Swali gumu....Lakini linajadilika

Mimi nafikiri si sawa kuwe na ruksa ya haya mambo. Lakini jamani kitu cha muhimu ni kujichunguza kwanza sisi walezi, wazazi na jukumu letu zima la kulea watoto wetu katika maadili yanayotakikana na yaliyo sahihi. Kamwe tusitegemee ustawi wa jamii walas erikali kwani sisi yenyewe ndio ustawi wa jamii na sisi wenyewe ndio serikali.
Mtoa mada anachokiongelea ni kweli kabisa kuwa tunajua kuwa haya yanatendeka tunayafumbia macho tu, kuna haja ya kuyachukulia hatua ili kunusuru vizazi vijavyo badala ya kuwaachia TACAIDS na Muhimbili kama vile inawahusu wao tu. TACAIDS wao watakuwa concerned na jinsi vitendo hivi vinavyochangia ongezeko la UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa. Imefika wakati sasa wasomi wetu wa nchi waanze kututumikia japo kwa kufanya tariti za kina za namna ambavyo tabia hizi zinachipukia, enezwa na ikiwezekana watupe recommendations za namna ya kuzizuia zisiendelee kuwepo na watuhabarishe wananchi wote madhara ya tabia hizo kisha tuungane kutokomeza lakini kusema tu Iruhusiwe au isiruhusiwe ni kupaka rangi nyumba chakavu.

Kujibu mada yako kagarama mimi kama mimi naomba isiruhusiwe na litafutiwe ufumbuzi wa kina.
 
mkuu hapa unakosea sana,mimi ni mwanaume sipendi taarabu lakini hapo zamani nilikuwa naenda kwenye kumbi za taarabu kufata totoz,huwa wanakuja totoz za ukweli wazazi wakijuwa eti kwenye taarabu ni 'safe'.<br />
Hamna kuhalalisha ushoga/usagaji waendelee hivyo hivyo kimyakimya kwa kujificha,tukianza kuwatambua itafuata ndoa za jinsia moja, kuasili watoto kwenye ndoa hizo za jinsia moja na hata kurithiana mali na vikorombwezo kibao,hamna kufungua mlango nusu.
mkuu huo ni ukweli. Kwenye show za taarabu huwa kuna matotoz ya ukweli. Yaani we acha tu, Hukosi wa kuopoa. Ila wapo wanaoenda kuopoa matotoz, na kuna wanaume wengine wanaenda eti kisa wanapenda miziki akina mama wa mipasho, aisee hao wanaume wanamapungufu.

Hamna kualalisha homo hapa nchini. Kama itakuwa inafanyika kisiri siri watajijua wenyewe. Ila hamna kuweka sheria ya kuwaruhusu.
 
Unajua
tatizo hili limeanzia Nchi za Ulaya na America. Na kama ambavyo sisi nchi za kiafrika tusivyo na msimamo na tabia ya kumuabudu mweupe,nahisi nchi hizi zikitulazimisha kuwatambua hawa watu lazima tutafanya tu.
Una hakika na ukisemacho ndugu? Fanya utafiti kwa kusoma an kudadisi.Kwa tarifa yako hizi tabia ziko na zimekuwepo toka enzi na enzi ila zilikuwa siri na jamii ilikuwa na mfumo kuzifunika maana ni tabia zisizokubalika kijamii.Waafrika - wakiwemo Tanzania ni tabia ziko miaka na karne. Unataja wamarekani Ulaya...Mbona umesahau waarabu na waasia?


Na ninasema hayo nikiwa nina uhakika na kile ninachoandika. Mfano AU imeshindwa kuzuia USA na NATO kuivamia Libya. Tutaweza suala dogo kama hilo?
Bado nasisitiza huna uhakika! Usilinganishe boga na jiwe.Huo mfano wako una walakini nahauwezi kuitegemeza hoja yako ya awali.
 
Hakuna haja ya kupitisha sheria ya kuhalalisha ushoga au ndoa za jinsia moja. Tunaweza kutafakari kwa kina na kutafuta suluhisho la hili tatizo.
 
Kwanza mimi siyo shoga.... Mimi nawajua mashoga kibao na pia Rafiki yangu aliwahi kumfumania mkewe anayefanyakazi pale "Long Room" akisagana na mwenzie anayefanyakazi TIB. kwa hiyo tusijibaraguze, ushoga upo na usagaji upo pia.

Sijui ni wasichana wangapi siku hizi Tigo zao zimesalimika!!
Hilo swali aulizwe papaaaa MS@#%&>,e'anaweza kuwa na jibu
 
ukifuatilia kwa makini habari zinazochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini tabia za ushoga na usagaji zinazidi kushika kasi. siku hata siku.

Jee kuna haja ya serikali kupitisha sheria zitakazoruhusu mahusiano haya yawe halali kisheria?

Swali gumu mie nikategemea swali kuhusu solution to a stable, long lived WIMP borne of a supersymmetric Grand Unified Theory, cure of cancer or reconciling the 26 spatial dimensions of string theory with the multiverse, or even better Einstein's "action at a distance" spookiness.

Nakuja kuambiwa habari ambazo ni function of socio-cultural systems?

Sioni swali gumu.

Mahusiano ya watu waliofikisha majority age yawe juu yao, na si kazi ya serikali.

Swali hapa sio whether or not ushoga uhalalishwe kisheria na serikali, swali ni kwa nini unafikiri serikali ina haki ya kuwaingilia watu wazima wawili wanaoamua kuishi kishoga.
 
ukifuatilia kwa makini habari zinazochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini tabia za ushoga na usagaji zinazidi kushika kasi. siku hata siku.

Jee kuna haja ya serikali kupitisha sheria zitakazoruhusu mahusiano haya yawe halali kisheria?

Swali hili linaulizwa na mhusika nini? Mjadala huu haufai hata kidogo
 
Swali hili linaulizwa na mhusika nini? Mjadala huu haufai hata kidogo
usiwe mwoga wa kujadili mambo mazito kwa kudhani watu watahisi wewe ni mhusika. Ukifika Magomeni na Kinondoni mashoga na wasagaji si wakutafuta wamejaa kibao. wewe wa wapi ndugu yetu unayeogopa mambo ya kimji.
 
ukifuatilia kwa makini habari zinazochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini tabia za ushoga na usagaji zinazidi kushika kasi. siku hata siku.

Jee kuna haja ya serikali kupitisha sheria zitakazoruhusu mahusiano haya yawe halali kisheria?

usagaji unasababishwa na uongozi mbaya ndio maana maadili yanavunjwa kila sehemu tujitahidi kufanya maombi kwa kweli..
 
huwa hairuhusiwi kujadiliwa na zaidi nikuwapa onyo kali wanaowapumulia kwenye vichogo wenzao..
 
Back
Top Bottom