Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,594
- Thread starter
-
- #21
Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?
Hapa kuna hoja ya msingi hasa katika upinzani wa Tanzania ambapo unafanya kazi kwa huruma ya watawala. Hivi hawa wote ambao wanatoka CCM dakika hizi wakati CDM wanapigwa mabomu, wanauawa na kunyanyaswa waliiwahi hata dakika moja kutoa kauli ya kuwatetea? au hata kuonesha sympathy?
Mkuu Mzee Mwanakijiji, hakuna yoyote anayekatwa CCM, na kuamua kuhamia Chadema eti kwa sababu haipendi CCM na sera zake, wahamiaji wote waliogombea CCM, waligombea CCM kwa sababu waliipenda, na kuhama kwao, CCM, sio kuhama kwa sababu sasa hawaipendi CCM, bali wanahama ili kuiadhibu CCM, na kujiunga kwao Chadema, sio kwa sababu sasa ndio wanaipenda Chadema, bali Chadema ndicho chama pekee kinachoweza kutumika kama bakora ya kuiadhibia CCM, and it is onlt wakiwa nje ya box, ndio wataingiwa na upendo wa kweli kwa Chadema, na hivi ndivyo walivyopatikana baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, Dr.W.Slaa, alikuwa CCM, akagombea kupitia CCM, akashinda kura za maoni za CCM, akakatwa na vikao vya juu vya CCM, akajiengua CCM (huku kadi yake ya CCM akiendelea kuihifadhi kama kumbukumbu hadi leo), ajajiunga Chadema (bila kukabidhi kadi ya CCM kama wafanyavyo wengine), Chadema kikampokea kwa mikono miwili, akagombea kupitia Chadema na akashinda kwa kishindo ubunge!. Hivyo hiki kinachoenelea sasa sio kitu kipya, kimekuwepo huko nyuma, kipo sasa, na kitaendelea kuwepo siku za usoni!.Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?.
Naunga mkono hoja yako ya Chadema kuwasimamisha walianguka Chadema, kwenye majimbo mengine yenye wagombea dhaifu wa CCM, ili siungi mkono hii kauli yako ya kibaguzi ya kuwaita wapokelewa wapya kuwa ni wanamageuzi uchwara!. Wengi ni mashahidi, kuna baadhi ya wana CCM walikuwa ni wana mageuzi shupavu zaidi hata walipokuwa ndani ya CCM kuliko hata baadhi ya wanamageuzi waliopo Chadema!. Tukianza kunyoosheana vidole vya kumuita kila aliyetoka CCM kujiunga Chadema ni mwana mageuzi uchwala, then tuache cherry picking na double standards, kwa kuwaweka wote waliotoka CCM kujiunga Chadema ni wanamageuzi uchara, akiwemo Dr. Wilbrod Slaa!. Is this fair kweli?!. To me, this is not fair hata kidogo!. Hebu pitia uzi huu, [h=3]Mbunge wa CCM, Mhe. Esta Bulaya, Afanya Tukio la KishujaaTusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?
Kama unatatizo nao, unaonaje kama tukianzia kwa Dr?!, maana na yeye alikatwa ndipo akakimbilia Chadema, kumbe kwako wewe Mkuu Mzee Mwanakijiji, hata Dr.W.Slaa ni mtu mwenye tamaa ya madaraka?!.Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
Rudi nyumbani ugombee udiwani, ujenge Taifa, nchi bado inakuhitaji
Mkuu , I see your point, ila siasa ni vita, ili kuingia ikulu, inabidi wapinzani watumie kila silaha, kamwe huwezi kumshinda adui yako kama hijui nguvu yake, ndio maana kwenye mbinu za medani kuna kitu kinaitwa infiltration, au hata kutumia chambo, au kukamata mateka!, hawa big fish kutoka CCM ni WMD zitakazo tumika kuiangamiza CCM na kuuingiza Chadema Ikulu!.uhalisia nimejifunza vitu vingi sana kwa sasa!!! na naanza kuamini kuwa Tanzania ya ya sasa haita pata ukombozi kutoka kwa chama chochote cha siasa!
Nimegundua vyama vyote vya siasa nchini hasa upinzani vipo kwa maslahi binafsi!!! rejea sasa umoja wa UKAWA unavyo hangaika na lowasa lengo sasa imekua kushika dola kwa kigezo kinaitwa ondoa mfumo wa ccm!!! wakati huo mfumo unao uondoa umejengwa na watu na watu wenyewe mmoja wao ni lowasa why sasa!!!!????
lakini pia Uwezo mdogo wa watanzania kupambanua mambo na kusababisha kulaghaiwa na wana siasa kuna nipa picha kuwa hakutakua nauongozi thabiti mika 100 tena ijayo! rejea mikutano ya CCM kwa wananchi hasa ya katibu wao mkuu utaona kabisa kuwa ni porojo kutafuta public sympath! kwa kujifanya kukemea ama kuibua matatizo ya wananchi nakujitia ukakamavu wa kuhaidi kuyatatua kitu ambacho wamefeli kwa 20 years sasa!!!! lakini juzi pia nimesikitishwa na CDM kuna kauli ilitoka pale mwanza kwamba MMEWASAMEHE??????? wengi wakajibu NDIOOOOO! kumbe ni mbinu ya maandalizi ya kumsamehe na Lowasa???? na wenzake walio jenga mfumo wa kifisadi huko ccm kwani cdm haijiamini kwa watuilio nao????
si vibaya kwa watu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine, ila naangalia mtindo wa sasa, watu wa nahama kutoka ccm kwenda CDM mainly kwasababu maslahi yao binafsi yameshindwa kutimia huko ccm, wengine wanatoka CDM kwasabababu wameshindwa kupata nafasi ya kutetea maslahi yao binafsi kwangu ndo naiona sababu kuu!!! sasa tujiulize swali hawa wanao hamia humu walikuwa wapi siku zote????? yakina kua ya akina shibuda mtafanyaje???? kunania yadhati kweli ya kutukwamua hapa tulipo????
sad news nikwamba viongozi wetu nao wanalalamika kama sisi!!! tutafika???
soma uelewe hatutasubiri bali aina maana hatutapokea wanachama wapya wa chadema.kugombea .kumbuka unakuwa mwanachadema kwanza baada ya hapo ruksa kugombea .kwa kazi muhimu kuitoa ccm madarakaniHii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!
Pitia hapa,.soma uelewe hatutasubiri bali aina maana hatutapokea wanachama wapya wa chadema.kugombea .kumbuka unakuwa mwanachadema kwanza baada ya hapo ruksa kugombea .kwa kazi muhimu kuitoa ccm madarakani
Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,
Ni vizuri kidogo kukumbuka mazingira ya siasa ya wakati ule 1995 na mazingira ya wakati huu... CDM ya 1995 siyo ya sasa; mwaka ule watu tulikuwa tunazungumzia NCCR Mageuzi, UMD, CUF n.k...
Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?
Hapa kuna hoja ya msingi hasa katika upinzani wa Tanzania ambapo unafanya kazi kwa huruma ya watawala. Hivi hawa wote ambao wanatoka CCM dakika hizi wakati CDM wanapigwa mabomu, wanauawa na kunyanyaswa waliiwahi hata dakika moja kutoa kauli ya kuwatetea? au hata kuonesha sympathy?
Mkuu, ukitumia kigezo cha aina hiyo siasa itakuwa ngumu. Kumbuka, CCM imekuwepo tangu wakati wa chama kushika
hatamu. Kwa mantiki hiyo, karibu kila Mtanzania, kabla ya mfumo wa vyama vingi alihesabiwa ni mwana CCM. Kwa wakati
huu, watu wana uhuru wa kuamua kwa sababu wana-ma-chaguo, vyama ni vingi. Sitoshangaa aliye CCM kwa miaka yote
anapoamua kwenda chama cha upinzania iwapo amejiridhisha katika hilo. Asiulizwe: "ulikuwa wapi miaka yote 20 ya
mfumo wa vyama vingi, mbona hukujiunga nasi tangu wakati huo?"
Tatizo nilionalo huko mbele ni kuwa wanaunda CCM ndani ya CHADEMA. Sina hakika watadhibitije hili na hasa watawafanyia nini wale wanachama wao waliokwishapita kwenye kura za maoni?Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?
Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?
Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...