Swali gumu. . . . . . .!!

@ madame x ,umefafanua kuhusu kuzini nimekuelewa,kucheat je?
 
Mathematically: Cheating = (Adultery)2. Yaani mahawara (wazinifu tayari) wanapozini nje ndio wanaita cheating, katika kujihalalishia ile dhambi yao ya awali.
 
Mh!Kuna ukakasi hapa,sijajua kama nimekuelewa!
Naona sio suala la concept, ni suala la msamiati wenyewe.
Kuzini= to fornicate
(kushiriki tendo la ndoa na mtu ambae sio spouse wako. kama hujaoa basi kila ukisex unazini, hata kama ni yule mmoja tu)
To cheat = Kusaliti
(una mtu tayari mme/mchumba, then unaenda na mngine tena. hapa anaweza kua mtu wa ndani au wa nje ya ndoa)

Kusaliti ni aina ya kuzini. unaweza kuzini bila kusaliti, ikiwa unasex na mtu nje ya ndoa, but hakuna mtu mngine maishani mwako.

Kwa maelezo mengine msome vizuri Erick. anapatikana counter ya juu na babu yake Asprini.
 
eiyer angalia post za Mnyama Hatari kwenye sredi ya All Men cheat, agree or Disagree.

Siwezi angalia page, mchina wangu haruhusu

Nimeiona na ndo ikabidi nijiulize zaidi kuhusu haya mambo?
 
So kwa mujibu wako ni kuwa,same action different label?

Dah Elyer futa jibu lako kichwani then anza kuchukua ya wanajamii...
Hazifanani....kwa kuwa application zao zinatifautiana....
Kimoja ndani ya ndoa na nyingine both
 
@ RR,nimekuelewa kidogo,but ukiwa una mke halafu ukawa na mwanamke mwingine utakua unacheat au unazini?Je haya yanaweza kutokea kwenye action moja?Halafu umesema kua unaweza kucheat bila kuzini,kivipi?
 
Dah Elyer futa jibu lako kichwani then anza kuchukua ya wanajamii...
Hazifanani....kwa kuwa application zao zinatifautiana....
Kimoja ndani ya ndoa na nyingine both

Hebu niambie ipi both?
 
Mathematically: Cheating = (Adultery)2. Yaani mahawara (wazinifu tayari) wanapozini nje ndio wanaita cheating, katika kujihalalishia ile dhambi yao ya awali.

Maswali yameongezeka hapa!Hebu fafanua post yako hii!
 
@ RR,nimekuelewa kidogo,but ukiwa una mke halafu ukawa na mwanamke mwingine utakua unacheat au unazini?Je haya yanaweza kutokea kwenye action moja?Halafu umesema kua unaweza kucheat bila kuzini,kivipi?
Kinacho kuchanganya ni lugha. tuongee lugha moja. Kiingereza tu, au kiswahili tu. mi nachagua kiswahili. hapa tunajadili kuzini na kusaliti. najibu swali zako sasa:
1. unaweza kuzini bila kusaliti ikiwa unamahusiano ya nje ya ndoa na mwanamke mmoja tu. huna ndoa nae wala na mtu mngine wowote, na hujawahi kumsaliti. hapo upo katika hali ya kuzini ila hakuna unae msaliti.
2. sijasema unaweza kusaliti bila kuzini, nimesema unaweza kuzini bila kusaliti (hapo juu). Ila kusaliti bila kuzini kunaweza tokea pia: Kama ukimkiss mwanamke A, wakati upo katika mahusiano na B, ila unamkiss A bila kukutana nae kimwili, utakua umemsaliti mpenzi wako B bila kuzini na A. Kuzini kunahusisha tendo la ndoa.
 
@Russin and Elyer....

Hapa shida tuliyonayo ni maana ya CHEAT....
Je ni kufanya mapenzi bila kuachana na mpenzi/mke au mume?
Je ni kumsaliti mazima na ahadi kuvunjika?
Au ni kutoka kidogo na kurudi huku ukimuaminisha mwenzio kuwa wewe mwaminifu??
Hapa tukielewana mgogogo wa Elyer utaisha
 
@Erick52,maswali yako yakijibiwa tunaweza angalau kupata mwanga!
 
RR,

Naona umejitahidi sana kutoa shule ya bure....Mie sikujua kama haya mambo yanaweza kuwa na mkanganyiko wa aina yoyote...Ila kwa jinsi watu wanavyoeleza, inaonekana kuna watu wana kwama mahali!!

Kwenye cheating...umenikumbusha mzee mzima Bill Clinton...alizidiwa uzalendo aka-cheat na mrembo Monica ila hakuzini naye!!

... Uzuri jamaa zetu kwa ujumla hazina matatizo sana na uzinzi+uasherati ila, wanakuwa wakali sana kwenye mambo ya usaliti!!

Babu DC!!
 
@RR
Bora umekuja, naona wengi wataelewe maana halisi ya cheating na nani anacheat.

Issue ya jana ni hii
Mimi sijaolewa ninatoka na mume wa mtu (ndiye nina commitment naye); na sina commitment na mtu mwingine yoyote zaidi ya huyo married man. Do l cheat? Najua si vizuri na bla bla zake, swali ni do l CHEAT?
 
Huyo dada hafanyi cheating (usaliti) yoyote kwani hana mtu anayemrusha roho...Ila huyo mume wa mtu anamcheat mke wake....

Kwa vile amekiri kuwa si vizuri na kwamba anapenda kuwa committed basi agentafuta wake aachane na ku-share mume wa mtu!!

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom