Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Mengi Uliyoandika hapa ni uongo mtupu.
 
Haiwezekani kuimaliza Russia bila kuweka usalama wa dunia nzima hatihati. Ukisha kuwa nuclear power to the level of Russia lazima uheshimiwe duniani bila ya kujali uchumi wako upo level gani.
Hata Kiduku wa Korea Kaskazini anaheshimiwa
 
Umeelezea kitaalamu sana mkuu.
Kudos.
 
Umeelezea kitaalamu sana mkuu.
Kudos.
Braza unachanganyikiwa kusikia ukweli, NATO ni kikundi cha wahuni, wahuni, wahuni watupu.
Ona sasa Ukraine yaliyompata, mpaka aje akomboe majimbo mawili ya donbase ni lini? Nato wameshindwa kuingia zaidi ya kutuma silaha uchwara.
Kiuchumi anawalizimisha Europe yote wanunue gas yake kwa ruble. Pesa ya urusi imeimarika dhidi ya dollar katikati ya vikwazo, maajabu!
 
Usipoangalia tarehe unaweza kusema uzi umeandikwa kutokana na kinachoendelea hivi sasa, kumbe ni uzi wa kitambo na lazima timu USA/Russia itakuja kichwa kichwa kwenye huu uzi
 
Hivi huwa mnatafakari madhara ya NATO kwenda frontline au huwa mnakurupuka kutoka vijiwe vya kahawa?
Nato ikiingiza pua ni vita ya ww3
 
Safi sana,namba 2 ndio kinachotokea sasa hivi huko Ukraine. Oligarchs wanateketeza Wanajeshi wa Russia kwa maslai yao binafsi.
 
Wasichokijua Wengi Kuwa Urusi ni taifa tajiri kinishati na kiteknologia..

Bila gesi ya Urusi chi nyingi za Ulaya watu watakufa kwa baridi, mfano Italia inategemea Gesi ya Urusi kwa asilimia 80%
 
Hiyo point namba 2 na 3 tunazishuhudia kwa Sasa, uhalifu unaofanyika huko Ukraine na utitiri wa utajiri wa hao Oligarch walioweka huko Ulaya na Marekani inaonyesha Urusi ya Sasa imetekwa na genge dogo la wahuni.
 
Kabla ya Ugunduzi na kuanza kuchimbwa wa gesi ya Urusi mwaka 1970 Nchi nyingine za Ulaya zilikuwa zinaishije na kwa nini watu wa huko hawakufa kwa Baridi?

Muwe mnashirikisha akili zenu kabla ya kubwatuka.
Wasichokijua Wengi Kuwa Urusi ni taifa tajiri kinishati na kiteknologia..

Bila gesi ya Urusi chi nyingi za Ulaya watu watakufa kwa baridi, mfano Italia inategemea Gesi ya Urusi kwa asilimia 80%
 
Sio tuu urusi sikuhizi majeshi mengi mdebwedo, Jeshi strong limebaki kuwa la Uchina... ndio maana America wanawekeza kwenye vifaa .. ulaya yote, majeshi yote mdebwedo. Hata huku BNG coplo ameota kitambi
 
Ni vyema ungedadavua, hili taifa linamsumbua Marekani kivipi na katika nyanja ipi? Uchumi? Technology? Nguvu ya ushawishi? Ama una maanisha nini. Hapo sijapaepewa mkuu. Weka mambo sawa.
Kweni wewe hujui kama hii vita inavyo endelea ingekua ni Africa au nchi za kiaarabu, US angesha ingia Kwa miguu yote na kuchakaza watu ipasavyo, lakini Kwa Russia anaishia maneno, hiyo ndo maana ya mtoa mada
 
Safi kabisa, binafsi namuunga mkono Putin mwenye spirit ya ki Magufuli, huwezi kua Rais unaye tingishwa hovyo hivyo tu na watu wasio kuhusu
 
Kabla ya Ugunduzi na kuanza kuchimbwa wa gesi ya Urusi mwaka 1970 Nchi nyingine za Ulaya zilikuwa zinaishije na kwa nini watu wa huko hawakufa kwa Baridi?

Muwe mnashirikisha akili zenu
hilo Swali ukiingia Google utapata jibu, Nchi za Ulaya zilikuwa zinatumia nisahati ya maakaa ya mawe

makaa ya mawe yanaharibu mazingira,wakamua kubadilisha mfumo na kuaanza kutumia Gesi,..

Leo Wamerekani wameiomba Algeria kuuza gesi Ulaya,Algeria ni nchi yenye ishirikiano mkubwa na Urusi..

Juu ya vita vinavyoendelea,vikwazo walivyomuwekea Mrusi lakini bado wananunua gesi kutoka Urusi..

Hivi unajua kuwa Urusi ndio nchi kubwa Dunia kwa ukubwa wa Ardhi?
 
Kiuchumi ni ya ngapi?
 
unafikiri Urusi ingeweza kuhimili vita na Ulaya pamoja na Marekani,kama uchumi wake sio mzuri

Juu ya vikwazo walivyomuwekea mwamba kakamata uzi ule ule hajatetereka

Hivi umesikia kuwa raisi wa Ukraine kaomba po,kwa upande wangu huyu ni mmoja kati ya maraisi wapumbavu kabisa

Baada ya nchi yake kuharibiwa,wananchi wake kuwa wakimbizi kila kona ya Ulaya, sasa amekubali kuomba Neutrality..
 
Wasichokijua Wengi Kuwa Urusi ni taifa tajiri kinishati na kiteknologia..

Bila gesi ya Urusi chi nyingi za Ulaya watu watakufa kwa baridi, mfano Italia inategemea Gesi ya Urusi kwa asilimia 80%
Halaf kwenye hili saga ITALY sijamsikia kabisaaa cjui atakuja kusema nn
Najamaa UCHUMI wake ulivyokumbwa na purukushani hapa kati cjui itakuaje ama atakuja na nn
Acha tumngojee maana kawa kimya sanaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…