GE2025 Swali Kabla ya Oct. 29: Waandamane au Wasusie Kura ya Urais?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,092
Reaction score
43,265
Na. M. M. Mwanakijiji

Oktoba 29, 2025 yaweza kuwa siku itakayoamua mwelekeo wa demokrasia katika Tanzania. Siku hiyo inaweza kuamua yale yatakayoendelea kutokea katika nchi yetu kuanzia Oktoba 30 na kuendelea kwa miaka mingi ijayo. Tukio moja limepangwa na huwa linatabirika; Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Hivyo, uchaguzi huu wa Oktoba 29, utaamua wale wanaoenda kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo hadi Oktoba 2030. Tukio hilo jingine limepangwa lakini halitabiriki (wengine tunafikiri linatabirika tukielewa hula ya Watanzania)

Uchaguzi wa mwaka huu kwa namna yake ni wa kipekee sana. Kwanza ni wa kihistoria mara tatu kama siyo zaidi. Upande mmoja ni wa kihistoria kwa sababu kwa mara ya kwanza mgombea wa Urais ni mtu aliyewahi kuwa Makamu wa Rais ambaye alirithi kiti cha Urais baada ya Rais aliyeko madarakani (John Magufuli) kufariki dunia. Hivyo ameweza kuwa Rais kwa kurithi na si kwa kupigiwa kura. Hili halijawahi kutokea nchini.

Ni wa kihistoria vile vile kwa sababu mgombea huyo Bi. Samia Suluhu Hassan ambaye tayari alikuwa ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Urais anaenda kuwa historia ya kuwa mgombea wa Urais wa chama tawala. Tayari tumeshawahi kuwa na wagombea Urais wanawake huko nyuma wa vyama vingine vidogo lakini hii ni mara ya kwanza Chama cha Mapinduzi kimemsimamisha mwanamke kugombea Urais. Hii ni historia kubwa.

Lakini pia ni uchaguzi wa kihistoria kwa namna fulani mbaya. Kwa mara ya kwanza tangu kurudiwa kwa mfumo wa vyama vingine, kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini amewekwa jela na chama chake kuvurugwa. Toka kusimamishwa kwa Mrema huko nyuma 1995 hadi hivi sasa vyama vya upinzani vimeweza kuwasimamisha wagombea Urais wenye majina makubwa na kutoa upinzani wa kweli kwa CCM. Uchaguzi wa Mwaka huu Rais Samia hana upinzani wowote wa maana na hivyo kuhakikishwa ushindi mkubwa tu. Hata kampeni anazofanya kwa baadhi ya watu zinaonekana si za lazima kivile kwani anaweza kushinda bila hata kushindana kweli kweli.

Ukweli wa jambo hili unafanya tarehe 29 Oktoba kuwa ya muhimu kwa wale ambao wanaamini katika mwendelezo wa sera na utawala wa Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia. Hivyo, watu wanaotaka Tanzania iendelee katika mwelekeo ule ule wa sasa hawana budi na ni lazima waende kumchagua Rais Samia kwa kishindo Oktoba 29. Hili si la kihistoria ni la kujirudia. Hili linatabirika.

Upande mwingine ni kuwa Oktoba 29 imepangwa kuwa siku ya maandamano makubwa dhidi ya serikali. Hili halitabiriki. Maandamano haya yana malengo mengi lakini kubwa ni kupinga kile kinachoonekana kama ni uminywaji mkubwa wa demokraia na kukithiri kwa vilie vinavyotajwa kuwa ni vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu; ikiwemo kutoweka kwa watu, ukamataji wa watu kiholela na kuwaweka kizuizini na ukandamizaji wa vya vya upinzani nchini. Kubwa ya hili ni kitendo cha kuwekwa ndani wa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Bw. Tundu Lissu ambaye ametungiwa kesi yenye mwelekeo wa kisiasa ya uhaini. Kwa maoni ya wengi kesi hii ilitungwa kuhakikisha kuwa Lissu hawi mgombea wa Urais dhidi ya Samia.

Mipango ya maandamano haya yanafanywa zaidi kupitia mitandao ya kijamii na kama ukipata nafasi ya kusikiliza Watanzania kwenye mitandao hiyo unaweza kuamini kabisa kuwa siku hiyo mambo yatakuwa motomoto. Kwa kutumia mitandao ya kijamii Watanzania wanahamasishana kujitokeza kuandamana na wengine wanataka hata kuiga mambo yaliyotokea kwenye nchi nyingine hivi karibuni.

Hivi karibuni kumekuwa na maandamano ya wale wanaoitwa ni Gen Z. Hiki ni kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya miaka 1997-2012. Kwenye nchi mbalimbali kizazi hiki kimekuwa kikitumia mitandao ya kijamii kujipanga kupinga serikali mbalimbali duniani. Hadi hivi sasa tumeona maandamano dhidi ya serikali yakiongozwa na kizazi hiki huko Kenya, Nepal, Madagascar, Morocco, Indonesia na Peru. Kubwa katika madai ya vijana hawa ni ile kuona kutokuridhika na mazingira ya kiuchumi katika nchi zao na matumizi mabaya ya madaraka kwa watawala.

Katika Tanzania tunaona lipo kundi la vijana ambao wamechoka kuona kuwa ile keki ya taifa inaendelea kutafunwa na kugawanywa miongoni mwa wale ambao tayari wana jiko la kutengeneza keki hiyo! Kwamba, mafanikio ya kimaisha yanendelea kurundikwa katika mikono ya kundi la watu wachache katika taifa, watu ambao wameshikamana na wale walioko madarakani. Bila kujisogeza karibu nao (uchawa) nafasi yako ya kufanikiwa inaendelea kuwa finyu na finyu zaidi.

Hivyo, wito wa maandamano kuelekea Oktoba 29 utaamua kama kweli Watanzania wamechoshwa na hali hii au la. Hata hivyo, jaribio la maandamano linaweza kuwa ni jaribio ambalo kufanikiwa kwake kunaweza kuwa kugumu zaidi. Watnazania - kwa maoni yangu - hawajafikia bado mahali pa nchi kama Kenya, Nepal, Madagascar au Indonesia. Bado hatujaona ugumu wa maisha wa kusababisha kweli watu wajitoe muhanga.

Hawa Watanzania wanaoimba kwenda kuandamana ndio hawahawa wanaotaka waende wakale nyama choma jioni, wapate moja moto moja baridi, na ndio hawahawa wanaotaka wasisumbuke. Na ukweli ukisemwa ni kuwa Rais Magufuli aliweza kulinyosha taifa na watu hawa hawa walikuwa wanalia kila siku! Na kinachoudhi ni kuwa wapo wengine wanataka eti jeshi lishike madaraka; yaani, wanataka njia ya mkato ya kuleta mabadiliko! Kama watu hawa walilia wakati wa JPM chini ya utawala wa kijeshi hawa watakimbia.

Kwangu mimi swali kubwa ni hili: Watu waandamane kupinga serikali kweli na kusababisha kushindwa kufanyika uchaguzi hadi walazimishe jeshi liingie madarakani na hivyo kumzuia Rais Samia kuwa Rais au kuamua kususia uchaguzi wenyewe na kutokujitokeza kupiga kura? Je, watu wengi wakisusa kupiga kura wale wachache watakaoenda kupiga kura wataweza kumuingiza Rais Samia madarakani kwa kuwa chache zaidi kuliko Rais mwingine yeyote katika historia ya nchi yetu?

Je, kwa kususia uchaguzi wa Rais - watu wanaweza kupiga kura kumchagua mbunge au diwani wao lakini wakaharibu kura za Rais yawezekana ikawa ndio njia bora zaidi ya kuandamana kuipinga serikali?

Inawezekana ukimya wa kutokupiga kura unaweza kupiga kelele kubwa zaidi kuliko maandamano.

Niandikie: klhnews@gmail.com
 
Mzee mwanakijiji bandiko zuri...

Swala la maandamano tarehe 29 ni la kimkakati sana.

Kama fujo za maandamano zitafika saa 8 mchana, maana yake Ratiba ya uchaguzi itakuwa imevurugika, uchaguzi hautafanyika tarehe 29... Baada ya hapo tutakuwa na swali la uhalali wa Samia....

Hapo ndio utaona unafiki wa CCM watakavyotoka wengi Samia asiendelee
 
Tukisusia na voters turnout ikiwa below 40% uhalali wa CCM kuongoza nchi unapotea.
Hakuna kitu kama kususia. Hata ajitokeze Samia na mwanaye mtaambiwa turn out ilikuwa 90%.

Kuna watu watasombwa na kulipwa kwa ajili ya publicity na kupiga picha za kusambaza kuonesha foleni refu la watu wakisubiri kupiga kura. Mkakati huu ushaanza. Watu wa ajili ya picha na mipango ya kusambaza kuonesha mwitikio wameshapatikana.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hivyo, wito wa maandamano kuelekea Oktoba 29 utaamua kama kweli Watanzania wamechoshwa na hali hii au la. Hata hivyo, jaribio la maandamano linaweza kuwa ni jaribio ambalo kufanikiwa kwake kunaweza kuwa kugumu zaidi. Watnazania - kwa maoni yangu - hawajafikia bado mahali pa nchi kama Kenya, Nepal, Madagascar au Indonesia. Bado hatujaona ugumu wa maisha wa kusababisha kweli watu wajitoe muhanga.
Mkuu Mzee Mwanakijiji , kwanza nimefurahi kukuona tena leo, baada ya kukusoma kule kwa Mwajuma Post in thread 'Kama siyo CHADEMA wala CHAUMMA - Twendeni na MWAJUMA?' Kama siyo CHADEMA wala CHAUMMA - Twendeni na MWAJUMA?

Huu ndio ukweli Mzee mwenzangu , 29 October hakuna maandamano yoyote wala machafuko yoyote Thread 'Watanzania ni watu wa maneno maneno, kupiga kelele na kulialia tuu, Tukija kwenye Vitendo ni sifuri, 0, zero, nil, hamna kitu!. Je Tutabadilika?' Watanzania ni watu wa maneno maneno, kupiga kelele na kulialia tuu, Tukija kwenye Vitendo ni sifuri, 0, zero, nil, hamna kitu!. Je Tutabadilika?

October 29 ni watu kujitokeza kwa wingi kwenda kutiki tuu!
P
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , kwanza nimefurahi kukuona tena leo, baada ya kukusoma kule kwa Mwajuma Post in thread 'Kama siyo CHADEMA wala CHAUMMA - Twendeni na MWAJUMA?' Kama siyo CHADEMA wala CHAUMMA - Twendeni na MWAJUMA?

Huu ndio ukweli Mzee mwenzangu , 29 October hakuna maandamano yoyote wala machafuko yoyote Thread 'Watanzania ni watu wa maneno maneno, kupiga kelele na kulialia tuu, Tukija kwenye Vitendo ni sifuri, 0, zero, nil, hamna kitu!. Je Tutabadilika?' Watanzania ni watu wa maneno maneno, kupiga kelele na kulialia tuu, Tukija kwenye Vitendo ni sifuri, 0, zero, nil, hamna kitu!. Je Tutabadilika?

October 29 ni watu kujitokeza kwa wingi kwenda kutiki tuu!
P
Pascal Mayalla tutakodi hata Macenerries
 
Back
Top Bottom