Swali kuhusu taasisi ya elimu ya watu wazima

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
4,471
11,367
Habari wakuu,

Jana nilipokuwa nasikiliza vipindi vya redio clouds fm nilisikia kuhusu taasisi ya elimu ya watu wazima, nikawa nimevutiwa kwa sababu kuna vijana wengi mtaani wanahitaji kupata elimu ile hali waliikosa walipokuwa wadogo. Hivyo ningependa kupata ufafanuzi zaidi kuhusu mambo yafuatayo;

a.taasisi hii ni ya kiserikali au ya kibinafisi?
b.ipo wapi hasa, au matawi yake yapo wapi?
c.usajili wake unafanyikaje na ni vigezo gani vinafatwa?
d.ada zake zipoje na mfumo wa kulipa ujoje?
 
Hii taasisi ilikuwepo tangu Enzi za Mchonga, wakati wa ujamaa ilikuwa na nguvu Zaidi. Ninakumbuka Enzi za vijiji vya ujamaa, baada ya shughuli za shambani, jioni wazee walikusanyika kufundishwa kusoma na kuandika na walimu wa taasisi hizi. Pia kulikuwa na vitabu vingi sana vya ukulima bora wa karibu kila zao.
 
siku hizi hiyo tasisi sio yawatu wazima kama unavyo sikia hata watoto waliyo maliza darasa la saba mwaka huu harafu hawakuchagulia na shule za serikali wanajiunga ndowame jaa tena wako kibiashara zaidi sio kama enzi zile. wana tawi kila mkoa na Wilayani kuna vituo vyao
 
Kama unataka kukifahamu hiki chuo nenda Dar es salaam eneo la posta Karibu na MAKTABA KUU YA TAIFA Lakin kumbuka hiki chuo ni cha serikali
 
Back
Top Bottom