Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,447
Zamani sana bendi moja hapo Dar: ama Dar es salaama Jazz au Western Jazz iliimba kuwa "Tenda Wema, nenda zako, usingoje shukurani". Maudhui ya wimbo huu yamesharudiwa na waimbaji wengi sana siku za hivi karibuni.
Mimi ni mtu wa makamo sana wakati huu na katika maisha yangu nimeshasaidia watu wengi sana, jambo ninalojivunia mno. Kila msaada ninaotoa huwa ina maana ya mimi na familia yangu kujinyima ili tuwasaide wengine, siyo kwamba huwa nina dimbwi kubwa la pesa za kuchota bure bure bure.
Sasa kinachonishangaza ni kuwa ndugu na marafiki wengi niliowahi kusaidia huwa hawaonyeshi shukrani yoyote ukilinganisha na wale ambao huwa sina uhusiano nao. Ndugu na marafiki huwa wanataka zaidi wala hawawezi kutosheka na msaada, na ikitokea nikasema sasa msaada niliokwishatoa unatosha inabidi ajiendeleze mwenyewe, basi wananilaumu kama vile kile nilichokwishawafanyia siyo kitu kabisa. Yaani wanakuwa wananiongea vibaya tu bila shukrani yoyote.
Ni wapi ninapokosea katika kusaidia ndugu na marafiki ili watambue msaada wangu kwao?
Kuna mmoja nilimlipia mtoto wake kwa miaka minne mfulizo chuo kikuu cha dar es salaama wala hakuchukua mkopo wa serikali, akamaliza na 3rd class.
Sasa mtu huyo ananilaumu kwa nini simsaidii mtoto huyo kusoma masters! Kibaya anatumia lugha mbaya kuwa nina wivu sipendi watoto wake waendelee kama mimi wakati bado ninasaidia mtoto wake mwingine ambaye yuko sekondari ninayomlipia mimi!!