Swali fikirishi: Vyombo vya dola hufuata maagizo ya chama tawala au chama tawala hufuata maagizo ya vyombo vya dola?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Hivi chama tawala cha siasa kinaweza kufata amri ya chombo cha usalama( Polisi, Jeshi au Magereza) au chombo cha usamala i.e Polisi, Jeshi, Magereza ndo kinafata amri ya chama tawala cha siasa....?

Kulingana na kauli ya mwalimu??
1473446942853.jpg

Comment ya Malcom Lumumba
Mzee alimaanisha Chama cha Upinzani kisichofuata amri ya vyombo vya dola vya CCM ni cha Kigaidi.
Hapa CCM haikuguswa kabisa kwasababu hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvitenga vyombo vya dola na CCM. Huu mfumo na hii laana inayotutesa sasa hivi Watanzania ilitengenezwa na Mzee Nyerere mwenyewe kwasababu zake anazozijua yeye.

Huyu Mzee alidiriki hadi kusema kwamba Chama kiko juu ya Serikali,
Serikali haiwezi kuwa na nguvu kama haikitii Chama Tawala, na hapa anaposema Serikali alikuwa anazungumzia Mihimili yote ya Serikali na vyombo vyote vya dola. Namnukuu hapa "Its not the Party that is an instrument of the Government, but the Government is an instrument of the Party from which the people have the mandate to rule their nation"

Ndiyo maana kuna baadhi ya mamboakiyafanya Raisi Magufuli sishangai kabisa,
Mzee Nyarere alishawahi hadi kudhalilishaMajaji na kuwatolea vitishi kwamba atawashughulikia na ameandaa dawa yao...
 
View attachment 702189

Ndiyo maana kuna baadhi ya mambo akiyafanya Raisi Magufuli sishangai kabisa,
Mzee Nyarere alishawahi hadi kudhalilisha Majaji na kuwatolea vitishi kwamba atawashughulikia na ameandaa dawa yao...
 
"Chama cha siasa kisichotii amri za vyombo vyetu vya usalama. Hicho ni kikundi cha kigaidi" Hii kauli inawahusu Chadema kwa asilimia nyingi tu.
 
Bahati mbaya sana hata CHADEMA hawako kabisa kwenye huu mfano,
Maana neno Ugaidi kwa lugha ya kiingereza ni Terrorism, sasa kwa lugha rahisi kabisa.
Terrorism "is the unlawful use of violence and intimidation, especially against civilians, in the pursuit of political aims"

NB: Sasa binfasi sijaona sehemu ambapo CHADEMA wanawatishia wananchi au wanatumia nguvu kinyume na sheria ili kufikia malengo fulani fulani ya kisiasa. Hapa kama una akili utakuwa ushaelewa kwamba nani ni Gaidi hapa nchini.
 
Tatizo la kimaadili ya madaraka ndani ya nchi hii linachangiwa na kifungu cha katiba kinachosema rais hatoshitakiwa akiwa madarakani au akitoka kwa kosa lolote. Hapa ndio ulipo mzizi wa fitina wa matatizo yote ya maadili ya kiungozi ndani ya nchi hii. Kifungu hicho na nguvu aliyopewa rais ya kuteua kila kiongozi wa mihimili ya dola, na ukizingatia ubinafsi wa viongozi watu na kujipendekeza, hapo ndio unaona mihimili yote ikiwa mateka wa rais ambaye ni zao la chama cha siasa. Jambo hili ndio limechangia kila kitu na maamuzi karibu yote ya nchi kufanyika kisiasa. Tukiweza kukitoa kifungu cha rais kushitakiwa akiwa madarakani au akitoka basi hapo mambo mengi yatafuata sheria bila macho.
 
Nyie ndio huwa mnafeli mitihani kwa kujifanya wajuaji sana. Hapo reference ni kauli ya Mwalimu Nyerere na siyo hizo tafsiri zako za wazungu.
 
Hivi chama tawala cha siasa kinaweza kufata amri ya chombo cha usalama( Polisi, Jeshi au Magereza) au chombo cha usamala i.e Polisi, Jeshi, Magereza ndo kinafata amri ya chama tawala cha siasa....?

Kulingana na kauli ya mwalimu??
View attachment 702189

Comment ya Malcom Lumumba
Mzee alimaanisha Chama cha Upinzani kisichofuata amri ya vyombo vya dola vya CCM ni cha Kigaidi.
Hapa CCM haikuguswa kabisa kwasababu hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvitenga vyombo vya dola na CCM. Huu mfumo na hii laana inayotutesa sasa hivi Watanzania ilitengenezwa na Mzee Nyerere mwenyewe kwasababu zake anazozijua yeye.

Huyu Mzee alidiriki hadi kusema kwamba Chama kiko juu ya Serikali,
Serikali haiwezi kuwa na nguvu kama haikitii Chama Tawala, na hapa anaposema Serikali alikuwa anazungumzia Mihimili yote ya Serikali na vyombo vyote vya dola. Namnukuu hapa "Its not the Party that is an instrument of the Government, but the Government is an instrument of the Party from which the people have the mandate to rule their nation"

Ndiyo maana kuna baadhi ya mamboakiyafanya Raisi Magufuli sishangai kabisa,
Mzee Nyarere alishawahi hadi kudhalilishaMajaji na kuwatolea vitishi kwamba atawashughulikia na ameandaa dawa yao...

Wote huwa wanafuatana kama Kumbikumbi tu Mkuu.
 
Tatizo la kimaadili ya madaraka ndani ya nchi hii linachangiwa na kifungu cha katiba kinachosema rais hatoshitakiwa akiwa madarakani au akitoka kwa kosa lolote. Hapa ndio ulipo mzizi wa fitina wa matatizo yote ya maadili ya kiungozi ndani ya nchi hii. Kifungu hicho na nguvu aliyopewa rais ya kuteua kila kiongozi wa mihimili ya dola, na ukizingatia ubinafsi wa viongozi watu na kujipendekeza, hapo ndio unaona mihimili yote ikiwa mateka wa rais ambaye ni zao la chama cha siasa. Jambo hili ndio limechangia kila kitu na maamuzi karibu yote ya nchi kufanyika kisiasa. Tukiweza kukitoa kifungu cha rais kushitakiwa akiwa madarakani au akitoka basi hapo mambo mengi yatafuata sheria bila macho.
Pamoja na hilo uliloliona kama mzizi wa fitna (Rais kutokushtakiwa) mbaya zaidi Chama hukimbilia kumpa uenyekiti. Kwa hiyo akiongea mambo ya chama huongea kama Rais vilevile. Kwa hiyo vyombo vya dola lazima vitakitiii chama hata kama maamuzi ni ya ki mami!!!
 
Mzee alimaanisha Chama cha Upinzani kisichofuata amri ya vyombo vya dola vya CCM ni cha Kigaidi.
Hapa CCM haikuguswa kabisa kwasababu hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuvitenga vyombo vya dola na CCM. Huu mfumo na hii laana inayotutesa sasa hivi Watanzania ilitengenezwa na Mzee Nyerere mwenyewe kwasababu zake anazozijua yeye.

Huyu Mzee alidiriki hadi kusema kwamba Chama kiko juu ya Serikali,
Serikali haiwezi kuwa na nguvu kama haikitii Chama Tawala, na hapa anaposema Serikali alikuwa anazungumzia Mihimili yote ya Serikali na vyombo vyote vya dola. Namnukuu hapa "Its not the Party that is an instrument of the Government, but the Government is an instrument of the Party from which the people have the mandate to rule their nation"

Ndiyo maana kuna baadhi ya mambo akiyafanya Raisi Magufuli sishangai kabisa,
Mzee Nyarere alishawahi hadi kudhalilisha Majaji na kuwatolea vitishi kwamba atawashughulikia na ameandaa dawa yao...
Halafu kuna watu wanamuona ni mtukufu wakati haya yanayotokea sasa ni matunda yake, japo kafa ila mti alioupanda unaendelea kuzaliana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Chama cha siasa kisichotii amri za vyombo vyetu vya usalama. Hicho ni kikundi cha kigaidi" Hii kauli inawahusu Chadema kwa asilimia nyingi tu.
Wakati anaongea hayo mfumo wa vyama vingi ulikuwepo? Maana enzi ya chama kimoja ilikuwa chama kimeshika hatamu mpaka kwenye majeshi yote kulikuwa na matawi ya CCM na pia huwezi kumuunga na jeshi lolote mpaka uwe na kadi ya CCM angalau hata ya vijana au UWT. Kiongozi wa chama mwenye majeshi alikuwa na sauti kuliko mkuu wa kambi, hata maofisini, mashirika yote ya umma walikuwa yana ofisi za chama.
Usikute haya aliongea enzi ya mfumo wa chama kimoja maana hata ukisomea uhasibu kulikuwa na somo la Siasa tena linasomeshwa kwa kiswahili ns lazima ufaulu ukifeli hupati cheti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom