nyumba ileile!

Mimi naanza na sipepesi juu ya hili nampinga kwakusema kuwa; Sera yake ya bomoa bomoa ina makosa mengi kiufundi! Pia kama siyo utapeli Mbona hakuinadi ili watu wamchague huku wakijua kuwa tutapambana na bomoa bomoa? Kama alivyoinadi sera ya mahakama ya ufisadi?

Nikuulize tena kwa mara ya tatu; Magufuli kafanya nini?
Hatutarajii kila mtu aone mambo ambayo rais Magufuli kafanya. Hivyo baki na ujinga wako...CCM mbele kwa mbele.
 
Nilikuwa tayari kuona Tanzania inaoongozwa na Rungwe lakini sio kumuona fisadi Lowassa anachukua nchi. Kila maamuzi ambayo rais Dkt Magufuli anafanya yapo kwenye Ilani ya CCM...Kama chuki ya hao Nyumbu ipo, basi waichukie CCM ambayo imemtuma rais Magufuli atekeleze Ilani yake. Na hiyo inajumuisha ishu ya bomoa bomoa pia. Kurasa mbili zimeongelea hili suala na rais analitekeleza kwa ufasaha kabisa.

Aanze na majipu makubwa kama Escrow,hili la bomoa bomoa lina haraka gani?Bado IPTL wanaendelea kutukamua 4 bilion a month,sasa kipi kipaumbele?Haya naona ni maigizo tu,majipu makubwa hayajaguswa
 
Kama kweli ni mzalendo nahitaji vitu vitatu toka kwake....
1.Arudie mchakato wakatiba mpya ile ya WARIOBA na siyo ya CCM yakutetea viongozi.
2.Aamru JECHA wa tume ya uchaguzi akamatwe na kufikishwa mahakamani na matokeo ya uchaguzi Zanzibar atangazwe mshindi wake.
3.Ile miswada ya gesi ifumliwe maana ilipitishwa kama kwa shinikizo la mtu mwenye hofu ya kitu fulani na siyo kwa maslahi kwa taifa.
AKITEKELEZA HAYO YOTE NITAMWEKA KWENYE KUNDI LA WAZALENDO.
 
Sawa MM, nimekusoma. Kwakuwa sie wengine hatukumchagua wala kumuunga mkono basi italazimu tuwe tunaomba kibali cha kumkosoa kutoka kwenye nyie mliomchagua. Better still, mtuhamishie nchi nyingine maana tulimkataa 'muokozi' wa taifa letu!!

Uchaguzi umeisha, kampeni zimeisha, mshindi kapatikana. Sherehe na nderemo za ushindi ziishe ile tujenge nchi. Sio busara kunyoosheana vidole kwa sasa. Pia tambua, hakuna mwenye haki ya kumuamlia mwingine amkosoe/asimkosoe fulani. Wanaomkosoa Magufuli wana haki kikatiba, hata kama hawatakuwa sahihi katika maoni yao.
Mfano, mpaka sasa kumekuwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu kuhusiana na uvunjaji wa makazi holela. Serikali inayoshindwa kupima viwanja wa kutosha kwa ajili ya makazi ya watu wake na ambayo kwa miongo mingi imeshindwa kuondoa urasimu katika taasisi zake za ardhi, haina 'moral authority' ya kuwavunjia watu nyumba. Hakuna asiyependa kiwanja kilichopimwa. Suala ni vinapimwa vingapi na vinatolewa kwa utaratibu gani. Hapa mheshimiwa rais wangu angeanza na kupima viwanja vya kutosha na kuvitoa hata kwa mkopo ili na wanyonge wafaidike na angeondoa urasimu halmashauri na wizara ya ardhi. Ndipo baada ya miaka 3 akianza kubomoa makazi holela tungemuelewa. Kubomoa nyumba ni rahisi sana kuliko kumuuzia mtu kiwanja kilichopimwa katika hiz serikali zetu za kiaAfrika.
 
Swali la Ugomvi: Kwa wale ambao hawakubali mabadiliko ambayo yanaongozwa na Magufuli na Serikali yake ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?

NINGETENGUA KUTUMIA "THE ENVIRONMENTAL MANAGEMENT ACT, 2004" THAT REPEALED "The National Environment Management Act, 1983" kuwabomolea wananchi ambao wamekuwa na makazi yao tokea miaka ya 1960 pasipo kuwalipa fidia na kupeleka kutendewa unyama mkubwa kiasi kile kwa familia na watoto kulala nje.
 
Hawana majibu. Ni chuki binafsi. Pembeni wanasema anatekeleza ilani yao!!!
Queen Esther
 
Mara ya mwisho mafuriko Dar yaliua watu wangapi?? Na wangapi waliachwa bila makazi??
Queen Esther

NINGETENGUA KUTUMIA "THE ENVIRONMENTAL MANAGEMENT ACT, 2004" THAT REPEALED "The National Environment Management Act, 1983" kuwabomolea wananchi ambao wamekuwa na makazi yao tokea miaka ya 1960 pasipo kuwalipa fidia na kupeleka kutendewa unyama mkubwa kiasi kile kwa familia na watoto kulala nje.
 
Swali la Ugomvi: Kwa wale ambao hawakubali mabadiliko ambayo yanaongozwa na Magufuli na Serikali yake ni kitu gani ambacho wao wasingekifanya ambacho Magufuli amekifanya? Kwamba, kama wangekuwa na uwezo "wangetengua" mambo gani ambayo Magufuli ameyafanya hadi sasa?
Sasa mzee naona unazeeka zaidi ungeyaeleza ambayo yanayofanya na Mh Magufuli na wanayoyapinga ili watu watoe hoja na sio chuki zaidi vinginevyo unataka watu wachangie kwa chuki na sio hoja
 
Halafu kuna jambo moja linanisumbua sana mimi.

Fine, lengo la bomoa bomoa kwa mujibu wa waboaji ni;

1. Kwanza wanasema ni kuokoa maisha ya hao watu kwa sababu eti wamejenga na wanaishi maeneo hatarishi ya mikondo ya maji na mafuriko na;

2. Pili wanasema wamejenga na wanaishi maeneo ambayo ni hifadhi za serikali kwa maana ya mito, sehemu za wazi nk

Kama haya ndivyo, hivi ilikuwaje serikali hiihii ambayo leo inabomolea watu wake makazi yao iliweza kutoa hadi hati za viwanja za baadhi ya watu hawa, ikawapelekea hadi huduma za kijamii kama umeme, barabara, simu, shule nk??

Leo inakuwaje serikali iwaone watu hawa wamejenga kinyume cha sheria na kisha inawabomelea nyumba zao kinyama, kuwaacha bila makazi na bila kuwapa maeneo mbadala ya wao na familia zao kuishi!!??.....Ki ukweli, I don't get it!

Sikatai kuwa ktk msafara wa kenge, lazima tu na mamba huwepo.

Nina maana kwamba, wapo ambao kweli ni wavamizi na hawana vibali vyovyote vya serikali kuwaruhusu kujenga na kuishi mahali flani

Lakini kuna watu wanabomolewa nyumba zao huku wakilalamika kuwa wanaishi mahali pale kihalali, na ndipo lilipo tatizo hapa!!

Kingine na ambacho kinashangaza kidogo ni kuwa, hivi inakuwaje watu ambao wameishi mahali kwa miaka 30, 50 au hata 70 leo anaambiwa yupo hapo kimakosa!!?

Hivi, kabla ya hapo hakukuwa na serikali inayoweza kuona hayo na kuyazuia kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi kama ilivyo leo?

Hapa kiukweli something is wrong somewhere!!.

Si rahisi kukomesha tatizo hili kabisa iwapo waliofumbia mambo haya yalipoanza kujitokeza nao hawatachukuliwa hatua za kisheria bila kujali ni kina nani.

Hawa nina maana ya wale watu waliokuwa na nguvu na mamlaka ya kisheria kuzuia/kusimamia sheria na hawakutenda au kutekeleza wajibu wao. Na hapa serikali na CCM hawawezi kukwepa lawama hizi, sharti yenyewe ijiwajibishe au wawajibishwe kwa nguvu!

Nadhani, kwangu mimi, Rais JPM akitekeleza hii operesheni bomoa bomoa kwa uelekeo huu nitamuona ana lengo zuri, lakini kama ni hivi.....no way, ni visasi vya kisiasa tu hivi!!

Sawa MM, nimekusoma. Kwakuwa sie wengine hatukumchagua wala kumuunga mkono basi italazimu tuwe tunaomba kibali cha kumkosoa kutoka kwenye nyie mliomchagua. Better still, mtuhamishie nchi nyingine maana tulimkataa 'muokozi' wa taifa letu!!

Uchaguzi umeisha, kampeni zimeisha, mshindi kapatikana. Sherehe na nderemo za ushindi ziishe ile tujenge nchi. Sio busara kunyoosheana vidole kwa sasa. Pia tambua, hakuna mwenye haki ya kumuamlia mwingine amkosoe/asimkosoe fulani. Wanaomkosoa Magufuli wana haki kikatiba, hata kama hawatakuwa sahihi katika maoni yao.
Mfano, mpaka sasa kumekuwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu kuhusiana na uvunjaji wa makazi holela. Serikali inayoshindwa kupima viwanja wa kutosha kwa ajili ya makazi ya watu wake na ambayo kwa miongo mingi imeshindwa kuondoa urasimu katika taasisi zake za ardhi, haina 'moral authority' ya kuwavunjia watu nyumba. Hakuna asiyependa kiwanja kilichopimwa. Suala ni vinapimwa vingapi na vinatolewa kwa utaratibu gani. Hapa mheshimiwa rais wangu angeanza na kupima viwanja vya kutosha na kuvitoa hata kwa mkopo ili na wanyonge wafaidike na angeondoa urasimu halmashauri na wizara ya ardhi. Ndipo baada ya miaka 3 akianza kubomoa makazi holela tungemuelewa. Kubomoa nyumba ni rahisi sana kuliko kumuuzia mtu kiwanja kilichopimwa katika hiz serikali zetu za kiaAfrika.
 
Last edited:
][/QUOTE]



Unaleta tu picha lkn hausemi ulitaka nini kifanyike au Serikali ifanye nini kwa watu waliojenga Mabondeni?
 
Last edited:
Naona usipo andika chochote utaulizwa huko
sasa inabidi uandike tu hata kama unajichanganya changanya

Mara hajaanza kazi,mara anaenda kwa kasi.....unahangaika sana


Makala


Kwa nini Magufuli hajaanza kufanya kazi?
Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 438
30 Dec 2015



MTU unaponunua eneo kwa ajili ya shamba au ujenzi vitu vya kwanza kabisa ambavyo unaangalia ni kitu gani kinatakiwa kufanyika kwanza kabla ya kuanza kwa kilimo au ujenzi. Kama eneo ni jipya kabisa bila ya shaka ni lazima uhakikishe mipaka iko sawa sawa, na kufanya uamuzi wa wapi patatumika kwa ajili ya nini na kwa vipi. Kama ni ujenzi wa nyumba basi utafanya uamuzi wa wapi nyumba yenyewe itajengwa na wapi vitu vingine vitakuwepo kwa kulinganisha na nyumba.
Na kabla ya kuanza kazi yenyewe kubwa kabisa utakalofanya ni kusafisha shamba – kama eneo ni la kilimo. Kama shamba lilikuwa linatumika tayari ni lazima uangalie kama utalitumia walivyolitumia wengine au utabadilisha matumizi yake ya zao unalotaka kulima kulinganisha na waliotangulia. Ni lazima usafishe shamba kwa ajili ya kilimo hata kama ulikuwa unalitumia kabla; hii ni kuhakikisha kuwa mazao mapya yanaandaliwa vizuri ili kuhakikisha mavuno unayotarajia.
Hadi hivi sasa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli hajaanza kazi; bado hajaanza kulima au kujenga. Amekabidhiwa ardhi kwa ajili ya kuihudumia kwa miaka mitano ijayo. Jambo la kwanza analolifanya na ambalo limemfanya achelewe kuanza kazi anayotaka ni lile la msingi; kusafisha shamba kwanza kabla ya kuanza kupanda mbegu anazotaka yeye kwa kutumia watalaamu wake.
Hii haina maana aliyekuwa kabla yake hakulima vizuri au hakusimamia shamba vizuri lakini ina maana tu kuwa sasa hivi kuna mkulima mwingine na y eye ana vipaumbele vyake. Kama mkulima aliyetangulia anaona kana kwamba mwenzie hafuati nyayo zake hili si jambo la kutolea maelezo; kila mtu kwa zamu yake na kwa nafasi yake. Hii ni zamu na nafasi ya Magufuli.
Kazi hii ya kusafisha kwa kiasi kikubwa ilioneshwa katika lile tukio la kusafisha siku ile ya Uhuru. Usafi ule haukumaanisha kuwa watu walikuwa hawasafishi (labda kweli walikuwa hawasafishi) lakini pia kulikuwa kunamaanisha juhudi zozote za kufanya usafi huko nyuma hazikuwa na matokeo yaliyotarajiwa. Hivyo, Magufuli anapokuja na wazo la kufanya usafi taifa zima alikuwa anatuma ujumbe tu kuwa hatuwezi kuishi na kuwa na maisha ya kufurahia kama hatuko safi; na hasa kama tumezungukwa na uchafu. Na sote tuliona jinsi gani nchi nzima kweli ilikuwa inahitaji usafi!
Hadi hivi sasa kwa kuangalia ambacho Magufuli amekifanya hadi hivi sasa hakuna shaka kabisa; kazi yake hasa itaanza baada ya bajeti ijayo. Miezi hii sita hadi wakati huo itatumiwa kwa kiasi kikubwa kusafisha na kupanga serikali na uongozi wake. Ni kwa sababu hiyo ni lazima watu wajiandae kiakili kuwa katika kutimiza lengo hilo la kupanga na kusafisha serikali kuna watu watang’oka, kuna watu wataenda kwenye ajira binafsi na tusije kushangaa baadhi ya watu ni lazima wang’oke kama kweli tunataka kujipanga vizuri.
Magufuli hadi hivi sasa ameshatuma ujumbe kuwa hakuna mti mtakatifu; kila kisiki kitaangaliwa na kile kinachotakiwa kung’olewa kitang’olewa. Ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono Rais katika juhudi hizi. Hadi hivi sasa bado watu hawajashtuka vya kutosha. Kama nilivyosema huko nyuma kuwa hii siyo siku ya jana; leo ni siku mpya na ambaye bado anadhani hii ni jana inabidi tumsaidie atambue kuwa hii ni siku mpya.
Magufuli atasafisha, atang’oa, atahamisha (vinavyostahili) lakini jambo moja la uhakika ni kuwa hakuna mahali ambapo hapataangaliwa kwa karibu. Kwa watu ambao tumefurahia kuingia kwa Magufuli jambo jingine ni lazima tuliseme kama tunataka tuwe wakweli. Magufuli hawezi kulima kama alivyolima mwingine; hapaswi kupanda alivyopanda mwingine; na hapaswi kusimamia shamba kama alivyofanya mwingine. Anaingia akiwa na malengo yake, vipaji vyake, mitazamo yake na malengo yake. Kama anataka kuona mazao ambayo ataweza kusema ni ya kwake kweli basi ni lazima awe tayari kutengeneza anavyotaka yeye na kuhakikisha anasimamia ili wengine wasimharibie.
Rais Kikwete kama kuna kitu watu walikuwa wanakisema ni kuwa “anaangushwa na wasaidizi wake”. Ilifika mahali watu walikuwa tayari kulaumu watu wengine wote isipokuwa Kikwete. Hadi siku ile John Mnyika wakati huo akiwa Mbunge wa Ubungo aliposimama bungeni na kusema kuwa taifa limefikishwa hapa kutokana udhaifu wa wengi lakini kubwa ni “udhaifu” wa Rais Kikwete. Kusema kweli Jeshi linasimama au kuanguka na Amiri Jeshi Mkuu wake! Huwezi kulaumu askari wa chini, brigedi moja au kushindwa kwa pigano moja hata kama mwisho wa siku Amiri Jeshi Mkuu haongozi jeshi vizuri wakati wa vita.
Hatutampa anasa hiyo Magufuli; hatutalaumu watendaji wake, hatutawasingizia watu wa chini; yeye ndiye atakayebeba lawama zote pale ambapo mambo yatatokea na yeye akachelewa kuchukua hatua au akaja na mtindo ule ule wa aliyemtangulia. Tutamnyoshea kidole na kusema kama ni udhaifu wake.
Lakini pia tutamuunga mkono na kumpongeza. Kama mavuno yatakuwa mazuri na ya kuridhisha kwani hata asafishe vipi, hata akate visiki vingi, hata achimbue wapi na wapi mwisho wa siku tutapima kwa matunda tu. Kuna faida gani kusafisha shamba, kupalilia, kufyeka, kukata miti, kuweka mbolea n.k kama mwisho wa siku mavuno yake yatakuwa mabaya?

- See more at: Raia Mwema - Kwa nini Magufuli hajaanza kufanya kazi?
01-Lowasa.jpg
 
Kwani Magufuli kafanya yapi hadi apingwe,Tuambizane ili nasisi tusioona angalau tusikie mazuri yake,maana kila siku watu wanalalamika kuwa kunabomoabomoa,maisha huku mitaani ni magumu sana..Natega sikio kusikia maana mimi ni kipofu.
 
By the way MM, Lula amekujibu. lakini ile makala uliyoandikia RAI wiki iliopita ilikuwa ushu.zi mtupu
Just give it a break
 
Utawala wake wa kimabavu yeye kwake hakuna kitu kinaitwa busara na mm niseme katika kipindi chake hiki bila kua na strong judiciary tutashuhudia aki za binadam zikivunjwa kwa kiasi kikubwa

Kipind cha nyerere mambo kama haya yalikuwepo ila hayakuonekana kwa sababu judiciary ilikua strong wastaafu kwa aman wazee wetu hakina judge nyarari ,mwalusanya na wengine weng walitafsir sheria vizur mno pongez za kipekee zimwendee judge wa kesi ya bomoabomoa ya juz kwa kufanya kaz nzur bila kufata pressure za makomeo
 
...nikikumbuka kuwa kuna wakati nikianza kukusoma siangaliii pembeni mpaka nimalize... lakini sasa hivi...mfano hii post yako hata sijamaliza neno la kwaza tangu saa tatu asubuhi nilivyoanza... argh!!!
 
Anawabomolea wanyonge nyumba badala ya kuwawezesha kujenga zilizo bora na mahali salama, Tunahitaji awape dignity wanyonge

Ameteua Waislamu wachache katika baraza la Mawaziri na Makatibu wakuu, ni matumaini yangu hatowapa wadini sababu ya kunong'ona katika teuzi zake huko mbeleni
 
Last edited:
Kama kweli ni mzalendo nahitaji vitu vitatu toka kwake....
1.Arudie mchakato wakatiba mpya ile ya WARIOBA na siyo ya CCM yakutetea viongozi.
2.Aamru JECHA wa tume ya uchaguzi akamatwe na kufikishwa mahakamani na matokeo ya uchaguzi Zanzibar atangazwe mshindi wake.
3.Ile miswada ya gesi ifumliwe maana ilipitishwa kama kwa shinikizo la mtu mwenye hofu ya kitu fulani na siyo kwa maslahi kwa taifa.
AKITEKELEZA HAYO YOTE NITAMWEKA KWENYE KUNDI LA WAZALENDO.



Hatutaki mambo ya Katiba hatuna huwo muda hii hii inatufaa na wala hatumchagua kwa wingi ili aje ashughulikie Katiba!
 
Nampenda magufuri ila spendi lichama lake, kwa kuwa lilifilisi nchi kwani hata majizi anayotumbua majipu yote ni makada ya ccm, au mafdhili, yani yanatuibia yanagawana na lichama ccm, kama Magufuri akiachana na lichama lake anaweza kupata kura za kishindo 98%
 
Back
Top Bottom