Swali fikirishi, mabalozi wetu nchi za nje hawawezi kutangaza na mpaka hiyo kazi afanye mkuu wa nchi?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Taifa letu lina mabalozi sehemu mbalimbali nje ya taifa letu. Karibu nchi zote tulizo na mahusiano nayo mazuri tumeweka balozi.

Ofisi ya ubalozi huwa ni sehemu ya taifa letu huko nje. Kwa sheria za kimataifa ofisi ya ubalozi huko China mfano ni sehemu ya eneo la Tanzania lililopo China.

Mabalozi wanawasadizi na hata wao wanamajukumu mengi tu mojawapo ni kutangaza biashara za taifa letu ikiwemo utalii.

Swali, hivi kazi ya kutangaza utalii au biashara mpaka ifanywe na mkuu wa nchi wakati kuna mabalozi?
 
Back
Top Bottom