Ni kwanini tukienda kusalimia kwa ndugu zetu huwa tunachokwa tukikaa muda mrefu?

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,835
Habari za asubuhi wanajukwaa, natumaini tumeamka salama salimini, binafsi huwa naamka saa kumi kamili kuoga na kuvaa saa kumi na moja kamili asubuhi nipo eneo la kazi huwa narudi nyumbani usiku wa saa sita au saa saba, na hii ndiyo daily rooten. Nawasihi vijana wenzangu tupambane mpaka maumivu ya mwisho kwani umasikini ni mbaya sana.

Ndugu jamaa na marafiki ni sehemu ya watu muhimu sana katika maisha ndiomana tunashauriwa kukumbukana na kusaidiana bila kuchokana. Ila Kuna upuuzi umejengeka sio mzuri mimi ni miongoni mwa vijana ninaependa sana kusalimia nyumbani kwa majirani, ndugu na marafiki ila Kuna kitu huwa nakiona hakipo Sawa

Unakuta umekaa mara ya kwanza wanakukaribisha kwa fujo na nderemo Meno 32 na maneno juu utasikia tumekumisi kweli tabia ya kukaa mda mrefu bila Kuja kutuona hatupendi, basi utaandaliwa kuku pale, kesho samaki, kesho kutwa mbuzi choma.

Lakini siku zinavyozidi kwenda umuhimu wako walivyokuwa wanakujali unapungua kabisa. Halii hii huwa inanikwaza sana inafika wakati tutakata tamaa ya kutembelea ndugu zetu. Wote wanakuacha peke ako uko sebleni tofauti na mwanzo ulikuwa una full kampani. Mwishowe tusipofika utasikia umetususa.

Hali hii nimeshuhudia kwa dada angu, mjomba, mtoto wa mjomba wangu, mtoto wa baba mdogo tena huyu hana busara kabisa za kujali wageni. Anyway Leo naondoka hapa kwa dada nikiwa na hasira sana sita rudi tena maana akufukuzae hakuambii toka. Mwanzo unapewa Maandazi Matano mpaka sita saizi unapewa Mawili ukizubaa anakuja tena kukata hilohilo andazo ulilopewa anampa mtoto wake anayemnyonyesha. Kebehi Kwangu Mwiko niombeeni nifike jiji la Dar Es Salaam salama salimini asanteni great thinkers.
 
Habari za asubuhi wanajukwaa, natumaini tumeamka salama salimini, binafsi huwa naamka saa kumi kamili kuoga na kuvaa saa kumi na moja kamili asubuhi nipo eneo la kazi huwa narudi nyumbani usiku wa saa sita au saa saba, na hii ndiyo daily rooten. Nawasihi vijana wenzangu tupambane mpaka maumivu ya mwisho kwani umasikini ni mbaya sana.
Safari njema
 
Hivi huo ujinga wa kusalimia watu ni wa nini? Mbona me huwa siendi kwa ndugu yoyote naishi maisha yangu

Tafuta hela jenga kwako ishi maisha yako kula vizuri kunywa nje na usafiri wako katembelee wanyama huko hifadhiñi rudi kwako

Maisha kwenda kutafuta kwa ndugu siwezi

Hata ningekua nasoma mzazi aniambie analipa tu ADA vile kuna ndugu karibu et nikakae kwake ni bora nisisome
 
Kwa sababu mnakaa muda mrefu mpaka mnasahaulika akilini mwa ndugu, jamaa, marafiki. So, mkienda mnawahi kuboa tu, hasa ukiongezea kwamba mnashuka pale home kwa majidai na mikogo ya Kihaya :)
 
Mimi siwapangii maisha yao
 
Back
Top Bottom